Msaada- Kubadili Matumizi ya Ardhi

Bobby

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
2,182
1,892
Habari za sikukuu wakuu!

Ninaomba ushauri wenu kwenye hili ninalosimulia hapa chini.

Ni kwamba hapa ninapoishi nina jirani yangu ambaye ana plots 2, moja niko opposite nayo na nyingine ni ya nne upande wangu wa kulia. Hii ya upande wa kulia (inapakana na plot yangu nyingine) kwa makosa amejenga guest house. Ninasema kwa makosa kwa kuwa nina original master plan ya eneo lote na inaonesha plots zote ni za makazi (residential) si kwa ajili ya biashara. Na sikuwahi kuona bango la Manispaa linalotaka consent ya kubadilisha matumizi ya ardhi kama sheria inavyotaka which means taratibu hazikufuatwa.

Kwa kujenga guest aliniboa sana lakini sikujali sana kwani usumbufu wake upo but si mkubwa sana. Miezi kadhaa iliyopita alinipigia simu akitaka tubadilishane plots, kwamba ni mpe ya upande wa kulia inayopakana na guest yake na yeye anipe yake ambayo iko opposite na nyumba yangu. Nikamweleza anipe muda. Nikajaribu kuuliza kwa majirani nini exactly anataka kujenga kwenye hiyo plot? Nikaambiwa ni bar, na of course ili kushindana na bar zilizoko barabara kubwa kwenye business center bar hii itakuwa na live band. Hili lilinikwaza sana kwani tumehama huko tulikotoka kuepuka hizi kelele tukatafuta huku ambako kuko planned ambako nako kelele zinatufuata tena so twende wapi? Ikabidi niandike barua kwenye serikali ya mtaa ambako waliipokea na kuahidi kuifanyia kazi. Ni mwezi wa pili sasa kila nikiulizia jibu ninalopewa ni kwamba hawajampata bado.

Kama wk moja iliyopita, wife alikuwa na jirani yake ambaye alimweleza kwamba amesikia maneno kuwa jirani yangu mwenye adhma ya kujenga bar analalamika kwamba mimi ninayafuatilia sana maisha yake na kwamba baya lolote litakalompata mimi nitakuwa responsible. Huu ni upuuzi wa mwisho, mambo yangu mengine nashindwa kuyafuatilia kwa kukosa muda nitawezaje kuyafuatlia ya mwingine?

Ninaomba ushauri kwenye haya:

(i) Serikali ya mtaa imekaa kimya muda mrefu sasa, je its ok kuwareport manispaa? Hofu yangu ni kwamba jamaa asije kuwa kawarambisha na akaja kujenga bar kama alivyojenga guest house kinyume cha sheria.

(ii) Suppose ni kweli jirani yangu ameyasema hayo niliyoyataja, je ipo haja ya kisheria kureport hicho alichokisema police ili kuwa safe just in case amepatwa na tatizo lolote?

Sorry kwa story ndefu hapo ndio nimejitahidi kufupisha. Ahsante.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom