Mrejesho: Ninadaiwa kodi ya nyumba na sina kazi kwa sasa, msamaria mwema nisaidie

Kwa mazingira ya mrejesho huu na Kwanjinsi nilivyo ongea naye anaonekana ni mwaminifu kama kuna mtu ana kazi ya kumpa mpeni abadilishe maisha yake pia,
 
yeah, kuna mdau wa kimara aliahid kumpa bati 12 kuukuu, na mwingine akaahidi kuzifikisha tegeta maana ana route ya kwenda wazo kuchukua kifusi. hizo bati siyo za kuacha poti, zitapigwa chumba cha watoto na kuzibwa vizuri tu

Hizi zinafaa azitumie halafu hiyo 150000/-ambayo Angelina mabati afanye mtaji wa genge na matunda sasa hv atasahau
 
Nami niseme tu ASANTENI wana jf kwa kumsaidia ndugu yetu japo me sikuwa vizuri ningechangia.Mungu awabariki.
 
Sikujua kama hili lingeweza kufanyika..! Tujipe hongera kwa ustaarabu humu jamvini..! Mungu ni Mkubwa.!
 
mda mrefu nilikuwa offline sikuiona hii...
but nawaombea sana wadau mliotoa Mungu awazidishie zaidi, na mleta mada Mungu akutangulie na kukutatulia changamoto ya kimaisha unayopitia.
Amen
 
JF...??????....!!!!!!
I salute you. Baraka nazimwaga kwenu wote mliomsaidia huyu mwenzetu Fundi Ujenzi. Nimeona hapo juu amesema leo kashindwa kwenda kununua bati kwa sababu anamsaidia fundi ujenzi kazi nyumba ya jirani. Huu ndio upendo wa kweli unaotakiwa. Hongereni sana.



Ulitakiwa hizo "Baraka" zako uzimwage kwa waliotoa na wasiotoa,coz ambao hawajatoa hujui nao wapo katika hali gani kifedha kwa muda huu!

Wewe umebagua na kuchagua waliotoa tu! Asiyetoa leo pengine anaweza akatoa kesho.
 
JF imeweza kusaidia watu wengi wenye shida mbalimbali,tunashukuru ndugu kwa kutuletea mrejesho na tunawashukuru wale wote walioguswa na Hili suala lako.
 
Mkuu Mkongoro pole sana na hongera kwa msaada uliyoupata,naisifu familia yako hasa mkeo kwa kusimama na wewe pamoja na changamoto yote hiyo,hakika umepata mke,Mungu awabariki muishi kwa amani,

Mambo yako yakitengemaa malipo mazuri ni kwa wewe kusaidia binadamu wengine wenye shida.
 
Mkuu Mkongoro pole sana na hongera kwa msaada uliyoupata,naisifu familia yako hasa mkeo kwa kusimama na wewe pamoja na changamoto yote hiyo,hakika umepata mke,Mungu awabariki muishi kwa amani,

Mambo yako yakitengemaa malipo mazuri ni kwa wewe kusaidia binadamu wengine wenye shida.

Sidhani kama post yake ya kwanza uliisoma.


In short mkewe alishafariki. R.I.P
 
Wabarikiwe wote waliotoa na wale waliotamani kutoa ila kwanamna moja au nyingine wameshindwa Mungu awabariki pia. No yako naisev mkuu nitakuona mwisho wa mwezi huu
 
Ikiwekwa mada ya "ni kituo gani cha kujaza mafuta kwenye gari ambacho hawaibi" hawa hawa wana jf kila mtu atasifia ni wapi anajaza hawaibi na wapi wanaiba. Ikija ya kupanda ndege ni hawa hawa wanajua Mashirika yote ulimwenguni na nauli zake. Kivumbi mada ya mchango weee!!! Utasikia sipo vizuri, mara na mimi yalishanikuta jipange. Kifupi kwa waliomchangia wengi hawaja comment hapa. Maana jf kila mtu ana nyumba kila mtu ana gari teh.Full ULIMBUKENI.
 
mkuu cjaelewa hapo kwenye western union iyo ni milioni moja na laki mbili au laki moja na ishirini maake huo mkato cjaelewa hapo ulipo uweka
but MSHUKURU MUNGU KWA UPENDO ULIONYESHWA NA HAYA MAMBO YANAPATIKANA TANZANIA AMBAPO MTU ANAEZA KUMSAIDIA MTU ASIE MJUA ..... ASANTEE SANA

Mamoja,makumi,mamia,maelfu,malaki,mamilioni...mkuu hii kitu inafundishwa darasa la tatu kama sikosei.usiniambie uliogopa umande
 
Back
Top Bottom