msaada,gari hii nitaitoa bandarini kwa Tsh ngapi?

mimi sijaelewa hapa yani hiyo Tsh. 6,845,310 ni itakayo mkosti kama kodi tu, ukitoa CIF au inclusive coz CIF yenyewe inazidi hiyo ulotaja ...ufafanuzi mkuu miye nataka kununua gari ila nashindwa pakupata maelezo sahihi. nisije lifikisha hapa likanishinda
nadhani jumla ni kama milioni 17hivi
 
Retail Selling Price46,463
Depreciation70%
Freight 1,227
Customs value 6,873
FOB Value 5,646
Import Duty 25% 1,718
Excise Base 8,591
Excise Duty 10% 859
VAT Base 9,450
VAT 18% 1,701
Total Taxes usd 4,278
Total Taxes in TSHs6,845,310

polisi! please naamini hii details ni muhimu, naamini hizo fugure zipo kwenye USD ila chini umemalizia (jumla) katika Tshs. Je hizo kodi zinatozwa katik USD au Tshs? je hizo % (kodi=VAT,excise duty,depreciation)zinatozwa katika figure zipi,?=retails selling price,FOB, CIF, etc? sijui kama nimeeleweka, tujuze maana wengine bado tunajiandaa, swali lingine je ni bora kuagiza gari nje au ninunue hapahapa TZ?
 
sijakuelewa mkuu hebu nifafanulie . nataka kuagiza kupitia hiyo kampuni ya tradeview. vipi hiyo kampuni ni ya uhakika . i mean siyo matapeli? naomba unifafanulie au na mwingine yeyote anayeifahamu
 
escudo - tl52w
≥ 2003
2000
petrol
77,321
hii ni ya zamani kidogo TRA wametoa RSP list nyingine almost a month sas ambayo ipo more recent bei zake zipo chini kidogo, mimi niliagiza swift 1.3 ya 2003, RSP ya zamani ilikuwa USD21,500, ila RSP ya karibuni ni kama USD 15,000. Nafkiri polisi yupo sawa
 
Badilisha hiyo hela uliyotuma kwa bei ya madafu, kwa hiyo itakugharimu robotatu yake. ila uhakikishe unafanya juhudi sana kuitoa kabla ya siku 7 ikizidi hapo storage ni dola 30 kwa siku

kwa hiyo inamaanisha nikinunua gari CIF ikawa kama tsh. mil 3 nitafte nyingine kama mil 2.5 inakuwa road tayari? msaada sijawai nunua gari japan sababu yakutokuwa na taarifa kamili...nimechoka third hand cars
 
wadau naombeni msaada wenu,nataka kununua hii gari
2003 Suzuki Escudo MANUAL,ALLOY RIM

na
CIF Dar Es Salaam USD 6490
mchanganuo upo hivi;

1.FOB-4811,
2.Freight-1227
3.Insurance-50,
4.Inspection-400
Total 6490USD
JE ITANIGHARIMU TSH NGAPI KWA TRA NA KUITOA

04.jpg

Specific information

More Photos
VIN(Vehicle Identification Number)/Serial No.
TL25W-203***Full VIN/Serial No. will be shown on Proforma Invoice and Invoice
Exterior Color
Pearl
BodyStyle1
SUV
Interior Color
Beige
BodyStyle2
-
Expiry Date
Nov / 14 / 2012 (JST)
Door
5
Condition
Used
Number Of Passengers
5
Drive Type
4wheel drive
Dimension
4155×1780×1740=12.87m[SUP]3[/SUP]
ReferenceNo
121015164337
Options
Anti-Lock Brakes / Driver Airbag / Passenger Airbag / Power Windows / Rear Window Defroster / Rear Window Wiper / Tinted Glass / A/C:front / Power Steering / Remote Keyless Entry / Tilt Wheel / Digital Meter / AM/FM Radio / CD Player / Alloy Wheels / Power Door Locks / Power Mirrors / No accidents
Comment
☆AUCTION GRADE 3.5
☆NO ACCIDENT HISTORY
☆VERY CLEAN CAR
☆VERY GOOD CONDITION
☆OUT SIDE INSIDE CLEAN
☆CD,MD
☆FRONT AUTO A/C
☆LEVELIZER HEAD LIGHT
☆KEY LESS ENTRY
☆FOG LAMP
☆MUST SEE
☆LOOKS & RUNS GREAT
☆NICE ORIGINAL ALLOY RIM
☆REAR SPOILER

[h=1]Ingia kwenye website hii : www.gariyangu.com[/h]hapo chini ni bei ya hiyo gari yako, siku hizi TRA hawaangalii umelipa kiasi gani wao wakipata aina ya gari, model, mwaka , na CC za engine unapata gharama za kodi utakayolipia TRA. gharama za clearing agency haimo. hapo chini nimekufanyia estimate isipokua sina uhakika na cc za engine ya gari yako. kama si 2000, rekebisha then utapata gharama sahihi.

Many of us want to import cars to Tanzania, but we don't know where to begin.

Some of us have been lucky enough to import cars with no problems, while some
have faced a lot of problems while clearing them from the port (and same have
abandoned their cars at the port), and some have been coned and sellers
disappeared without trace after money was sent.

Despite all that, importing a car can be the easiest option for you to own
one, and experience tells us that its safe if done with care. This website tries
to guide you so that u can import your car safely, and help u estimate total
costs u will have to bear so that u can prepare yourself and clear it at the
port.

To start with follow this importing guide.

[h=2]Tax Estimator[/h]
Use
the calculator below to estimate the amount of tax you will have to pay for your
imported car

CurrencyUSDGBPTZSExchange Rate
Make/Model
Tax ProfileNon-UtilityPickupsTrucks ( 5tons-18.5tons)Trucks ( above
18.5tons)Tractors(trucks for pulling semi
trailers)Buses (from 10 passengers)Land cruiser Hard tops carrying from 10
passengers
Car Year
Displacement (cc)

Customs Value3,858.60 USD
Import Duty964.65 USD
Dumping Fee0.00 USD
Excise Duty482.32 USD
VAT955.00 USD
Total Taxes2,401.97
USD
 
polisi! please naamini hii details ni muhimu, naamini hizo fugure zipo kwenye USD ila chini umemalizia (jumla) katika Tshs. Je hizo kodi zinatozwa katik USD au Tshs? je hizo % (kodi=VAT,excise duty,depreciation)zinatozwa katika figure zipi,?=retails selling price,FOB, CIF, etc? sijui kama nimeeleweka, tujuze maana wengine bado tunajiandaa, swali lingine je ni bora kuagiza gari nje au ninunue hapahapa TZ?

1. Malipo TRA hufanyika kwa shilingi za kitanzania ila TRA huanza kwa kukokotoa customs value ambayo huwa katika dollar, kisha wanapigia exchange rate ya siku hiyo ambayo huwa iko chini kuliko za kwenye bureau.
2. Kodi inatozwa kwenye base value kama alivyoonyesha Polisi. Kwa mfano Excise Duty 10% inaokana na customs value kujumlisha 25% ya import duty.
3. Kuagiza ama kutoagiza inategemea vitu vingi kidogo.
- Kwa mfano budget yako ikoje, magari mengi yauzwayo na watu binafsi huwa yamepita kwa watumiaji angalau wawili hivyo bei huwa chini. Shida yake hutoambiwa gari ina tatizo gani zaidi sana utaelezwa "naenda masomoni au kuna gari nimeagiza iko bandarini au namalizia ujenzi, gari ya wife ameichoka......" kumbe gari linakunywa mafuta kama jini..
- Kuna yard zipo dar na mikoani magari yanauzwa..Hapa kuna tatizo moja tu...Uhakika wa unachonunua yakupasa uwe makini maana bongo kwa makarateee ni sawa na uji kwa mgonjwa. Uzuri wake ni kwamba hubebi risk ya kuagiza gari Japan ambayo huna uhakika itakuja na ikija itakuwa sawa na uloiona kwenye mtandao.

Binafsi nina uzoefu wa zote na hakuna ktk isiyo na mushkeli cha msingi ni kuchukua tahadhari kwa risk zinazojulikana...
 
mimi sijaelewa hapa yani hiyo Tsh. 6,845,310 ni itakayo mkosti kama kodi tu, ukitoa CIF au inclusive coz CIF yenyewe inazidi hiyo ulotaja ...ufafanuzi mkuu miye nataka kununua gari ila nashindwa pakupata maelezo sahihi. nisije lifikisha hapa likanishinda
Mkuum ni kodi tu achilia mbali gharama ya kulifikisha gaari bandarini yaani CIF. Kama ulivyoona hapo juu
Import duty usd 1,718
Excise duty usd 859
VAT usd 1,701
JUMLA usd 4, 278
Kwa hiyo ukabadilisha kwa hela yetu, mimi niliweka usd/ths = 1,600 ndo unapata sh. 6,845,310. Na hiyo bado hajalitoa gari maana kuna makolokolo mengine mengi kama vile ushuru wa bandari, usajili n.k
 
polisi
ukiona watu wanaendesha gari nzuri mjini ujue pesa imewatoka,si unaona hiyo gari ilivyokuwa juu,
 
