Msaada: Kuagiza vitu toka China kwa njia ya mtandao

kisinzi

Member
Mar 12, 2012
18
6
Ninahitaji kununua kifaa tiba fulani toka katika kampuni ya Maya medical equipment limited yenye anwani hii hapa:No 10, Haiyue building ,HaiBin garden, Shangjiao Dashi town, Panyu Area,Guangzhou,China. Je kuna mtu mwenye taarifa au uzoefu wa kununua vitu kwa mtandao toka China? Naogopa kulizwa na hawa jamaa!
 
Call me 0754485762
 
Mtu anahitaji msaada jinsi ya kuagiza bidhaa China, Kama Unajua jinsi ya kumsaidia si umwelekeze. Sasa unapoandika "Call Me" na kuweka namba yako kwani amekuambia anahitaji huduma ya massage au kitchen party!!??
 
Ninahitaji kununua kifaa tiba fulani toka katika kampuni ya Maya medical equipment limited yenye anwani hii hapa:No 10, Haiyue building ,HaiBin garden, Shangjiao Dashi town, Panyu Area,Guangzhou,China. Je kuna mtu mwenye taarifa au uzoefu wa kununua vitu kwa mtandao toka China? Naogopa kulizwa na hawa jamaa!

Mkuu,
Kitu kikubwa cha kuzingatia ni physical address na contacts za hao jamaa. Pia kuna kitu kinaitwa RCN (Registered Corporate Number),kampuni ya kueleweka lazima iwe na hii number ili ijulikane na serikali ya China.
Pia jinsi ya malipo nakushauri Kama unaweza utumie L/C ni salama zaidi. Kama supplier ni tapeli utaona anakwepa sana hii njia ya malipo. Wanapenda sana kutumia Western Union, T/T,Paypal n.k...Ila pia kuna makampuni ya kweli yanatumia njia hizo za malipo pia.

Ushauri mwingine Kama unaweza kupata Mtanzania anaishi China inaweza ikasaidia zaidi kwa kumuomba akapate uhakika moja kwa moja kwa kampuni husika kutokana na anuani (Physical address) uliyonayo.
Kuwa makini ndugu yangu,watu wanalizwa sana.
 
Ninahitaji kununua kifaa tiba fulani toka katika kampuni ya Maya medical equipment limited yenye anwani hii hapa:No 10, Haiyue building ,HaiBin garden, Shangjiao Dashi town, Panyu Area,Guangzhou,China. Je kuna mtu mwenye taarifa au uzoefu wa kununua vitu kwa mtandao toka China? Naogopa kulizwa na hawa jamaa!

tembela alibaba.com angalia kama supplier ni verified,kama ni verified,unaweza kutumia makampuni ambayo yapo Tanzania na yana matawi kule,watathibitisha uwepo wa hiyo ofisi,then ndiyo utawalipa na kusafirishiwa mzigo wako.

Kila la heri.
 
Hapa hapam kuna watu wanataka Kuneemeka, hizi call me huwa zinaniboa sana,

Ok kama wadau wengine walivyo sema tembelea Alibaba na Cheki kama huyo supplier ni verfied au la, na kikubwa kama utafanya nao manunuzi jaribu sana kutumia ESCROW, Hawa escrow wao ndo hushikilia pesa za mteja mpaka pale mteja atakapo pata B/L na hapo huachia pesa ziende kwa muuzaji, na kama bado utapata mzigo na ukawa na kasoro bado unatakiwa kufunga madai ndani ya siku 60 tangia transaction ifanyike na utarudishiowa pesa yako,

Ila kwa sasa Suplier wengi walioko Alibaba sio wasanii make Kuna msako ambao ulifanyika na kukamata Wanegeria wengi sana walio kuwa wanatumia kutapeli,

Na ukisha zoeana na suplie hakuna haja ya Kupitia ESCROW, Kwa sababu escro nao kuna % unawapatia, so unaweza ukawa unaagiza moja kwa moja na kumplipa suplier bila kupitia popote pale
 
Ntajuaje
tembela alibaba.com angalia kama supplier ni verified,kama ni verified,unaweza kutumia makampuni ambayo yapo Tanzania na yana matawi kule,watathibitisha uwepo wa hiyo ofisi,then ndiyo utawalipa na kusafirishiwa mzigo wako.

Kila la heri.
kma ni verified au laa mkuu?
 
Kama uko serious nitakusaidia kupitia influence yangu. Kuna kijana wa kichina yuko na dada yake ,wako na kampuni yao inaitwa: HELLEN CARGO OFFICE. Address: Room 628,6/F, Zhao Qing hotel, Huanshi Zhong road. Guangzhou. China.
Anaitwa Ali Liang Zhu. Simu namba: +86 18688863469 ni ya Whatsapp pia. E-mail: aliliangchina@163.com ni vijana waaminifu sana, nime deal nao zaidi ya miaka 8. Kiasi kwamba nikiwa na order ya China sihitaji kusafiri bali ninawatumia pesa, wananunua vitu na kunitumia. Na hata sasa hivi wanayo order yangu wanaishughulikia.
Kwa hiyo unaweza kumtumia huyo kijana. Atanunua mzigo na atakutumia. Utapata msaada ambao hukutarajia.
Unaweza kuwasiliana na mimi kama utataka maelezo zaidi. Joseph Ryoba. Tel: 0754377397, 0789531559 or 0787538394(Whatsapp). E-mail: ryobaus@gmail.com
 
Ninahitaji kununua kifaa tiba fulani toka katika kampuni ya Maya medical equipment limited yenye anwani hii hapa:No 10, Haiyue building ,HaiBin garden, Shangjiao Dashi town, Panyu Area,Guangzhou,China. Je kuna mtu mwenye taarifa au uzoefu wa kununua vitu kwa mtandao toka China? Naogopa kulizwa na hawa jamaa!
Kuna kampuni hua inajitatangza kupitia channel ten, ipo china na dar kwa ajili ya kusafirisha vifurushi. jaribu kuulizia.
 
Back
Top Bottom