Changamoto za uke wenza

Sina uzoefu ila nna swali. . .
Yeye alipokubali aongezewe mke mwenza alitegemea nini? Ofcourse lazima kiwango cha maisha kishuke kwasababu mume kaongeza mtu mwingine wa kumhudumia.

Sometimes sio kwamba hao wanaoongezewa wake wenza huwa wanakubali..unless unadefine una maanisha nini.Wanawake wenzetu wengi hawana kauli manyumbani mwao na mfumo dume bado upo sana hapa Tz.
 
Naona hakuna mtu anayeishi na mkemwenzie humu! Mwambie afuate moyo wake; that's all l can say!

Yaani! Kwani wanaoishi na wake wenza wanakuwa watu wa namna gani? Ina maana hawawezi kuingia JF au hawana mitandao au ni nini?Sitaki kuamini kwamba JF yenye members zaidi ya 30,000 mods mnisaidie stats, hamna wenye kuishi maisha hayo.

Huyo shosti wangu anaingiaga humu ila kwa hili hakutaka kuandika mwenyewe.Huenda anasoma taratibu na anakusanya tips za hapa na pale na pia kupokea pole zenu.
 
Nadhani dini inataratibu zake na hutoa ruhusa sahihi kuoa mke wa pili, na mke wa kwanza ananafasi yake ya kuridhia. Ndoa ya pili sio ya kificho na ya kubalika kidini - si kwa kuwa umependa tu kuoa mke wa pili basi unao. Kwa upeo wangu finyu, unao pale ambapo kuna mahitaji ya kufany hivyo - kupata mtoto au jinsia unayotaka wewe, mkeo mgonjwa, umesafiri uko mbali. Na hiyo yafanyike kwa utaratibu wake na uwe na uwezo wa kuwatosheleza wakeo sawa.

Lakini hapa inaonekana swala sio mke wa pili tena. Maana ameshaingia na shoti kutokana na ushauri wa nduguze anataka kuendelea kuwepo. Kuna mambo mawili hapa, kwanza aache kupambana - hili joto la hasira lipite. Kwa kuwa anakazi yake basi ajaribu kutumia hicho kidogo alichonacho kujikimu - kwahiyo tunaondoa magomvi ya matumizi. Pili kunaswala la kukubali na kujiwekea taratibu na masharti anayoyaona yanamfaa yeye - ratiba za mambo yao ya ndani na matumizi yao. Maana, asibaki anapambana kwanini kao wakati mtu keshaolewa - sasa yeye aseme mumewe anapaswa kufanya ni na nini kwake.

Ktk dini ya Kiislam hakuna dalili inayoonyesha mwanamme akitaka kuoa mke wa pili atake ruhusa kwa mkewe. Mwanamme anaruhusiwa kuoa hata bila kumwambia mkewe na hiyo ndoa ikawa ni sahihi. Uzoefu unaonyesha kuwa hakuna hata mwanamke mmoja duniani humu anayeweza kumpa mumewe ruhusa akaoe mwanamke mwingine. Hiyo ruhusa utasubiri mpaka Kiyama kifike hutoipata. Ila ni jambo zuri kwa mke na mume kushauriana kabla ya kuoa mke wa pili. Ikiwa mke atakataa mume ana haki ya kuendelea.

Pili ningewaomba wanawake wa Kiislam na wengineo watambue kwamba hii ruhusa ya kuoa mke zaidi ya mmoja imetolewa kwa mantiki zake na kuna falsafa kubwa ndani yake. Wasipinge tu kwa sababu ya matamanio ya nafsi zao. Tunajua kwa wanawake inauma sana kwa mume kuoa mke mwingine lkn Mungu ndo kesharuhusu kwa hiyo wawe na subira tu. Wajiulize swali moja: ingekuwa mmoja wao hajaolewa kabisa na nafasi iliyopo ni hiyo ya yy kuolewa mke wa pili halafu mwenzake kule anakataa yy angejifikiria vipi. Wanawake wawahurumie wenzao ambao hawana waume mpaka inafikia kujiingiza kwenye uchafu wa zinaa.
 