Thanks mkuu, nitaku-PM ikifika wakati nikiwa tayari nipate ushauri zaidi
1. Malipo TRA hufanyika kwa shilingi za kitanzania ila TRA huanza kwa kukokotoa customs value ambayo huwa katika dollar, kisha wanapigia exchange rate ya siku hiyo ambayo huwa iko chini kuliko za kwenye bureau.
2. Kodi inatozwa kwenye base value kama alivyoonyesha Polisi. Kwa mfano Excise Duty 10% inaokana na customs value kujumlisha 25% ya import duty.
3. Kuagiza ama kutoagiza inategemea vitu vingi kidogo.
- Kwa mfano budget yako ikoje, magari mengi yauzwayo na watu binafsi huwa yamepita kwa watumiaji angalau wawili hivyo bei huwa chini. Shida yake hutoambiwa gari ina tatizo gani zaidi sana utaelezwa "naenda masomoni au kuna gari nimeagiza iko bandarini au namalizia ujenzi, gari ya wife ameichoka......" kumbe gari linakunywa mafuta kama jini..
- Kuna yard zipo dar na mikoani magari yanauzwa..Hapa kuna tatizo moja tu...Uhakika wa unachonunua yakupasa uwe makini maana bongo kwa makarateee ni sawa na uji kwa mgonjwa. Uzuri wake ni kwamba hubebi risk ya kuagiza gari Japan ambayo huna uhakika itakuja na ikija itakuwa sawa na uloiona kwenye mtandao.

Binafsi nina uzoefu wa zote na hakuna ktk isiyo na mushkeli cha msingi ni kuchukua tahadhari kwa risk zinazojulikana...
 
Mkuum ni kodi tu achilia mbali gharama ya kulifikisha gaari bandarini yaani CIF. Kama ulivyoona hapo juu
Import duty usd 1,718
Excise duty usd 859
VAT usd 1,701
JUMLA usd 4, 278
Kwa hiyo ukabadilisha kwa hela yetu, mimi niliweka usd/ths = 1,600 ndo unapata sh. 6,845,310. Na hiyo bado hajalitoa gari maana kuna makolokolo mengine mengi kama vile ushuru wa bandari, usajili n.k

yani natamani gari ila nahofiaga pale bandarini nisije liacha, niliwai kupata swift kali mpaka linafika ilikuwa kama mil 3 hivi kwa makadrio lakini kwasababu yakutojua kodi nikaona isije nikatokwa milioni 6 nyingine hapa mpaka linakaa road. haha ha aha
 
Kiongozi kwa sasa ni rahisi sana kukadiria gharama ya gari unaloagiza hata kabla hujalipia tofauti na zamani ambapo ushuru ulitegemea assessment ya customs officer (rushwa).

Ukiondoa kodi za serikali kuna gharama zingine kama:
- Other charges za tra (e.g registration) sio zaidi ya shs. 350,000
- Shipping line Usd 70 hadi USd 85 inategemea na ukubwa wa gari (CBM)
- Port charges kama hakuna storage charges (shs. 250,000 hadi shs. 500,000) hutegemea ukubwa wa gari pia
- Number plates shs 38,000 (Masasi Signwriters)
- Clearing Agents wanagonga hadi Usd 250 kwa gari ila mimi hulipa about shs. 200,000. Kuna kitu clearing agents wanaita facilitation fee usilipe unless documents zako zina mushkeli...
KWA KAWAIDA HAIZIDI MILIONI...

Pia kuna Insurance: comprehensive 3% ya thamani ya gari; 3rd party hata sh.40,000 unapata

Kwa hiyo usiogope sana cha msingi (kwa mtazamo wangu) USIKOPE BANK ILI KUNUNUA GARI ya kutembelea iwapo haitakusaidia kuongeza kipato chako ama ufanisi ktk kazi zako.
 
mkuu hapo kwenye red, kwa sie walala hoi kununua gar km hiyo ya mshkaj inaonekana ni zaidi ya mill 14, je tunaweza kuweka vipato vyetu mpaka kufikia hapo?, au ndo tusahai mambo ya magari?
 
Mabreka,

Sidhani kama u-mmoja wa wanaotaka kununua gari kwa vile jirani yangu kanunua...

Mimi ni muumini wa "kula kutokana na jasho" kwa maana ya kipato halali.
Kama gari haitakuongezea kipato wala kuongeza ufanisi wa shughuli zako unataka gari ya nini iwapo hata kipato ulicho nacho sasa hakikidhi mahitaji yako muhimu???

Budget ya gari inaweza ikazidi hata budget ya chakula nyumbani.....sasa kwa nini niwalishe watoto kauzu kisa baba anaendesha "alteza".

Sasa engineer mtorela yeye pengine uwezo wake ni hiyo 14m, wewe tafuta iliyo ndani ya uwezo wako maana vidole havilingani...

