Mrisho Ngassa, Kiggi Makassy waongezwa U-23 kuikanili Cameroon

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
KOCHA wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23, Jamhuri Kiwhelu 'Julio' ameongeza wachezaji saba katika kikosi chake ili kukiongezea nguvu kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa kutafuta nafasi ya kucheza mashindano ya Olimpiki dhidi ya timu ya Cameroon utakaofanyika Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi kwa niaba ya kocha huyo msemaji wa Shirikisho la soka nchini, Boniface Wambura alisema kulingana na umuhimu wa mchezo huo kocha wa timu hiyo ameongeza wachezaji saba katika kikosi hicho.

Wambura aliwataja wachezaji hao kuwa ni Mrisho Ngasa kutoka katika timu ya Azam ,Kigi Makasi wa Yanga ,David Luhende kutoka katika timu ya Kagera Sugar ,Jabiri Azizi wa Azam, Calvin Charles wa Simba Ally Lundenga wa Kagera Sugar na Juma Abdul wa mtibwa Sugar.

"Kulingana na umuhimu wa mchezo huo mwalimu ameona aongeze nguvu kwa kuwaita wachezaji hao, Kwa kuwa kigezo cha kucheza katika timu ya vijana ni umri hivyo hilo la kuwaongeza wachezaji hao siyo tatizo,"alisema Wambura.

Wakati huo huo, Shirikisho la Soka Tanzania TFF limetangaza viingilio vya mechi hiyo ambapo kiingilio cha juu kitakuwa ni shilingi 10,000 na kiingilio cha chini ni shilingi 1000.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema mashabiki watakaokaa kwenye viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa ndio watalipa shilingi 1000.

Alifafanua kuwa mashabiki watakaokaa VIP B na C kiingilio kitakuwa ni shilingi 5000 na jukwaa la VIP A lenye viti 745 kiingilio kitakuwa ni shilingi 10,000.

Alisema kuwa tiketi za mchezo huo ambao utapigwa kwenye uwanja wa taifa kuanzia saa kumi jioni zinauzwa katika vituo vya OilCom Ubungo ,Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa ,Mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora na Ohio.Aidha aliyataja maeneo mengine ambayo tiketi hizo zinauzwa kuwa ni pamoja na Big Bon Msimbazi Kariakoo na Uwanja wa Uhuru.

Alisema kuwa timu ya Kameroon imewasili juzi saa tano usiku na ndegeya Kenya Air Ways ikiwa na wachezaji 23 na imefikia katikas Hoteli ya Paradise
iliyopo Posta Jijini Dar es Salaam na itakuwa inafanya mazoezi katika uwanja wa Karume.
 
Tanzania uchakachuaji ni kila sehemu..... Ngassa ni under 23?????????? I doubt that though I cant establish and prove..... Ila kwa muonekano, ukomavu wa kisoka etc nachelea kusema Ngassa ain't under 23......... Early 2000's (mwaka nimesahau) tulichakachua Serengeti Boys kukanyimwa nafasi though tulipita..... Naona bomu lile lile tunalitengeneza............ Why can't we learn from our mistakes? Nauliza kwanini historia haiwi mwalimu wetu wa kujifunza?
 
Ni kweli kabisa mdau haiingii akilini Ngassa awe ana umri chini ya miaka 23 ina maana amezaliwa 1990 I cant buy it???
 
Ngasa amecheza ligi kuu kwa karibu miaka 6 then yuko u23 ?
 
Kwa mwendo huu tunategemea soka la Bongo litaendelea? Yaani jamaa anakaribia kustaafu soka leo mnamchagua U-23 team!!!
 
nyie ndio mama yake? au nyie ndio manesi mliomzalisha? siri hii anaijua yeye na mama yake tu.
angalia wachezaji wa africa wanaocheza ulaya wanavyofoji umrikama documents zake zinaonyesha huo umri basi period
 
Logic tu. Ndio tuseme alinza kucheza Premier League na miaka 17?
 
nyie ndio mama yake? au nyie ndio manesi mliomzalisha? siri hii anaijua yeye na mama yake tu.
angalia wachezaji wa africa wanaocheza ulaya wanavyofoji umrikama documents zake zinaonyesha huo umri basi period

Mapovu yote ya nini wakati jibu unalo?
Hao wachezaji wa Afrika wanaocheza Ulaya wewe ndie mama yao? Umejuaje kama wamefoji umri?
Yaani kwa vile nchi zingine zinadanganya umri basi nasi tufanye hivyo?
Watanzania hawajifunzi kutokana na makosa ya nyuma. Si unakumbuka kilichowapata wale vijana miaka michache iliyopita??
 
nyie ndio mama yake? au nyie ndio manesi mliomzalisha? siri hii anaijua yeye na mama yake tu.
angalia wachezaji wa africa wanaocheza ulaya wanavyofoji umrikama documents zake zinaonyesha huo umri basi period

Tatizo tunafoji kizembe, tunakamatwa kirahisi. Najiuliza, kama kweli ana umri chini ya 23 miaka yote tulikua wapi kumchagua timu ya vijana????
 
Iwe ukweli au si ukweli Ngassa ni kababu tu wakati anaenda kufanya majaribio west ham walisema ana miaka twenty three mpaka leo ana mingapi?inamaana miaka yake haiongezeki tunawanyima vijana wengine nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwa sababu ya kuendekeza vibabu,Tz nzima kweli hao ndo wanaofaa kuongeza hebu Julio badilika kaka ,unajitia aibu mwenyewe!
 
Inawezekana akawa na 23, nafikiri khalfan ngassa alikuwa kwenye peak kipindi cha miaka ya 90, i assume ndipo mama yake mrisho alipodanganyika!
 
Ok, wapenda mpira, navyojua kuna sheria inaruhusu kuwa na wachezaji 3 wenye umri zaidi ya miaka 23 katika timu. Ambacho sina uhakika nacho ni kama hii sheria inatumika katika steji hii ya mashindano kuelekea Olimpiki, ila katika fainali zenyewe, wanaruhusu hao wachezaji 3.
Kabla hatujarusha madongo, tujaribu kufahamu sheria inasema vipi.
 
Back
Top Bottom