Mpenzi wangu hana wivu na mimi wala hayuko 'romantic' nifanyaje?

Kifanya 2021

Member
Apr 8, 2022
8
10
Jamani kama nilivyotangulia kusema hapo juu kwenye heading, naombeni Ushauri wenu kwenye Hili. Iko hivi nina mpenzi wangu ambaye tuna mda wa miezi 6+ kwenye mahusiano, japo tumekua karibu tangu 2020, ila mahusiano rasmi ni hiyo miezi 6.

Huyu mpenzi wangu nilipanga kumuoa mwishoni mwa mwaka huu au mwakani mwanzoni. Ila amekua akinichanganya kwenye baadhi ya mambo kama ifutavyo.
1. Amekua ni mtu wa kutoa sababu nyingi sana hasa pale ninapohitaji kuonana naye. NB hatukai pamoja ila ni karibu, kwa maana umbali wake ni mwendo wa masaa machache tu.

2. Kwa mda wote huu hajawahi kuniambia ananipenda. Nikimhoji, anasema mtu anaweza kukuambia hizo romantic words na bado asikupende. HIVYO yeye husema ananipenda hata kama haniambii.

3.Mawasiliano. hana ile akutafute asubuhi mchana na jioni. Bali mnaweza kuongea hata saa 11 jioni, hiyo ndiyo imetoka, usiku hataki mzungumze tena au kutakiana usiku kwema. Kwake mkiongea mara moja tu kwa siku inatosha. Kiufupi hapendi sana mawasiliano ya KILA mara.

4. Hayuko romantic sana. Neno pekee analolijua ni "mpenzi" hajawahi niita kwa neno nje zaidi ya hilo. Hata tu mpenzi wangu, mchumba wangu, or even mume wangu sijawahi sikia masikioni mwangu. Simply hana kabisa yale mambo ya kihindi

5. Haonyeshi wivu wowote wala hofu au wasiwasi juu yangu, siyo mdadisi juu ya maisha yangu kabisa

6. Usipomtafta, lazima atakutafta sana tu ila shida zake ndio hizo hapo 1-5

. UBORA WAKE. 1. Mchapa kazi, mcheshi, charming and disciplined na mkarimu
2.Anavaa vizuri/Anajua kujistiri, hababaiki, etc.
3. Siyo mlalamishi au mtu wa kupenda kesi kesi
4. Ni mwepesi sana kusamehe na kupotezea vitu, hata kama utamkosea
5. Ni mchakarikaji siyo mtu wa kubweteka.

She is 22 hasomi, yupo home since 2018 after completing form 4, I am 27, nampenda sana, ila yeye sielewi kama ananipenda kweli kulingana na sababu hapo juu.

Wazoefu naombeni mnisaidie niendelee naye au nishike hamsini zangu . Kulingana na hayo niloyaeleza hapo juu. Wakuu nipo njia panda karibuni kwa mchango wenu wadau situation kama hiyo hapo juu innakua na maana gani?
 
Jamani kama nilivyotangulia kusema hapo juu kwenye heading, naombeni Ushauri wenu kwenye Hili. Iko hivi nina mpenzi wangu ambaye tuna mda wa miezi 6+ kwenye mahusiano, japo tumekua karibu tangu 2020, ila mahusiano rasmi ni hiyo miezi 6.
Hata mm niko hvyo kwa mtu nisiempenda.. yaan hvyo hvyoo.. ila nakua nae tuu mtu huyo kwasabab fulan.. ila kumpenda .. noo
 
Nipe namba yake nimshauri kuwa anavyofanya sio vizuri then baada ya hapo utaona atakavyokuwa na hisia juu yako mkuu.

Atakupenda sana na pia atakuwa romantic kwako, namba yake ni ngapi mkuu...?
 
Jamani kama nilivyotangulia kusema hapo juu kwenye heading, naombeni Ushauri wenu kwenye Hili. Iko hivi nina mpenzi wangu ambaye tuna mda wa miezi 6+ kwenye mahusiano, japo tumekua karibu tangu 2020, ila mahusiano rasmi ni hiyo miezi 6.
Sifa za koloni langu hizi, japo mimi huwa ananiita Mume, mpenzi, mpendwa(tukigombana)

Yaani kwa sifa ulizoandika hapo hilo ni koloni langu kabisa, sema maneno ya kimahaba napewa na siku yangu ya kuzaliwa aliniletea keki ofisini na kreti ya soda
 
Haya maneno ya Romantic huwa yanapotea baada ya muda mfupi kwa hiyo isiwe kigezo sana cha kumuonea dada wa watu kuhusu simu za usiku achana nazo ni muda wa kupumzika
 
Baada ya kusoma content, nikushauri

Kama unatafuta mwanamke wa kuuzia sura na yale mahaba ndi ndi ndi,
UYO HAKUFAI ACHANA NAE HARAKA SANA.

Ila Kama unatafuta mwanamke wa kuoa na kua mama Bora wa familia yako,
UYO ANAKUFAA 100% MUOE HARAKA SANA.

Kama ujaelewa sema nikufafanulie
 
Back
Top Bottom