Msaada unahitajika. Michongo miwili yote imetiki

Kaparare

Member
Apr 19, 2021
93
230
Iko hivi Kuna mdogo wangu alifanya interview sehemu mbili tofauti ya kwanza ni taasisi ya Fedha ya pili ni taasisi ya Afya na kote akafaulu vizuri.

Taasisi ya Fedha akaambiwa asubiri ataitwa baada ya kukumilisha hatua kadhaa ila kwasasa bado sio Muajiliwa japokuwa tayari mguu mmoja uko ndani.

Ile taasisi ya Afya nao wakamuita na ajira Yao ni ya mkataba wa Mwaka mmoja (renewable) dogo akasaini na yuko kazini sasa ana wiki mbili hivi.

My question is siku taasisi ya Fedha wakimuita AONDOKE vipi pale AFYA bila kuathiri chochote?

Je kufanya kazi mwezi mmoja na kuchukua ya Kujikimu na Mshahara itamletea shida?

Njia ipi Sahihi kuachana na hiyo ya mkataba na kwenda ajira ya Kudumu bila kuonekana msumbufu?

Naomba msaada wenu wa Mawazo na Ushauri.

Asanteni Sana
 
Mshika mawili........... Hapo lazima akubali kufanya kazi hii anayofanya Sasa maana yupo ndani ya mkataba. Kama anataka kuvunja mkataba arejee vigezo na masharti ya kazi yake Mara nyingi huwa Ni kurudisha mshahara wa miezi mitatu mbeleni wanapotafuta mbadala wake.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Alichokosea ni kusain mkataba, kama alikua ana plan za kuibukia chimbo lingine angeomba hata makataba wa miez3 kwa kutafuta sababu za hapa na pale.

Cha kufanya ni atafute sababu nzito either kufiwa au kupata matatizo hapo kusepa inaweza kua easy ila kinyume chake itamcost coz ya mkataba aliotia wino.
 
HUYO MDOGO WAKO NDIO WEWE KUMBE EEE

OKAY... CHAGUA MOJA KWA KUWA HUWEZI KUTUMIKIA MABWANA WAWILI KWA WAKATI MMOJA, NAMAANISHA MSHIKA MAWILI MOJA HUMPONYOKA
 
Kwani mkataba si una maelezo juu ya termination? Atafuata walivyokubaliana ktk mkataba
 
Akipata mwingine aangalie kwenye maslahi zaidi na mkataba mzuri.

Kuacha kazi mbona easy tu.... Si yupo probation huyo?

Akipata panono aandike barua ya kuresign asepe...
 
Mh kwanza inabidi umuambie mdogo wako anielekeze namna gani na mimi nitapata kazi.

Pili nafikiri ishu ya wapi pana maslahi mapana ndiyo inamatter ila pia kuondoka kazini mwezi tangu uajiriwe itakua siyo ishu sana kwakua huwezi jua lini utakutana nao huko mbele tangu uwatose.

So kwa maoni yangu kama hii finance inatoa mkataba wa kudumu basi aende huko ila kama ni renewable kama hapo alipo basi astick nao ili ajenge heshima yake.
 
Mshika mawili........... Hapo lazima akubali kufanya kazi hii anayofanya Sasa maana yupo ndani ya mkataba. Kama anataka kuvunja mkataba arejee vigezo na masharti ya kazi yake Mara nyingi huwa Ni kurudisha mshahara wa miezi mitatu mbeleni wanapotafuta mbadala wake.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Sheria ya kuvunja mkataba ni kutoa notisi ya mwezi mmoja kabla au kumlipa mwajiri mshahara wa mwezi 1, kwa mfanyakazi. Hiyo yako ya miezi 3 sijui umeipata wapi.

Na aliye probation ndani ya mwezi ni siku 7 tu au inategemea terms za mkataba wao.
 
Mwambie akavunje kwa sheria yako wakati vipengele vya mkataba amepewa na vinamaelezo yake.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ataandika barua ya kuacha kazi ndani ya masaa 24, baada ya hapo atatakiwa kuacha mshahara wa mwezi 1; wapo pia wanaotoka ajira ya kudumu kwenda mkataba, muhimu ni maslai tu
 
Ataandika barua ya kuacha kazi ndani ya masaa 24, baada ya hapo atatakiwa kuacha mshahara wa mwezi 1; wapo pia wanaotoka ajira ya kudumu kwenda mkataba, muhimu ni maslai tu
Mshahara wa Mwezi upi ?? Huu alioufanyia kazi (March) au April ambao ataamua kuacha kazi kama mwezi kuisha
 
Back
Top Bottom