Msaada please...Ninampenda dada yangu(Mtoto wa mama yangu mdogo)

Tuvako

Member
May 19, 2012
82
13
Wakuu...Naombeni msaada wenu wa mawazo...
Nimetokea kumpenda sana mtoto wa mama yangu mdogo na nafikiri labda MUNGU akipenda,nafikiria kumuoa huko baadae..Ila bado sijamwambia kuhusu hisia zangu juu yake.

Sasa je,Itakuwa sawa kama tukiamua kuoana? Hasa ukizingatia kuwa sisi ni ndugu..Je imekaaje hili katika tamaduni zetu za kitanzania?
Naomba msaada wakuu
 
Inategemea upo Dini gani? Muislam au Mkristo? ikiwa wewe ni Muislam unaweza

kumuowa mtoto wa mama yako mdogo,mtoto wa mama yako mkubwa mtoto wa baba yako mkubwa,mtoto wa bab yako

mdogo,mtoto wa shangazi yako,mtoto wa mjomba wako.Hurusiwi kumuowa yule mwanamke ambaye mumezaliwa na Baba

Mmoja anakuwa ni ndugu yako.Kwa Mfano Baba ameowa mke mwengine na huko amezaa mtoto wa kike anakuwa huyo ni

ndugu yako wa damu huruhusiwi kumuowa huyo mtoto wa kike. Swali langu lipo pale pale wewe upo dini gani?
 
Mkuu Nashukuru...Mi ni mkristo
 
Mkuu Nashukuru...Mi ni mkristo

Mambo ya Walawi, Chapter 18

[SUP]18:4[/SUP] Mtazifanya hukumu zangu, nanyi mtazishika amri zangu, ili mwenende katika hizo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

[SUP]18:5[/SUP] Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi Bwana.

[SUP]18:6[/SUP] Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana.

[SUP]18:7[/SUP] Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake.

[SUP]18:8[/SUP] Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako.

[SUP]18:9[/SUP] Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue.

[SUP]18:10[/SUP] Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe.

[SUP]18:11[/SUP] Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake.

[SUP]18:12[/SUP] Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu.

[SUP]18:13[/SUP] Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu.

[SUP]18:14[/SUP] Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako.

[SUP]18:15[/SUP] Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo.

[SUP]18:16[/SUP] Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo.

[SUP]18:17[/SUP] Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu.

[SUP]18:18[/SUP] Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai.

[SUP]18:19[/SUP] Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake.

[SUP]18:20[/SUP] Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye.

[SUP]18:21[/SUP] Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana.

[SUP]18:22[/SUP] Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.

(MKUU MTOTO WA MAMA YAKO MDOGO UNAWEZA KUMUOWA)
 
Inategemea upo Dini gani? Muislam au Mkristo? ikiwa wewe ni Muislam unaweza

kumuowa mtoto wa mama yako mdogo,mtoto wa mama yako mkubwa mtoto wa baba yako mkubwa,mtoto wa bab yako

mdogo,mtoto wa shangazi yako,mtoto wa mjomba wako.Hurusiwi kumuowa yule mwanamke ambaye mumezaliwa na Baba

Mmoja anakuwa ni ndugu yako.Kwa Mfano Baba ameowa mke mwengine na huko amezaa mtoto wa kike anakuwa huyo ni

ndugu yako wa damu huruhusiwi kumuowa huyo mtoto wa kike. Swali langu lipo pale pale wewe upo dini gani?

Hata msichana ambae mmenyonyeshwa na mwanamke mmoja (sio ndugu wa kuzaliwa nae) pia hufai kumuoa..
 
wewe mchumbie tu huyo binti na umsitiri,mimi nikirudi na nikikuta bado hujamuoa,namtia mimba halafu nakuachia mzigo mjomba ulee.
Nalog off
 
Wakuu...Naombeni msaada wenu wa mawazo...
Nimetokea kumpenda sana mtoto wa mama yangu mdogo na nafikiri labda MUNGU akipenda,nafikiria kumuoa huko baadae..Ila bado sijamwambia kuhusu hisia zangu juu yake.

Sasa je,Itakuwa sawa kama tukiamua kuoana? Hasa ukizingatia kuwa sisi ni ndugu..Je imekaaje hili katika tamaduni zetu za kitanzania?
Naomba msaada wakuu

Ukiona haya na mengne yanayofanana na haya, ujue kuja kwa mwana wa adamu kutuhukumu tuliohai na wafu kumekaribia.
 
Sasa je,Itakuwa sawa kama tukiamua kuoana? Hasa ukizingatia kuwa sisi ni ndugu..Je imekaaje hili katika tamaduni zetu za kitanzania?
Naomba msaada wakuu

Ndio matatizo ya mwanadamu kuwa na ubongo wa kuku wa kienyeji, kila mahali unataka kuchakura tu.
 
Badili dini uwe muislamu. Umshawishi nae awe muislamu na muoane.
Mkuu Nashukuru...Mi ni mkristo

Japokuwa kisayansi pia haishauriwi, kwa sababu mmetoka gene pool moja kuna uwezekano mkubwa wa kujitokeza kwa magonjwa ya kurithi ambayo yapo recessive kwenu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom