Msaada tafadhali kuna njia yoyote isiyo na madhara ya kuongeza ukubwa wa matiti?

Kingcobra

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,000
309
Wapendwa,
Mke wangu nimeishi nae kwa miaka tisa na Mungu ametujalia watoto watatu. Kinachoninyima raha ni udogo wa matiti ya mke wangu. Anapokuwa na mimba na anaponyonyessha huwa yanakuwa makubwa na yanapendeza sana.

Lakini miezi michache baada ya kumwachisha mtoto huwa yanarudi kuwa madogo sana. Je, kuna njia ya asili au dawa isiyo na madhara ya kukuza matiti? Msaada tafadhali.

Am serious!
 
Akina dada wa JF tujuzeni tafadhali japo Kingcobra hajaweka wazi anataka matiti yawe makubwa kiasi gani! Jambo moja nataka nimfahamishe ni kwamba hakuna dawa isiyo na madhara. Kinachotofautisha kati ya dawa na dawa ni kiwango cha madhara basi. Lakini lazima yawepo.
 
Nenda kwa wachina, mmmh hata hivo kwa nn unashindwa kuukubali uumbaji wa Mungu?
 
Kuna wadudu fulani muda wote huwa wanazunguka kwenye maji yaliyotulia. Ukifanikiwa kumkamata msogeze kwenye chuchu za titi la mkeo. Yule mdudu atamuuma. Nasikia hapaumi sana. Fanya hivyo

kwenye titi la pili. Baada ya wiki moja utaona mambo yanavyobadilika.
 
Sor,hivi kabla hujamwoa hukuona kuwa ana matiti madogo? Kama yalikua hivyo ukaridhika ukaoa imekuaje sasa?
 
Sor,hivi kabla hujamwoa hukuona kuwa ana matiti madogo? Kama yalikua hivyo ukaridhika ukaoa imekuaje sasa?

Waswahili bwana! Badala ya kujibu na wewe unauliza na kuacha swali la mwenzio. Kama huna jibu si utulie tu!
 
Kuna wadudu fulani muda wote huwa wanazunguka kwenye maji yaliyotulia. Ukifanikiwa kumkamata msogeze kwenye chuchu za titi la mkeo. Yule mdudu atamuuma. Nasikia hapaumi sana. Fanya hivyo kwenye titi la pili. Baada ya wiki moja utaona mambo yanavyobadilika.

hizi tiba za babu! Hata nyuki akiuma chuchu, ziwa litavimba sana tu sasa na nyuki anaweza kutumika?
 
Wapendwa,
Mke wangu nimeishi nae kwa miaka tisa na Mungu ametujalia watoto watatu. Kinachoninyima raha ni udogo wa matiti ya mke wangu. Anapokuwa na mimba na anaponyonyessha huwa yanakuwa makubwa na yanapendeza sana. Lakini miezi michache baada ya kumwachisha mtoto huwa yanarudi kuwa madogo sana. Je, kuna njia ya asili au dawa isiyo na madhara ya kukuza matiti? Msaada tafadhali. Am serious!
huyu mke uliozeshwa ndoa ya mkeka? au ulimchagua akiwa na mimba kwa hiyo hukujua maziwa yake yana kasoro? au umeonja nani...h kutoka nyumba ndogo?

Anyway nenda kamfanyie plastic surgery ,lakini hapa atahitaji kuchukua mafuta kutoka sehemu nyingine ya mwili hasa mapaja kama yeye ni 'slim' itabidi uendelee kumvumilia.

Hakuna tiba isiyo na madhara!!
 
hizi tiba za babu! Hata nyuki akiuma chuchu, ziwa litavimba sana tu sasa na nyuki anaweza kutumika?

Utakuja umkumbuke babu utakapokuja uugue kisawasawa. Wengi wanaombeza babu hawajaugua kwa kiwango cha kupoteza matumaini, kama wanavyougua wale wanaosafiri kutoka Namtumbo mpaka Loliondo. Sikuombei lakini huo ndiyo ukweli na maadamu unaishi utayakumbuka maneno yangu. Samahani kama nimekukwaza.
 
Wapendwa,
Mke wangu nimeishi nae kwa miaka tisa na Mungu ametujalia watoto watatu. Kinachoninyima raha ni udogo wa matiti ya mke wangu. Anapokuwa na mimba na anaponyonyessha huwa yanakuwa makubwa na yanapendeza sana. Lakini miezi michache baada ya kumwachisha mtoto huwa yanarudi kuwa madogo sana. Je, kuna njia ya asili au dawa isiyo na madhara ya kukuza matiti? Msaada tafadhali. Am serious!
Kabla ya kumuoa matiti yake yalikuwa na size gani ? Natumai ulimpenda wakati hana mimba wala hanyonyeshi.
 
Its obvious kwamba mwanzoni tunaongozwa na tamaa ambayo inapelekea kukosa maamuzi sahihi of which tunafanya commitment zinazokuja kutusuta baada ya tamaa kutulia...Haiwezekani ukutane na binti of whom naamini ulimsifu sana maumbile yake (ikiwa ni pamoa na matiti yake madogo),ukambadili mawazo na kufanikiwa kuzaa nae watoto watatu halafu leo udogo wa maziwa uwe kero!

Yumkini ushaanza kukosa uaminifu kwenye ndoa yako ila bado unampenda mkeo so unafanya comparison.

Vyovyote iwavyo unalotaka kufanya ni against ethics za uumbaji!
 
Kuna wadudu fulani muda wote huwa wanazunguka kwenye maji yaliyotulia. Ukifanikiwa kumkamata msogeze kwenye chuchu za titi la mkeo. Yule mdudu atamuuma. Nasikia hapaumi sana. Fanya hivyo kwenye titi la pili. Baada ya wiki moja utaona mambo yanavyobadilika.

akitumia nyoka yataongezeka maradufu.
 
kaka Mungu alikujaalia aina hio ya maumbile kwa mkeo mi nadhani hatua moja ya kutatua tatizo ni kukubali tatizo,leo unataka mkuze maziwa miaka 9 baadae uzee ukimyemelea utatuomba ushaur jins ya kumrudisha ujana na labda mungu akimchukua je utatuambia namna ya kumfufua.

Yakubidi ukubali kila kukicha binadam tuna mahitaji mapya na tumetawaliwa na tamaa cha msingi kama mnapendana kwa dhati matiti tu c tatizo kubwa kihivyo mpende mkeo bwana.
 
Nilipata kusikia affection ya mapenzi ya ujana likely inarudi uzeeni...moral ya fundisho hili ni kwamba namna ulimpenda kwanza ndivyo utakavyompenda uzeeni...kwa maana nyingine ni kwamba umri wa kati ya ujana na uzee una mambo mengi sana ambayo yanatokea tu purposely...angalizo!

Epuka kufanya jambo lolote litakalokuja kuchakachua natural love kwa mkeo km Mwenyezi Mungu akikujaalieni uzee!
 
Pole sana kaka kwa hilo! Ingawa mi naona si tatizo maan kama lingekuwa tatizo lingetokea mwanzoni mwa mahusiano yenu! Ila kwa ushauri wangu ni kwamba mshukuru Mungu kwa kumwumb mkeo hivyo na wala usitafute njia ya kufanya matiti yake yawe makubwa, mana kama utafanya hivyo utayafurahia kwa mda tu halafu baadae yatakaposhuka,utaleta tena thread ya kuyarudisha kama zamani.

Sasa cha kufanya ni kitu kimoja, jaribu kutafuta sehemu zingine za mwili wa mkeo ambazo zitakusisimua zaidi..maana kuna sehemu nyingi tu ukiachana na matiti yake..Halafu angalia familia yako na watoto pia usije ukaumiza kichwa kwa jambo dogo kama hilo ukasahau familia na Kuanza toka nje kisa matiti makubwa..Ni hayo tu.

Ingawa mi ni mgeni ndani humu na nimevutiwa sana na mada mbalimbali..Naombeni mnikaribishe.

THANKS.
 
mkuu ridhika na maumbile ya mkeo...usiyumbishwe na wachina wanavyotuharibia maumbile halisi ya dada zetu..yakiwa makubwa au madogo swaga ni zile zile tuu inategemea na wewe unataka kuyafanyia utundu gani...huko unakotaka kuelekea utamsababishia mkeo matatizo mengine ambayo baadae utajutia..dawa za kijana zipo ila hazina kiwango cha ukubwa yanaweza kuwa makubwa kiasi ambacho utaona karaha...watch out mkuu
 
Mmmh, please angalia usije ukamuua mkeo ukakosa vyote.

Isitoshe matiti fake hutakuwa na raha nayo.
 
Kama ni mwembamba basi mwambie ale hovyo hovyo ili anenepe. Kwa kawaida akinenepa mwili na manyonyo huongezeka. Ila je unapenda anenepe? otherwise hakuna dawa nyingine isiyokuwa na madhara.
 
Back
Top Bottom