Shosti wangu analalamika sana kuhusu kuishi maisha ya uke wenza.Mumewe alimuolea mke mwenza na toka wakati huo maisha yao ni ya shida tupu.Kiwango cha maisha kimeshuka sana.Hakuna maelewano baina yake na mume, ukiachilia mbali mke mwenzie.Nyumbani kumekua kama kituo cha polisi.

Kwa wale wenye uzoefu na mitala, hebu mwageni siri ya mafanikio yenu tafadhali maana shosti anakaribia kupata wazimu!

Dini inaruhusu ndoa za uke wenza ila kwa watu waadilifu sana na wenye uwezo wa kuhudumia huduma zote 100% equally; Tamaa za kibinadam zinapelekea mijitu kujichumia zambi kuoa wakati uwezo hawana. Kama vipi aombe talaka tu; HER HAPPINESS SHOULD BE HER CHIEF AIM OF LIFE.
 
kuna dini zingine ngumu sana, kama ni dini yako huna budi kuvumilia na kumwomba mungu tu
 
Nilishawai muuliza dada mmoja ambaye alikuwa ameolewa mke wa pili na jamaa flani;
Hivi kwanini unachepuka wakati umeolewa?
Jibu alonijibu wallah niliishiwa nguvu,
Yule dada alisema hivi; Tatizo dushelele la foleni yeye hawezi,
dah niliishiwa nguvu sasa mpaka nikajiuliza kwanini akubali kama alikuwa hawezi kulisubiria mpaka litoke uko kwenye mzunguko.

Ukiachana na mfano huo hapo juu upo mwingine ambao nao pia ni dada ambaye najua makuzi na malezi yake, alikulia katika dini na alikuwa na msimamo thabiti katika dini, aliolewa na jamaa flani, ambaye waliishi vizuri wakafanikiwa kujenga na kuwa na maisha mazuri.

Baada ya kuwa na maisha mazuri jamaa aliowa mke wa pili na hapa ndipo timbwili lilipoanza, maana mwisho wa siku yule dada naye alitafta mtu wa pembeni kwa ajili ya kumtoa mawazo.

Jambo hili limekuwa likinichanganya sana, maana nikitazama wengi walokuwa na mahusiano na mke zaidi ya mmoja, wengi wanasaidiwa wake zao awe mkubwa au mdogo.

Nimejikuta naogopa hata ikifikia kuja kuoa wake wawili, maana wengi wanachapiwa na hawajui wanachapiwa.

Na sababu kubwa nimeiona wanayoijenga wanawake ni kuwa bwana wakuchangia hawawezi.

Sina lengo na kupingana naafundisho alokuja nayo bwana mtume, (Rehma na Amani zimshukie), ila nikitazama wanawake wa zama hizi ni mtihani kwakweli, maana kila ninapozungumza kwa hawa watu hali ni hiyo hiyo, yani kumi kwa mmoja ukute ndo mwenye kujiheshimu, maana haya mambo yanafanywa mpaka na wamama wa makamo yaani ukiwaangalia huwezi amini.

Angalizo kwa walioa wake wawili;
1;Jamani msijisahau sana iwe nyumba kubwa au ndogo basi kule ambapo utakuacha basi ujuwe watu wanakusaidia.

2;Pia ziara za kustukiza muhimu sana,maana wengi akiwa zamu ya bi mkubwa, huku kwa bi mdogo anamuacha free tu usiku kucha hata kupitia pita hakuna mpaka ifike zamu ya mchana, au kama atapita basi mchana,
Jamani kuweni makini mkitoa tu miguuu watu usiku wanakuja kulala na uzuri ratiba zenu wanazijua fika siku ambazo hampo.

Ebu wadau mkuje hapa tupeane maarifa maana mpaka nimekuwa muoga sana wakumiliki majiko mawili japo natamani sana hapo baadae, maana kwa sasa hali tete.
 
Kwani wanapooa wake wengi wanategemea nini?

Maisha yenyewe ya sasa hivi wanaume wenye nguvu ni wa kuhesabu ikiwa mwanamke mmoja mtu anashindwa kumridhisha unadhani ukiwa na zaidi ya mmoja nini kitatokea.
wanaowa kwa kufata mafundisho ya dini mkuu
 
Back
Top Bottom