Mr Blue ndie alieweza kumfanya Ali Kiba aache mpira aingie kwenye sanaa ya Muziki

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Hawa watu mbali na mziki pia ni marafiki wa kitambo sana, sema wabongo tumekalili kua ili watu wawe mabest lazma wafanye ngoma nyingi za pamoja Kama ilivo kwa mwana fa na ay

STORY INAANZIA HAPA......

Kimzik Mr blue ni mkongwe Zaid kuliko alikiba na blue ndie msanii alianza mziki ktk umri mdogo kwa miaka ya nyuma Sasa baada ya Mr blue kua star na kashatoa ngoma nyingi Kali na kashatambulika ktk solo la mziki

Alikuja Abby skills na goma lake la Malia akiomba collable na mr blue,
Kweli blue akamwambia Abby amuimbue , bas Abby alivoimba ikaonekana Kuna utofaut kidogo Yan Kuna vesi ya pili ilionekana kua nzuri kuliko vesi ya kwanza
Bas ikabid blue ahoji

" Bana hii vesi ya pili mbona ni Kali mno?"
" Hii vesi bana Kuna mshikaji kaniandikia"
" Tuko wap huyo jamaa na kwann ujampa aimbe?"
" Jamaa anajua kuandika lakn hapendelei mziki yeye ni anapenda Sana kucheza mpira"

Hapa alikua anazungumziwa kiba ambapo enzi hizo alikua anacheza mpira wa miguu kabla hajaanza mziki, so vijana wa 2000. Wakiona kiba anaingia uwanjani na kucheza mpira wanahis labda ni kiki hapana, kiba alianza kua mchezaj Mpira kabla hajaingia ktk mziki

So ikabid Mr blue na Abby skills wamfate Ali kiba na mwenyewe alikua hana time na mziki Ila Mr blue alimshawish Sana na kumwambia

" Mwanangu unajua kuimba kwann tusiingie studio ukatua sauti yako?"

Bas kiba akiwa hajiamin kweli akakubal na kuimba Ile vesi yake ktk wimbo wa maria na Mungu sibasumani ngoma ikawa Kali

So tangu hapo kiba akaingia rasm ktk tasnia ya mziki na Mpira kauacha ijapo kipaji hakizeek ,had Leo kiba Mpira anaucheza na mziki anaufanya na Kama asingekua msanii bas huenda angekua mchezaj mkubwa Mana kipindi anaimba aliachana na Mpira , tunaona miaka hii ndo kiba anacheza cheza ball mara moja moja

So mziki una historia Pana na wasanii wa zaman walikua wanatoka kwa kushikana Yan flan kmatoa flan ,flan kampeleka flan studio
 
Hahaha kiba namba10 alikuwa anachezea timu yake ya mtaani kariakoo kota pale kabla hazijavunjwa tulienda piga nao game uwanjani kwao walitufunga goli kibao ilikuwa game ya watoto wa kota wa kariakoo vs watoto wa kota za bandari temeke, wao vifua wazi sisi tumetinga jezi, time flies my friends...
Baada ya game tukaenda mshangaa Abby skills...ushamba huu
 
Thanks for sharing
 
Alikuja Solo thang sehemu nilishangaaa yaani kweli muda unaenda

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hahaha kiba namba10 alikuwa anachezea timu yake ya mtaani kariakoo kota pale kabla hazijavunjwa tulienda piga nao game uwanjani kwao walitufunga goli kibao ilikuwa game ya watoto wa kota wa kariakoo vs watoto wa kota za bandari temeke, wao vifua wazi sisi tumetinga jezi, time flies my friends...
Baada ya game tukaenda mshangaa Abby skills...ushamba huu
wewe ni mtoto wa kota za bandari?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom