Mradi wa Uvinza–Malagarasi (Kilometa 51) umetoa ajira 216

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
Mradi wa Uvinza–Malagarasi (Kilometa 51) ambao gharama zake ni Tsh. Bilioni 62.7, ni sehemu ya barabara kutoka Kigoma, Uvinza, Malagarasi na Tabora ambapo kwa jumla urefu wake ni Kilometa 214.
IMG-20230420-WA0027.jpg

Akizungumzia mradi huo, Mhandisi Ngoko Mirumbe ambaye ni Kaimu Meneja wa TANROADS Kigoma amesema “Mgawanyo upo hivi, Kilometa 105 kwa Kigoma-Uvinza hatua ya lami ipo tayari, kipande kilichobaki kuelekea Tabora ni Kilometa 61 wakati Kilometa 51 ndio hizi zinazozungumziwa hapa na Kilometa 10 zipo Kigoma ambazo Mkandarasi anaendelea na mchakato wa ujenzi.”
IMG-20230420-WA0069.jpg

IMG-20230420-WA0046.jpg

Mradi huo ulianza Oktoba 7, 2021 imeelezwa kuwa unatarajiwa kukamilika Oktoba 7, 2023 wakati ambapo maendeleo ya ujenzi yamefikia hatua ya asilimia 31.

Mhandisi Ngoko anaeleza kuwa mradi huo umetoa ajira 216 kati yao wageni ni 21 tu na waliosalia ni wazawa.

Wakati huohuo, Mhandisi Yusuph Karela amesema wamejenga makaravati matatu katika mradi huo, kati ya hayo mawili ni makubwa na jumla kuna makaravati madogo 117 lakini ambayo yamejengwa ni 19.

Mhandisi Yusuph anasema: “Kwenye malipo tayari Mkandarasi ameshalipwa malipo ya awali Tsh. Bilioni 8, kasi yake ya ujenzi si kubwa kama ilivyotarajiwa kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo mvua lakini kwa sasa anaendelea na juhudi ili kufidia muda uliopotea.”
IMG-20230420-WA0062.jpg
IMG-20230420-WA0056.jpg
IMG-20230420-WA0039.jpg
IMG-20230420-WA0039.jpg
 
Back
Top Bottom