Mrejesho....nimwambie mjomba wake?

huenda mke mwenzako huyo fanya utafit kimya kimya. usisahau mrejesho

 
Una complicate sana Mambo wewe au ndo huna vitu vya msingi vya kukuumiza kichwa ???

Mnapendaga ligi za kijingaaaaaaaa na kuona mna tabia nzuri dhidi ya wanawake wenzenu kila mkikutana wawili sehemu Moja basi lazima muanzishe stress eneo likose amani

Hapo nachoona wewe huwezi kukaa na mtu mwingine bila kumtoa kasoro toka uzi wa mwanzo ulionyesha Ni complicater au huyu binti Ni mzuri sana kakupita ???? hahahaahah....huyo n mtoto tu treat her like a child Tena kama mwanao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juma lililopita nimeona taarifa ya habari wakiripoti baba kumtia mimba bintiye na mwingine kamuingilia kingono bintiye, zote ni usukumani hukooo
 
Unaonekana ni mwanamke mnyonge sana na hujui kusimamia nafasi yako katika mahusiano.

Pengine makosa ni yako ila unapenda kuonyesha umeonewa au Pengine umeshamwonyesha huyo mwanamme unampenda/kumuhitaji sana kuliko yeye alivyo kwako. Atakupelekesha atakavyo.

Jitafakari sana la sivyo mahusiano yako na mumeo yatakufa mda si mrefu.
 
Unaonekana ni mwanamke mnyonge sana na hujui kusimamia nafasi yako katika mahusiano.

Pengine makosa ni yako ila unapenda kuonyesha umeonewa au Pengine umeshamwonyesha huyo mwanamme unampenda/kumuhitaji sana kuliko yeye alivyo kwako. Atakupelekesha atakavyo.

Jitafakari sana la sivyo mahusiano yako na mumeo yatakufa mda si mrefu.

Yuko hivyo unavyosema, jaribu kupitia profile yake utaona threads zake za 'Why Me?'
 
Natumai mko wazima wote
Siku kadhaa zilizopita nilileta thread ya mtoto wa wifi angu kuingia chumbani kwangu na kua na madaraka..

Wengi walinishaur niitishe kikao ,,nilifanya hivyo nikamwambia mjomba wake na bint akiwepo
Mjomba wake akaniambia huyu Ni bint mdogo nakushaur uwe unamwelekeza taratibu nikamwambia nimeshakaa nikaongea nae naona haelew akadai usichoke kumwelewesha
Ajabu hata mwanae hakumwambia/ hata akumkanya basi nikanyamaza tu

Kilichonishangaza leo
asubuh bint kaenda kanisan,, Kuna kitu mme wangu alikua anatafuta alivyokosa nikamwambia subir labda kipo chumba Cha bint ngoja nikakutafutie maana kabla bint ajaja tulikua tunakutumia icho chumba labda katika kuhamisha tulikisahau
Mume akasema acha niende nikaangalie mwenyewe...nikamwambia utaingiaje chumba Cha mtoto wa kike mi nipo?
Akaingia akatafuta kakuta Kuna chupi kitandan zingine, zimeanikwa hapo...bint naona yupo kwenye siku zake maana Kuna pedi pale kitandan lkn haijatumika
nikamwambia umefurahi Sasa ulivyoona??? Ajabu ananilaum Mimi ninamawazo negative yule Ni Kama mwanae so haoni ajabu kuingia chumbani kwake Wala bint kuingia chumbani kwetu
Nimechoka mwili na roho
huyu Ni ndugu yake kweli maana nilienda ukweni nilimkuta
Nilichogundua inawezekana kwao ndio tabia yao hawana privacy au nikawaida yao
Kama Kuna wasukum hum watanisaidia inawezekana kwao Ni kitu Cha kawaida ivyo wananiona mimi ndio ninamatatizo ...jumapil njema jamani hata mood yakwenda kanisan imeisha
Kama ni ngosha basi.....nenda nao taratibu Tu...
Usukumani hakunaga hizo za privacy aisee unless wasukuma waliostaarabika....
Be positive with them, waelewe wakuelewe muende sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa mbona leo hapo sioni Kosa la Mumeoo???? Yeye kaenda chumbani na wewe ukamruhusu sasa kuona hizo vyupi sio kosa lakeee ungetaka ungeenda wewe kama ni ishu ya Maadili...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejikuta nalazimika kupitia threads zako kwanza kabla sijatia neno hapa.
Kimuonekano nahisi wewe ni mwanamke mkorofi na mwenye gubu sana, yaani nahisi hata huyo unae muita mumeo tayari amesha kuchoka kwa tabia zako za kupenda kulalamika sana na kuhisi kwamba wewe ni mtu wa kuonewa tu muda wote.
Mwanaume wako amechoshwa na wewe kwasababu unaongea sana, na ndio maana anakupuuza.
Ebu ngoja niishie hapa kwanza, nikakate lock
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom