Msaada pls

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
113
Binafsi kauli ya TUCTA sioni kama inaniwakilisha mie km mfanyakazi wa Umma. Kiuhalisia katika mambo ambayo nilitarajia TUCTA ifanye si la kunishawishi nani awe kiongozi wangu bali kutetea maslahi na ustawi wa wafanyakazi kwa njia sahihi. Kwa mtindo huu TUCTA inataka kujipa wajibu wa kutuchagulia viongozi bila kujali kuna baadhi wanaridhishwa na utawala uliopo na kuna wengine kwao siasa ni upuuzi.

Msaada wangu ni kwamba hivi TUCTA wapo accountable kwa nani? Je, ni lazima mtumishi yoyote wa UMMA awe mwanachama wa chama cha wafanyakazi hata km aridhishi? Je, mtumishi huyo anaweza kuswitch kutoka chama kimoja kwenda kingine kwa hiari yake bila kizuizi chochote. Maana siamini km makato yangu kwenye mshahara yanafanya kazi niliyokusudia.
 
Mambo ya kujiunga au kutojiunga vyama vya wafanyakazi ni masuala ya hiari. Lakini faida moja ya vyama vya wafanyakazi duniani kote ni collective bargaining to the employer(s) and/or authority that regulates wages -- in this case -- the government. Hata ukijiunga na chama cha wafanyakazi, si lazima ukubaliane na maamuzi ya viongozi wake -- pamoja na wito wa kugoma -- kadhalika na huo wa kukuchjagulia kiongozi wa nci -- kama unavyosema. NI HIARI YAKO!!!!

Wao wanaelekeza tu. Aidha duniani kote ni vigumu sana kutenganisha vyama vya wafanyakazi na siasa za nchi na hii huonekana wazi wakati wa uchaguzi -- hata katika nchi zilizoendelea, hususan Marekani. Vyama vya wafanyakazi huchagua vchama gani cha siasa ikiunge mkono -- iwapo wakiona chama hicho kitawapa masilahi zaidi.
 
Nakumbuka mwaka jana wafanyakai wa NBC walikuwa wanataka wajitoe uanachama wa TUICO
Wakaweka msimamo kuwa hawataki wakatwe ada ya uanahama.
Iliwacost kwani wakubwa waliingilia kati.
By the way swala la uanachama ni hiari ya mwajiriwa but by the meaning,
Sio hiari ya mwairiwa.
 
Nimelazimika nikujibu ndugu yangu japo nilikuwa kimya kwa muda. Kimsingi kauli ya Mgaya nafikiri ni sahihi kabisa hasa ukizangatia CCM walishatoa ya kwao kupitia Rais wao tena na wao wakishangilia na kupongeza kwa maandamano.

Nikukumbushe tu kinachozungumzwa na TUCTA ni kwamba, Serikali inaouwezo wa kuongeza mshara hadi kufikia laki tatu na kumi na tano kutokana na taifiti mbalimbali ikiwemo ile waliyoifanya TUCTA wenyewe, inakadiriwa kuwa asilimia 80 ya pesa zinazotengwa katika bajeti serikali hutumika kuwalipa posho viongozi wakubwa, mawaziri, manaibu, makatibu wakuu, wakurugenzi, na vibosile wengine. Hebu fikiria mbunge analipwa 70,000 hadi 80,000 akihudhuria kikao bunge na marurupu kibao ikifika mwisho wa mwezi tena atalipwa hadi hela ya mafuta ya gari lake bila kujali analitumia kwa kazi gani. Huku Msomi wa ngazi ya Prof, Dr na hata Digrii anaehenyeka kila kukicha anaambulia laki 3 na ushee kama salio la juu au la kati.

Mfanyakazi kama wewe wa umma ukistaafu nahakika huwezi kufikisha alau milioni 10 hata utumikie miaka 40, wakati mbung akimaliza miaka yake mitano 5 anaondoka na si chini ya milioni 45. Sasa TUCTA inajaribu kupigania haya masuala ili tuweze kuwa na watumishi ambao wanafaidi jasho lao badala ya wachache kuwafaidi watumishi hawa. Usishangae wasomi wengi sasa wameamua kukimbilia siasa ujue wanasema jambo kubwa kwa viongozi wetu. Nafikiri unahitaji kuwasiliana na kiongozi wa TUCTA katika ofisi yako akupe somo zaidi badala ya kusema maneno kama mtu aliyetumwa kupotosha hali halisi waliyo nayo wafanyakazi wa umma.

Nikuulize swali, lipi unaweza kujivunia kutoka katika serikali ya kikwete? Huo mshahara uliongezeka kwa 30,000?
 
Binafsi kauli ya TUCTA sioni kama inaniwakilisha mie km mfanyakazi wa Umma. Kiuhalisia katika mambo ambayo nilitarajia TUCTA ifanye si la kunishawishi nani awe kiongozi wangu bali kutetea maslahi na ustawi wa wafanyakazi kwa njia sahihi. Kwa mtindo huu TUCTA inataka kujipa wajibu wa kutuchagulia viongozi bila kujali kuna baadhi wanaridhishwa na utawala uliopo na kuna wengine kwao siasa ni upuuzi.

Msaada wangu ni kwamba hivi TUCTA wapo accountable kwa nani? Je, ni lazima mtumishi yoyote wa UMMA awe mwanachama wa chama cha wafanyakazi hata km aridhishi? Je, mtumishi huyo anaweza kuswitch kutoka chama kimoja kwenda kingine kwa hiari yake bila kizuizi chochote. Maana siamini km makato yangu kwenye mshahara yanafanya kazi niliyokusudia.

Kwani kwenye chumba cha kura unakwenda na TUCTA? wewe ni mfanyakazi mwoga na msaliti. Nijuavyo mimi una haki ya kuchagua umpendaye, lakini waingereza wana msemo usemao "United we stand, devided we fall" NI mtanzania gani mfanyakazi asiyejali maslahi yake mwenyewe? nyie ndio wale waoga Ah! basi ngoja niachie hapa
 
Wewe ni mfanyakazi wa umma kivipi

  • BOT nayo ni tasisi ya umma

  • Wabunge nao wana haki ya kujiita watumishi wa umma
Kwa hiyo inawezekana
Madai yanaolezwa na TUCTA hayakugusi kwa kuwa ni kati ya wafanyakazi wachache sana wa umma mnaopata juu ya kile kinachodaiwa

Lakini hata kama hivi ndivyo
Demokrasia inasema wengi wape na Demokrasia inawaruhusu viongozi walichaguliwa kutumia busara zao kufanya maamuzi yenye faida kwa watu wao.

Ndio maana unaona mambo ya Richmond ,EPA, RADA. haimaanishi alichoamua Chenge ni mawazo ya watanzania achilia mbali wanasheria wote wa iliyokuwa Ofisi yake. Ni Demokasia iliyomchagua ndo ilimpa uwezo wa kuyafanya hayo. Cha kujiluza je alitumia Busara na Uzalendo?

Kwa hiyo kwa matamhi ya mgaya usiwe mbinafsi jaribu kuangalia ukweli halisi kwa asilimia kubwa ya wafanyakazi japo wewe yanaweza kuwa hayakuhusu.
__________________________________________________________________________________

Ukingalia Muunda wa TUCTA ni jumla ya vyama vya wafanyakazi wa aina mbali mbali, kuna chama cha wauguzi, madaktai, walimu, n.k Kwa hiyo kabla ya kuilaumu TUCTA ulitakiwa kujua Chama gani cha wafanyakazi ulitegmea kifanye nini.
 
Mambo ya kujiunga au kutojiunga vyama vya wafanyakazi ni masuala ya hiari. Lakini faida moja ya vyama vya wafanyakazi duniani kote ni collective bargaining to the employer(s) and/or authority that regulates wages -- in this case -- the government. Hata ukijiunga na chama cha wafanyakazi, si lazima ukubaliane na maamuzi ya viongozi wake -- pamoja na wito wa kugoma -- kadhalika na huo wa kukuchjagulia kiongozi wa nci -- kama unavyosema. NI HIARI YAKO!!!!

