Msaada: Tofauti kati ya DP World, TICTS na Hutchinson Port

Phamarcist

JF-Expert Member
Apr 18, 2021
211
449
Habari,

Wakati nchi inapitia vuguvugu la changamoto za kimkataba kati ya serikali yetu na kampuni ya DP WORLD. Na huku spin doctors wakijaribu kututoa kwenye reli nilikua naomba kufahamishwa yafuatayo.

Kuna tofauti gani kati ya kampuni ya TICTS ( Tanzania international container terminal service) na HUTCHINSON PORT OF TANZANIA,

Kwanini nimeuliza hivi, ni hivi TICTS ndiye aliyeingia mkataba na serikali ya Tanzania mwaka 2000 juu ya uendeshaji bandari kitengo cha makasha. Lakini kipindi chote hicho TICTS akiendelea na shughuli zake kuna kampuni ilionekana ndani ya TICTS ikiitwa Hutchinson port of Tanzania.

Kama kuna mtu aliwahi kupata zabuni yeyote enzi za TICTS basi atakua shahidi juu ya hili swala kwani kuna document zilizotoka TICTS lakini zikiwa zimepitishwa na Hutchinson port.

Swali la pili, ikitokea DP WORLD wakaanza kazi rasmi je, Hutchinson port wataendelea kuwepo kama walivyokua wakifanya kwa TICTS. Kwanini nimeuliza hivi, ni kwasababu enzi za TICTS Hutchinson port alifanya kazi pia ilihali hakua na mkataba wowote na serikali.

Je, Hutchinson port watafanya hivyo pia kwa DP WORLD?

Naomba kuwasilisha,
 
Kifupi ni kwamba sio kweli,tunabandari nzuri kuliko zote,Hao Dp world wanaweza SEMA bakini na bandari yenu,na wasiwe na shida.Hili deal ni viongozi wetu wamelipigania Kwa maslahi yetu/Yao,But let's be clear Waarabu hawatuhitaji zaidi ya tunavyowahitaji.Kuna msemo unasema ukitaka kitu tofauti fanya kitu tofauti,na ndio Mama alivyofanya.Nasimama na Maza.
 
Back
Top Bottom