Watu wakizibiana mwisho wa siku na yeye watamzibia. ..kukomoanaWatu bwana. Ati weka ukuta. Hata jirani? Sasa atakuwa jirani wa JF? Zungumzeni. Mpe sehemu ya kupita, hata kama hawezi ku afford.
Muuzie hyo njia,sio vizuri kuwa na uhasama na jirani yako.
Ushauri mzuri sana huu. Wakati mwingine ukiangalia binadamu tunavyogombania ardhi na kujimilikisha utadhani tutadumu hapa duniani milele kumbe kaeneo tunakohitaji ni kadogo sana kakuchimbiwa shimo la kuzikwa. Na bahati mbaya yetu tukifa tunaondolewa pale tulipokuwa tunagombania na kupelekwa mbali kabisa wakati mwingine porini na kuzikwa huko. Biblia inasema amelaaniwa yule agombaniaye ardhi.Hata ukiweka ukuta utakufa tu na kuviacha hapa duniani. Mpatie njia jirani yako kwani ndio ndugu yako
Ushari wa ajabu sana huu! kwahiyo akishamuuzia njia hiyo hela ndo atatumia milele au? unahisi kufanya hivyo kutaleta suluhu? thamani ya ujirani itakuwepo tena?
Mkuu Saitot ulishaona wapi mtu kanunua njia ya kupita??? kiwanja chako kipo kwenye disorganized habitat, jifunze namna nzuri ya kuishi uswahilini vinginevyo hutakaa na amani!! tafuta eneo jingine uweka hiyo project yako.
Mpende jirani yako kama nafsi yako life is easy man!!! :what:
Ushauri mzuri sana huu. Wakati mwingine ukiangalia binadamu tunavyogombania ardhi na kujimilikisha utadhani tutadumu hapa duniani milele kumbe kaeneo tunakohitaji ni kadogo sana kakuchimbiwa shimo la kuzikwa. Na bahati mbaya yetu tukifa tunaondolewa pale tulipokuwa tunagombania na kupelekwa mbali kabisa wakati mwingine porini na kuzikwa huko. Biblia inasema amelaaniwa yule agombaniaye ardhi. Kweli ni laana. Tukifa tunachimbiwa chini ya ardhi na kuzikwa huko hivyo ardhi inatumeza na kupotea kabisa juu ya uso wa dunia. Itatufaa nini kugombania ardhi ambayo kwayo tunapita tu? Nikifaika hapa huwa namkumbuka sana Nyerere alijua kuwa duniani tunapita tu. Enzi zake hakukuwa na mtu wa kumhoji hivyo angeweza hata kuambua kuchukua ardhi yote kutoka Ubungo mpaka Kiluvya na likaitwa eneo la rais. Nani angeligusa? Lakini mzee akapiga kazi pale akarudi zake kijijini kwake ha hatimaye kuzikwa huko. Ingemfaa nini leo kama angejimilikisha ardhi kubwa kama nilivyo sema halafu kumbe hatuwezi kuishi hata miaka 100. Samba Mapangala anasema dunia tunapita, binadamu ni mchanga, ... itabaki milele ni milima... Ubarikiwe mkuu.