Wao wanaelekeza tu. Aidha duniani kote ni vigumu sana kutenganisha vyama vya wafanyakazi na siasa za nchi na hii huonekana wazi wakati wa uchaguzi -- hata katika nchi zilizoendelea, hususan Marekani. Vyama vya wafanyakazi huchagua vchama gani cha siasa ikiunge mkono -- iwapo wakiona chama hicho kitawapa masilahi zaidi.
Ndugu yangu Marksman asante saana kwa kutoa ufafanuzi huo. Lakini pia naomba nikukumbushe kuwa mfumo wa Marekani ni tofauti na wa kwetu kiasi kikubwa saana. Mf Marekani ukiangalia hata kwenye kampuni shareholders wanasauti kubwa sana kuliko nchi nyingine yoyote namaanisha shareholders wako highly protected. Vivyohivyo kwenye suala la kazi mwajiri na muajiriwa wote wana haki na wajibu. Sasa ukija kwenye nchi kama zetu, tunapata shida saana kujadili swala la haki, wajibu lakini pia tukiangalia hali halisi ya kiuchumi, tukiondoa dhana nzima ya kisiasa. Mf. Sijaona manifesto ya chama cha kisiasa kinachoweza kulipa mshahara huo wa TUCTA km ipo watuwekee hapa na tuanze kuichambua. Nashawishika kuwaona TUCTA kuwa wamevamia siasa zaidi kuliko uhalisia na ndio maana nafsi yangu inanituma kuhamia kwa wale watakaokuwa wanatoa ufafanuzi wakihusisha na hali halisi. Tuache blah blah, tujadili ukweli tuweke tarakimu, tuainisha huduma zoote za msingi na hapo fact itapatikana.
 
Wewe ni mfanyakazi wa umma kivipi

  • BOT nayo ni tasisi ya umma

  • Wabunge nao wana haki ya kujiita watumishi wa umma
Kwa hiyo inawezekana
Madai yanaolezwa na TUCTA hayakugusi kwa kuwa ni kati ya wafanyakazi wachache sana wa umma mnaopata juu ya kile kinachodaiwa

Lakini hata kama hivi ndivyo
Demokrasia inasema wengi wape na Demokrasia inawaruhusu viongozi walichaguliwa kutumia busara zao kufanya maamuzi yenye faida kwa watu wao.

Ndio maana unaona mambo ya Richmond ,EPA, RADA. haimaanishi alichoamua Chenge ni mawazo ya watanzania achilia mbali wanasheria wote wa iliyokuwa Ofisi yake. Ni Demokasia iliyomchagua ndo ilimpa uwezo wa kuyafanya hayo. Cha kujiluza je alitumia Busara na Uzalendo?

Kwa hiyo kwa matamhi ya mgaya usiwe mbinafsi jaribu kuangalia ukweli halisi kwa asilimia kubwa ya wafanyakazi japo wewe yanaweza kuwa hayakuhusu.
__________________________________________________________________________________

Ukingalia Muunda wa TUCTA ni jumla ya vyama vya wafanyakazi wa aina mbali mbali, kuna chama cha wauguzi, madaktai, walimu, n.k Kwa hiyo kabla ya kuilaumu TUCTA ulitakiwa kujua Chama gani cha wafanyakazi ulitegmea kifanye nini.
Naomba unielewe, sijawahi kukanusha kuwa mshahara ni mdogo la hasha! Lakini tatizo ninaloliona ni uwezo wa serikali kulipa pesa hizo na watu wengine kutaka kutuaminisha wafanyakazi kuwa na msimamo unaofanana. Binafsi natoafautiana saana na siasa za chama Tawala lkn kwa hoja ya TUCTA si sahihi. Pia kuna maswali ya msingi hapo juu nimeuliza, TUCTA wapo accountable kwa nani? Na nini hasa majukumu yao?
 
Kama hujui TUCTA ni nini,na hujui TUCTA wako kwa ajili ya nani na majukumu yake,basi wewe sio mtanzania na sio mfanyakazi hapa TANZANIA.
Kwa kukusaidia bofya hapa Trade Union' Congress of Tanzania - Wikipedia, the free encyclopedia
Tunajua lengo lako kama sio unajifanya kutojua ukweli halisi.
Mh Mgaya yuko sahihi kutetea maslahi ya wafanyakazi wote Tanzania,huyu ni shujaa.
Chama chochote cha kisisasa kinapoingia madarakani lazima kiwe na ushawishi mkubwa kwa wafanyakazi ukizingatia kuwa wafanyakazi ndio nguzo kuu ya utendaji weledi wa serekali itakayoingia madarakani.Endapo wafanyakazi hawatakuwa tayari kufanya kazi na chama husika matatizo yatakayojitokeza ni kama haya tunayoyashuhudia kipindi hiki kila sehemu rushwa inanuka.,utendaji mbovu wa wafanyakazi wa kipata cha chini.nk.
 
Vyama vya wafanyakazi duniani kote ni kati ya wadau wakubwa katika kuendesha nchi..
Huwezi ukaongelea siasa ukaacha kugusa maslahi ya wafanyakazi...
Tatizo nilionalo ni kwa Watanzania wengi tunadhani mambo ya kujiunga na hivi vyama ni "ushamba"...
Laiti kama watu makini wangegombea uongozi katika hivi vyama tungeona transformation ya ajabu katika kushughulikia masuala anuai ya kitaifa..
Tazama nguvu ya COSATU huko SA ndo utaelewa dhana nzima ya nini trade Union inatakiwa ifanye haswa inapokuwa na watu makini..
Nakusihi Umoja ni nguvu...
Solidarity Forever...!
 
(1) Umoja ni nguvu. Bargaining power ya wafanyakazi, kwa umoja wao ni kubwa. TANU na CCM vilikuwa vimezoea kuburuza NUTA na JUWATA. Sasa wamegonga kisiki. Ghafla wanaogopa sana nia ya TUCTA. Lakini wamechelewa.

(2) Kusema mfumo wetu sio wa Marekani hakufanyi kila kitu kinachofanyika Marekani kikawa kibaya kwetu. Vyama vya wafanyakazi Marekani vina kawaida ya ku-endorse mgombea wa Urais. Hiki ni kitu kizuri kwani kinavipa nguvu hivyo vyama. Ni kitu kinafaa hapa kwetu vile vile. Mgaya kagundua hilo, Anfael anaogopa sana! Kwa nini?

(3) Natoa mwito kwa vyombo vingine, sio vyama vya wafanyakazi tu, kujitayarisha ku-endorse mgombea. Vyama vya wanafunzi wa vyuo vikuu, UDASA na magazeti yatoe endorsement zao (for what they are worth) kampeni zitakapoanza.

Anfael usijaribu kuwagawa wafanyakazi. Waache wasikike. Wamedharauliwa muda mrefu mno. They have found their voice. Watanguruma! We acha tu!
 
Ndugu yangu Marksman asante saana kwa kutoa ufafanuzi huo. Lakini pia naomba nikukumbushe kuwa mfumo wa Marekani ni tofauti na wa kwetu kiasi kikubwa saana. Mf Marekani ukiangalia hata kwenye kampuni shareholders wanasauti kubwa sana kuliko nchi nyingine yoyote namaanisha shareholders wako highly protected. Vivyohivyo kwenye suala la kazi mwajiri na muajiriwa wote wana haki na wajibu. Sasa ukija kwenye nchi kama zetu, tunapata shida saana kujadili swala la haki, wajibu lakini pia tukiangalia hali halisi ya kiuchumi, tukiondoa dhana nzima ya kisiasa. Mf. Sijaona manifesto ya chama cha kisiasa kinachoweza kulipa mshahara huo wa TUCTA km ipo watuwekee hapa na tuanze kuichambua. Nashawishika kuwaona TUCTA kuwa wamevamia siasa zaidi kuliko uhalisia na ndio maana nafsi yangu inanituma kuhamia kwa wale watakaokuwa wanatoa ufafanuzi wakihusisha na hali halisi. Tuache blah blah, tujadili ukweli tuweke tarakimu, tuainisha huduma zoote za msingi na hapo fact itapatikana.
mkuu afadhali tuvijaribu vyama vingine maana CCM kupitia mwenyekiti wao wa Taifa wamekiri wameshindwa kulipa hiyo mishaara hata iweje hawatalipa wafanyakazi kiasi hicho. pili ujasoma ilani za vyama vingine ndio maana unasema hivyo lakini viko wazi kuhusu maslahi ya wafanyakazi kwa ujumla
 
