Msaada: Nina gari aina ya Noah, nifanye biashara gani?

IPILIMO

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,819
799
Hello wana-JF, Tafadhari naomba msaada kwa mwenye IDEA ya kuweza Kuingiza kipato kwa kutumia Gari aina ya NOAH, naomba anisaidie ili niweze kutumia hii gari kama mtaji na hivyo kutengeneza fedha kiasi.
Naishi Mbeya mjini; Nilishawahi kujaribu kutumia kusafirisha Abiria wanao safiri jioni kutoka Mbeya-Dar na Dar-Mbeya; Changamoto zikawa nyingi sana mfano askari njiani, lakini pia wapiga debe wanataka hela nyingi na sometimes wanakusanya wenyewe nauli mfano mby-dar sh 40,000 wenyewe wanakwambia abiria anayo 25,000 au 30,000 au 35,000 na bado ukikubali kila kichwa sh 5000 unampa; (kumbuka nao wamefanya vile vijiwe ni mali yao hivyo si rahisi kubishana nao), pia sometimes sio rahisi kupata abiria wa kutosha Noah....angalau abiria 8,9 au 10...hivyo hesabu kugoma kwakuwa gharama za mafuta na emergence ya askari uaweza kuta hubaki na kitu kwenda na kurudi au ukabaki na sh 20,000 tu. PIA dar-mby ni tabu sana kuwapata abiria kwakuwa kuna IT nyingi za kuja Mbeya/Tunduma

Nilifanya hivyo mara mbili tu nikaona ni ngumu kupata angalau kifaida cha wastani.
Hivyo naomba kwa mwenye wazo bora zaidi ya hili au kureboresha hili.
GARI ni nzima kabisa; aina Extra limo, pearl white. NO C.

NI hayo tu ndugu zangu.
 
piga trip fupi fupi huko huko mbeya, au kodisha maharusi... kubebea maids.

ukishindwa kabisa fikiria biashara nyingine.. hiyo noah uiuze upate mtaji
 
piga routes fupi mkuu, mfano mbeya-vwawa-tunduma. au mtafute mzoefu mkodishie halafu mkubaliane tu malipo kwa siku.
 
Back
Top Bottom