Ukiweka nia na malengo thabiti unaweza kufanya mambo makubwa kuliko hata thamani ya magari tunayoongelea hapa.....
 
thanx for grat information mkuu...umenitia moyo sana. thanx in advance

Kiongozi kwa sasa ni rahisi sana kukadiria gharama ya gari unaloagiza hata kabla hujalipia tofauti na zamani ambapo ushuru ulitegemea assessment ya customs officer (rushwa).

Ukiondoa kodi za serikali kuna gharama zingine kama:
- Other charges za tra (e.g registration) sio zaidi ya shs. 350,000
- Shipping line Usd 70 hadi USd 85 inategemea na ukubwa wa gari (CBM)
- Port charges kama hakuna storage charges (shs. 250,000 hadi shs. 500,000) hutegemea ukubwa wa gari pia
- Number plates shs 38,000 (Masasi Signwriters)
- Clearing Agents wanagonga hadi Usd 250 kwa gari ila mimi hulipa about shs. 200,000. Kuna kitu clearing agents wanaita facilitation fee usilipe unless documents zako zina mushkeli...
KWA KAWAIDA HAIZIDI MILIONI...

Pia kuna Insurance: comprehensive 3% ya thamani ya gari; 3rd party hata sh.40,000 unapata

Kwa hiyo usiogope sana cha msingi (kwa mtazamo wangu) USIKOPE BANK ILI KUNUNUA GARI ya kutembelea iwapo haitakusaidia kuongeza kipato chako ama ufanisi ktk kazi zako.
 
Kiongozi kwa sasa ni rahisi sana kukadiria gharama ya gari unaloagiza hata kabla hujalipia tofauti na zamani ambapo ushuru ulitegemea assessment ya customs officer (rushwa).
Kwa hiyo sasa hivi bandarini hakuna rushwa?

Clearing Agents wanagonga hadi ...KWA KAWAIDA HAIZIDI MILIONI...
Clearing agent kazi yake nini? Hivi ukiwa na hela yote ambayo TRA wanataka, na unajua kujaza fomu (tuseme hata kama hujui kusoma na kuandika, manake mahesabu yote wanafanya wao, inabidi wao TRA ndio wafanye paper work yote, hivi hapo clearing agent wa nini?

Kwa hiyo usiogope sana cha msingi (kwa mtazamo wangu) USIKOPE BANK ILI KUNUNUA GARI ya kutembelea iwapo haitakusaidia kuongeza kipato chako ama ufanisi ktk kazi zako.
Kwa hiyo kama unaweza kupanda dala dala na ukawahi kazini kila siku na ufanisi ukawa pale pale basi usi finance gari? Udandie madala dala maisha?
 
Kwa hiyo sasa hivi bandarini hakuna rushwa?

Kwa kweli kama doc ziko kamili sioni kwa nini utoe rushwa. Kwa sasa unajua unachotakiwa kulipa na una hiari ya kuweka pingamizi iwapo haukubaliani na hesabu ya afisa wa kodi, zamani ingekuchukua wiki nzima malalamiko yako kushughulikiwa jambo ambalo liliongeza gharama za storage.
Angalizo: Iwapo invoice value ni kubwa kuliko tra calculation, invoice value will apply.
Sasa kuwepo ama kutokuwepo kwa rushwa bandarini ni mjadala mwingine, kumbuka bandari ni taasisi tofauti na tra.

Clearing agent kazi yake nini? Hivi ukiwa na hela yote ambayo TRA wanataka, na unajua kujaza fomu (tuseme hata kama hujui kusoma na kuandika, manake mahesabu yote wanafanya wao, inabidi wao TRA ndio wafanye paper work yote, hivi hapo clearing agent wa nini?

Sijui kama DIY - "Do It Yourself" inawezekana ila nijuavyo mfumo wa sasa unakulazimisha kupitia kwa clearing Agent coz ndiye mwenye leseni ya uondoshaji mizigo idara ya forodha.
Niliwahi kusikia kwamba muda nao ni pesa, kutoa gari bandarini inachukua wastani wa siku 7. Ikiwa nitafanya mwenyewe manake zaidi ya siku 7 nisimamishe ratiba zingine. I would rather pay someone for that.

Kwa hiyo kama unaweza kupanda dala dala na ukawahi kazini kila siku na ufanisi ukawa pale pale basi usi finance gari? Udandie madala dala maisha?

Hoja yangu ilizungumzia kukopa ili kuongeza kipato/ufanisi (sio kuwa pale pale) na imekaa kijasiriamali zaidi ambapo inakosa mashiko ukiitazama kwa jicho la "Ponda mali kufa kwaja"....
Mwisho wa siku kila mtu amejiwekea kanuni za kiuchumi/maisha. Kwa nini unahitaji gari ndio itakuwa sababu ya kununua gari...
Umewahi kusoma/kusikia nadharia ya HIERARCHY OF NEEDS???
450px-Maslow%27s_Hierarchy_of_Needs.svg.png
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom