Msaada vijiji gani nipeleke dagaa wa Mwanza?

DOLA 100

Senior Member
Jul 17, 2023
174
265
Habari wakuu.

Nataraji kufanya biashara ya kuuza dagaa wa wakavu wa mwanza,Vijiji gani naweza kupeleka dagaa na nikawauza kwa bei ya jumla?

Ama hata isipokuwa kuuza kwa jumla ama reja reja?
Vijiji ama miji iwe Ni kuzunguuka ukanda huu wa ziwa na maeneo ya Tabora na Igunga ama ikishindikana hata popote kwenye soko.

Msaada wakuu.
 
Mkuu Gharama za kuwafikisha huko zinaweza kula faida?
Kutokea Mwanza?
Dagaa wa kavu.
Ushauri wangu Kama ndio unaanza.. Nunua dagaa kutoka kwa wavuvi huko visiwani Kisha nenda kauzie pale Mwaloni Kirumba Mwanza.
Unaweza uza kwa Bei ya Jumla au reja reja.. wanunuzi pale wapo.

My take:- Vijijini hasa huko sijui tabora, Katavi, sumbawanga na nk wahitaji na watuamiji wa hizo dagaa ni wapo na Ni wengi lakini hawana pesa (( Cash in hand hawana )) labda uende ukakopeshe.

Mjini (( Mwaloni Kirumba pale )) wahitaji (wafanya Biashara na watuamiji ) wote wapo na pesa pia wanazo tena cash in hand.. issue bageinini pawa yako katika Bei ya kuuzia.

Back to my Experience.
Nilikuwa naenda kuchukua dagaa tena wale fresh wanene wa jua moja.. kutoka kisiwa Cha GOZIBA.. Nusu nilikuwa nauzia pale Mwaloni Kirumba Mwanza, Mzigo mwingine nilikuwa naupeleka huko Kusini magharibi mwa Tanzania.. Vijiji Kama majimoto, chamalendi, Mamba, inyonga, usevya nk

Faida: Huko Vijijini kote nilikopita zaidi ya kujifunza ukomandoo sikuona faida zaidi ya kuuzia Kirumba Mwanza pale pale. Sababu pale mzunguko unakuwa chapu.
 
Mchawi ni usafiri, kuanzia Runzewe, Masumbwe, Ushirombo, Kahama, Kagongwa Isaka, Tinde dagaa ni dhaabu ya ziwani
Mkuu uliweza swala la usafiri Ina maana soko lipo?

Na je huko unaweza kujua Bei ya Gunia,ndooa ya lita 10,au Sado moja Ni Bei gani?
 
Ushauri wangu Kama ndio unaanza.. Nunua dagaa kutoka kwa wavuvi huko visiwani Kisha nenda kauzie pale Mwaloni Kirumba Mwanza.
Unaweza uza kwa Bei ya Jumla au reja reja.. wanunuzi pale wapo.

My take:- Vijijini hasa huko sijui tabora, Katavi, sumbawanga na nk wahitaji na watuamiji wa hizo dagaa ni wapo na Ni wengi lakini hawana pesa (( Cash in hand hawana )) labda uende ukakopeshe.

Mjini (( Mwaloni Kirumba pale )) wahitaji (wafanya Biashara na watuamiji ) wote wapo na pesa pia wanazo tena cash in hand.. issue bageinini pawa yako katika Bei ya kuuzia.

Back to my Experience.
Nilikuwa naenda kuchukua dagaa tena wale fresh wanene wa jua moja.. kutoka kisiwa Cha GOZIBA.. Nusu nilikuwa nauzia pale Mwaloni Kirumba Mwanza, Mzigo mwingine nilikuwa naupeleka huko Kusini magharibi mwa Tanzania.. Vijiji Kama majimoto, chamalendi, Mamba, inyonga, usevya nk

Faida: Huko Vijijini kote nilikopita zaidi ya kujifunza ukomandoo sikuona faida zaidi ya kuuzia Kirumba Mwanza pale pale. Sababu pale mzunguko unakuwa chapu.
Mkuu kwa hiyo biashara ipo hapo hapo Mwaloni?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom