Msaada: Ulaji mkubwa wa umeme kwa matumizi yale yale kwenye mita ya 3-Phase

coronath julius

New Member
Sep 18, 2018
2
2
Wadau naombeni msaada kwa hili jambo,,

Yaani siku hizi tangia wiki jana , ulaji wa umeme kwenye mita za 3phase umekuwa mkubwa mno.
Yaani, ukiweka umeme ambao kwa kazi ileile ulikuwa unatumia labda siku 4, siku hizi unatumia siku moja kwa kazi hiyohiyo unaisha.

Nimeleta mafundi wa umeme tofautitofauti kuniangalizia mfumo wa wiring na earth lakini wote wanasema mifumo yangu haina shida.
Nikajaribu kuwauliza na baadhi ya watu wanaotumia hizi mita za 3phase nao wakawa wanalalamika kwamba mambo yamebadilika.

Naomba kujua kama hili tatizo nilakitaifa kwamba serikali imebadili mfumo wa ulaji umeme kwakuwa vitu vimeoanda bei au mfumo umeyumba unarekebishwa hivyo tuwe watulivu??

Kwa mwenye mita ya 3phase na yeye anaweza kutushirikisha huko kwake hali ipoje
 
Mimi pia nimepata hiyo changamoto, nina 3 phase meter, umeme unaotumika kwa siku units zimeongezeka bila kuwa na matumizi ya ziada, sijajua kama ni TANESCO wamebadilisha rates kwa sisi wenye 3 phase au kuna shida gani. Pia nimeuliza mafundi umeme na wamecheck system ya wiring ya nyumba wanasema haina shida yoyote. TANESCO inabidi watupe maelezo kuhusiana na tatizo hili
 
Wadau naombeni msaada kwa hili jambo,,

Yaani siku hizi tangia wiki jana , ulaji wa umeme kwenye mita za 3phase umekuwa mkubwa mno.
Yaani, ukiweka umeme ambao kwa kazi ileile ulikuwa unatumia labda siku 4, siku hizi unatumia siku moja kwa kazi hiyohiyo unaisha.

Nimeleta mafundi wa umeme tofautitofauti kuniangalizia mfumo wa wiring na earth lakini wote wanasema mifumo yangu haina shida.
Nikajaribu kuwauliza na baadhi ya watu wanaotumia hizi mita za 3phase nao wakawa wanalalamika kwamba mambo yamebadilika.

Naomba kujua kama hili tatizo nilakitaifa kwamba serikali imebadili mfumo wa ulaji umeme kwakuwa vitu vimeoanda bei au mfumo umeyumba unarekebishwa hivyo tuwe watulivu??

Kwa mwenye mita ya 3phase na yeye anaweza kutushirikisha huko kwake hali ipoje
Tafadhali onesha namba ya mita na namba ya simu kwa maelezo sahihi
 
nachowependea TANESCO humu ndani hawachelewi kujibu changamoto za wadau hongera admin wa Tanesco hapa jf
 
Back
Top Bottom