Msaada, Nina tatizo la uoga uliopitiliza

benny boy

Member
Nov 21, 2023
31
57
Ndugu wapendwa mimi ni kijana wa miaka 22. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza nasumbuliwa sana na tatazo la uoga tena uliopitiliza.
Katika kipindi chote ambacho nimeishi hapa duniani nimeishi maisha ya taabu sana kwa sababu ya hali yangu hii. Mfano tangu npo shule ya msingi hata kama jibu nalijua nikitaka kunyoosha tu mkono ghafla ntaanza kutetemeka bila hata sababu. Natetemeka sana mapigo ya moyo huenda mbio na hujisikia aibu kali sana. Niki pointiwa na mwalimu au mtu yeyote kutoa hoja mbele za watu naweza hata kuzimia kwa mshtuko wa uoga

Pia hata kama nasafiri nikikiribia tu kufika stendi najikuta naingiwa na uoga mkubwa sana. Kwenye suala la kutongoza sasa ndio usiseme huwezi amini mpaka umri wangu huu sijawahi kuwa na mpenzi kabisa.
Nimekuwa sijiamini hata kama natembea najishtukia sana. Naogopa Ku socialize iwe
kwenye sherehe, msiba au shughuli yoyote ya kijamii. Nimekuwa nashinda ndani sitaki kabisa kuchanganyikana na jamii.

Wakuu hali hii imenepotezea confidence kabisa na imenifanya niwe na mawazo mabaya kabisa sababu huu ni ujinga mtoto wa kiume kabisa ila naishi kama demu

Kwa hiyo basi nimekuja kwenu kuwaomba msaada hasa wa kimatibabu maana naamini humu wapo wengi wenye uelewa na tatizo hili. Karibuni!!.
 
Watu waliokulea mpaka unakuwa mkubwa watakuwa walikulea Kwa kukukaripia na kukugombeza hovyohovyo ndo maana unakuwa na hiyo hali. Fanya uchunguzi. Watoto wa wazungu Wanajiamini hata wanaweza kuimba mbele ya jukwaa kubwa la watu. Lakini watoto wa kibongo ni kukaripiwa Mda wote.
 
Watu waliokulea mpaka unakuwa mkubwa watakuwa walikulea Kwa kukukaripia na kukugombeza hovyohovyo ndo maana unakuwa na hiyo hali. Fanya uchunguzi. Watoto wa wazungu Wanajiamini hata wanaweza kuimba mbele ya jukwaa kubwa la watu. Lakini watoto wa kibongo ni kukaripiwa Mda wote.
Daaaah yaweza kuwa kweli maana mimi nimelelewa kwenye malezi ya kukuripiwa sana.
 
Back
Top Bottom