Naomba unielewe, sijawahi kukanusha kuwa mshahara ni mdogo la hasha! Lakini tatizo ninaloliona ni uwezo wa serikali kulipa pesa hizo na watu wengine kutaka kutuaminisha wafanyakazi kuwa na msimamo unaofanana. Binafsi natoafautiana saana na siasa za chama Tawala lkn kwa hoja ya TUCTA si sahihi. Pia kuna maswali ya msingi hapo juu nimeuliza, TUCTA wapo accountable kwa nani? Na nini hasa majukumu yao?

Wewe mfanyakazi kweli au mzushi?Unasema "unaloona ni uwezo wa serikali kulipa pesa hizo..." kwani serikali inawezaje kuwalipa wabunge mamilioni?Inawezaje kumudu ununuzi wa magari na samani za thamani kubwa?Usitubabaishe hapa.Hakuna mfanyakazi mwenye akili timamu (na ambaye analipwa mshahara usitosha matumizi japo ya wiki moja) atakayehoji shinikizo la TUCTA kwa serikali.Au wewe unatoka kwenye ajira ambazo zina "mafungu maalum"?

Eti TUCTA hawako sahihi!Yaani hawako sahihi kudai maslahi bora kwa wafanyakazi?Hawako sahihi kudai kuwa chama kinachostahili kupewa kura za wafanyakazi ni kile chenye kujali maslahi ya wananchi wote kwa ujumla (including wafanyakazi) na sio kikundi cha wateule wachache?

Ushaambiwa,TUCTA hawataingia nawe kwenye chumba cha kupiga kura.Kwahiyo kama unataka kuipigia kura CCM,go ahead.Unasema una maswali ya msingi...eti "nini hasa majukumu ya yao (TUCTA)"?Sasa kama hujui majukumu yao umewezaje kuhitimisha kuwa hawako sahihi?

Halafu unachekesha kweli unaposema

Sijaona manifesto ya chama cha kisiasa kinachoweza kulipa mshahara huo wa TUCTA km ipo watuwekee hapa na tuanze kuichambua. Nashawishika kuwaona TUCTA kuwa wamevamia siasa zaidi kuliko uhalisia na ndio maana nafsi yangu inanituma kuhamia kwa wale watakaokuwa wanatoa ufafanuzi wakihusisha na hali halisi. Tuache blah blah, tujadili ukweli tuweke tarakimu, tuainisha huduma zoote za msingi na hapo fact itapatikana.

Kama hujaona manifesto ya chama kinachozungumzia maslahi bora ya wafanyakazi basi subiri ya Chadema....au endelea kuiamini hiyo ya CCM.Wanaofanya blah blah ni TUCTA au watu wa aina yako ambao mnatetewa lakini hamtaki?Wenye blah blah ni watu wa aina yako waliopiga vigeregere wakati Kikwete anatukana wafanyakazi na mifano yake ya mbayuwayu na tetere.
 
Kitendo cha JK kutukana viongozi halali wa chama cha wafanyakazi ina maana kuwa katukana wafanyakazi wote. Kitendo chakusema hataki kura zetu maanaa yake hawataki wafanyakazi na hayuko tayari kuwasaidia kwa lolote lile na anatuona kama mavuvuzela tu.

Inatakiwa tukumkumbushe kuwa tunaumuhimu kwa kutompa kura pls shima hima wafanyakazi hakikisha wote unaowasaidia ndugu jamaa na marafiki hawampi jamaa kura ili ajifunze kuheshimu wafanyakazi
 
Majukumu ya chama cha wafanyakazi si kuamulia wafanyakazi wachague kiongozi yupi kwani kila mmoja ana itikadi yake. anachofanya mgaya kwa sasa ni kinyume na taratibu za majukumu yake coz siamini kuwa wafanyakazi wote ni members wa chadema ambako inadaiwa kuwa anataka kugombea ubunge wa Lushoto kwa tiketi ya chama hicho(sijui how true is that).
kila mfanyakazi anatetewa na chama cha fani yake husika lakini sidhani kama haki ya kikatiba ya kuchagua kiongozi ni wajibu wa Tucta kukuamulia..ushauri wangu ni kila mtu abebe kadi yake na mgombea wake amweke moyoni akajimwage nae karatasini oktoba 31 kwa siri (ktk maana halisi ya siri). ukimfata Mgaya utajikuta unalia bure pale mgombea watakaeamua kumsapoti akishindwa na wewe kujikuta on the losing side..coz utakuwa mjinga kuamuliwa hata mambo ya msingi..mengine tuyasikilize tu kwa ushabiki wa kisiasa ila binafsi nitampigia kura ambaye atanishawishi katika kampeni na kuona ilani ya chama chake ikoje this time around...
naamini wafanyakazi wote kila mmoja ana utashi wake na hatakubali kuburuzwa...tazama mivutano ya TUICO na FIBUCA utagundua mkiwa ofisini mnaamua pamoja lakini mkutanoni kila mmoja ana lake na mwisho uwakilishi wa wafanyakazi unakuwa haufanyiki kwa ufasaha kutokana na mivutano ya vyama hivi.
KILA MMOJA ACHAGUE KIONGOZI ANAYEMTAKA NA USIKUBALI KUBURUZWA...hata kama ni mpinzani wa chama chako kama anafaa DO THE RIGHT THING...coz si kila mwanachama kumpa kura mgombea wa chama chake.
 
Kama hujui TUCTA ni nini,na hujui TUCTA wako kwa ajili ya nani na majukumu yake,basi wewe sio mtanzania na sio mfanyakazi hapa TANZANIA.
Kwa kukusaidia bofya hapa Trade Union' Congress of Tanzania - Wikipedia, the free encyclopedia
Tunajua lengo lako kama sio unajifanya kutojua ukweli halisi.
Mh Mgaya yuko sahihi kutetea maslahi ya wafanyakazi wote Tanzania,huyu ni shujaa.
Chama chochote cha kisisasa kinapoingia madarakani lazima kiwe na ushawishi mkubwa kwa wafanyakazi ukizingatia kuwa wafanyakazi ndio nguzo kuu ya utendaji weledi wa serekali itakayoingia madarakani.Endapo wafanyakazi hawatakuwa tayari kufanya kazi na chama husika matatizo yatakayojitokeza ni kama haya tunayoyashuhudia kipindi hiki kila sehemu rushwa inanuka.,utendaji mbovu wa wafanyakazi wa kipata cha chini.nk.
Asante kwa link ya kwenye wikipedia. Lakini huko nilishapita nikajaribu pia kuitafuta website ya TUCTA ili nione wanaeleza nini huko nasikitika sikufanikiwa kuipata. TUCTA naifaham kwa juu juu sana nasipendi niwe km wengi nijiridhishe kuwa naifaham kiundani. Ningependa nisome katiba yao na muundo wao wa uongozi na accountability ndio vinavyonisukuma kuuliza. Nahitaji saana kufaham achievement zao kipindi hiki choote ambacho michango yetu imekuwa ikichukuliwa.
Mtizamo wa kuwa chama chochote cha wafanyakazi kinapokuwa madarakani ni lazima kiwe na nguvu, binafsi nauona ni mtazamo wa kucopy na kupaste. Naliongea hili kwa kuwa na uhakika kabisa katika nchi yetu pendwa Tanzania, wafanyakazi ni wachache saana kuliko wakulima au makundi mengineyo. Kwahiyo sitaki kujiaminisha na siku ya mwisho kuaibika eti wafanyakazi wana nguvu. Wakulima angalau wanaweza kutishia kuidhibu serikali au chama chochote maana wao ni wengi hasa katika nchi yetu.
 
(1) Umoja ni nguvu. Bargaining power ya wafanyakazi, kwa umoja wao ni kubwa. TANU na CCM vilikuwa vimezoea kuburuza NUTA na JUWATA. Sasa wamegonga kisiki. Ghafla wanaogopa sana nia ya TUCTA. Lakini wamechelewa.

(2) Kusema mfumo wetu sio wa Marekani hakufanyi kila kitu kinachofanyika Marekani kikawa kibaya kwetu. Vyama vya wafanyakazi Marekani vina kawaida ya ku-endorse mgombea wa Urais. Hiki ni kitu kizuri kwani kinavipa nguvu hivyo vyama. Ni kitu kinafaa hapa kwetu vile vile. Mgaya kagundua hilo, Anfael anaogopa sana! Kwa nini?

(3) Natoa mwito kwa vyombo vingine, sio vyama vya wafanyakazi tu, kujitayarisha ku-endorse mgombea. Vyama vya wanafunzi wa vyuo vikuu, UDASA na magazeti yatoe endorsement zao (for what they are worth) kampeni zitakapoanza.

Anfael usijaribu kuwagawa wafanyakazi. Waache wasikike. Wamedharauliwa muda mrefu mno. They have found their voice. Watanguruma! We acha tu!
Tatizo wafanyakazi wanaamini wao ndio Watanzania peke yao. Wanasahau kuwa kuna kundi kubwa zaidi kuliko wao wanahitaji huduma kutoka serikalini na wanaushawishi mkubwa.
 
Wewe mfanyakazi kweli au mzushi?Unasema "unaloona ni uwezo wa serikali kulipa pesa hizo..." kwani serikali inawezaje kuwalipa wabunge mamilioni?Inawezaje kumudu ununuzi wa magari na samani za thamani kubwa?Usitubabaishe hapa.Hakuna mfanyakazi mwenye akili timamu (na ambaye analipwa mshahara usitosha matumizi japo ya wiki moja) atakayehoji shinikizo la TUCTA kwa serikali.Au wewe unatoka kwenye ajira ambazo zina "mafungu maalum"?
!

Eti TUCTA hawako sahihi!Yaani hawako sahihi kudai maslahi bora kwa wafanyakazi?Hawako sahihi kudai kuwa chama kinachostahili kupewa kura za wafanyakazi ni kile chenye kujali maslahi ya wananchi wote kwa ujumla (including wafanyakazi) na sio kikundi cha wateule wachache?

Ushaambiwa,TUCTA hawataingia nawe kwenye chumba cha kupiga kura.Kwahiyo kama unataka kuipigia kura CCM,go ahead.Unasema una maswali ya msingi...eti "nini hasa majukumu ya yao (TUCTA)"?Sasa kama hujui majukumu yao umewezaje kuhitimisha kuwa hawako sahihi?

Halafu unachekesha kweli unaposema

Kama hujaona manifesto ya chama kinachozungumzia maslahi bora ya wafanyakazi basi subiri ya Chadema....au endelea kuiamini hiyo ya CCM.Wanaofanya blah blah ni TUCTA au watu wa aina yako ambao mnatetewa lakini hamtaki?Wenye blah blah ni watu wa aina yako waliopiga vigeregere wakati Kikwete anatukana wafanyakazi na mifano yake ya mbayuwayu na tetere.
Sina sababu ya kuzua mie ni mfanyakazi na ninapenda kusimamia ukweli licha ya kuwa kwa wengi unauma. Tuwe realistic kidogo, unaweza kuja na hizo figure za mishahara kwa mwaka za mbunge na thamani za hizo furniture ili tuhakiki huo uwezo?? Pia katika figure zako tueleze wabunge walipwe kiasi gani! Maana sielewi tatizo ni mishahara ya wabunge ya wafanyakazi Ishu si kusema bila kuonyesha, tumeomba manifesto iweke hapo tuanalyse uwezo wa Chama kiuhalisia wa kulipa wafanyakazi pesa hizo.
 
Back
Top Bottom