Msaada: Naomba ufafanuzi kwa hili tafadhari

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Kuna wakuu wa mikoa wanafanya kazi ndani ya mikoa Miwili,je wanawezaje kuwatumikia hawa wananchi na je gharama za kila siku kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine ni nani anayegharamikia?

Mfano:Mkuu wa mkoa wa Mbeya John Mwakipesile ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dk Parseko Ole Kone ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Na yawezekana kuna wengine wengi je Mkuu wa mkoa pekee na Mkurugenzi na mameya wanakazi gani? Naombeni msaada wenu Tafadhari.
 
Coz kama kuna marupurupu, posho n.k nadhani atalipwa double achilia mbali mshahara
 
Huyu Mwakipesile kuna kipindi alilalamikiwa kufanya kazi za Chama na kusahau majukumu yake ya Mkuu wa Mkoa na je alikuwa analipwa marupurupu na chama?
 
Na kuna wengine ni wabunge na ni wakuu wa Mikoa ,na wawapo bungeni shuighuli zake husimama kwa muda. Na mkuu wa mkoa ana mshahara wake na Mbunge ana mshahara wake sasa hawa sijui ndo wanapokea mishahara miwili?
 
Kuna wakuu wa mikoa wanafanya kazi ndani ya mikoa Miwili,je wanawezaje kuwatumikia hawa wananchi na je gharama za kila siku kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine ni nani anayegharamikia?

Mfano:Mkuu wa mkoa wa Mbeya John Mwakipesile ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa

Mkuu wa mkoa wa Singida Dk Parseko Ole Kone ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara

Na yawezekana kuna wengine wengi je Mkuu wa mkoa pekee na Mkurugenzi na mameya wanakazi gani? Naombeni msaada wenu Tafadhari.

Ni ukosefu wa maadili, kujali, nidhamu, umakini na akili wa anaewateua...

Kwangu mimi hawana kosa, kama mkulu kakuteua unafanyaje wakati maslahi nje nje..
 
Na kuna wengine ni wabunge na ni wakuu wa Mikoa ,na wawapo bungeni shuighuli zake husimama kwa muda. Na mkuu wa mkoa ana mshahara wake na Mbunge ana mshahara wake sasa hawa sijui ndo wanapokea mishahara miwili?

Yaani we acha tu, haya mambo kila nikiwaza nasikia kutapika. Utasikia mtu ni mbunge, mkuu wa mkoa then naibu mkuu wa mkoa, na bado hapo sijakwambia atakuwemo ktk kamati ngapi za bunge.

Kusanya pesa anayolipwa kama hujaona ni sawa mishahara ya madaktari 50 wa Muhimbili
 
Hapo ni kutafutia Rushwa wakati wa uchaguzi,unakuta mtu katumia Milioni 100 kwenye kampeni,hapa kweli umepatia,na ukifika wakati wa kampeni basi mikoa inakuwa wazi kwa sababu wakuu wako kwenye kampeni.
 
Back
Top Bottom