Mpambano Arumeru ni kama Fallujah: Mwanzo wa Safari ya CDM kuelekea 2015

MMM umesema vizuri, mimi nina hakika Nassari kihalali atashinda tena kwa kura nyingi. Mashaka yangu ni tume ambayo itachelewesha matokeo na kufanya umati wa watu ambao watakuwa na hamu ya kusubiri matokeo au kuogopa kuchakachuliwa utakapotakiwa uondoke eneo la kutangazia matokeo na hapo ndipo vurugu zitakapoanzia.
 
Kwamba cdm lazima washinde ili kuweka imani kwa wapiga kura no matter what/how... hakuna kulalamika ni lazima watumie mbinu zote.

Safi kabisa; nadhani mashabiki, wanachama na wapenzi wa CDM wakiwapa pressure viongozi wa CDM kushinda watu wangejua hakuna kuchukulia mambo kiutani utani.
 
Unarekebisha,Unakosoa,Unasuta, au unaleta mipasho?
Sidhani kama Mwanakijiji yupo kwa ajili ya kupotosha au kuleta Uzushi ni moja ya watu wenye kipaji cha juu cha uchambuzi wa habari za kitaifa au kimataifa, unajua wakati mwingine inawezekana source alizotumia ndizo zina Mushkeri lakini sio lengo lake kuupotosha umma wa JF.
One thing! Kuwa na staha mkuu wangu inawezekana lengo lako lilikua zuri lakini umeharibu kwa comments zako za shari!

Wewe unadhani MMM hawezi kujibu hadi umjibie? Hapa JF watu wanapashana habari na kama tutapashana habari zisizo na ukweli basi nini faida ya kuja hapa jamvini? mtu anayeleta habari zisizosahihi hata kama anaheshima kubwa kiasi gani ni lazima akosolewe kwa makali yote ili kulinda heshima ya JF.
 
Unapokosoa historia jaribu basi kuonesha kujua historia japo kidogo.

Hiyo vita ya iraq siyo historia kwa sababu imeisha miezi michache tu iliyopita pale ambapo majeshi ya waamerika yalivuka mpaka wa iraq kuelekea makwao kupitia kuwait. Kwa vyovyote vile maelezo uliyoandika kuhusu mpambano wa fallujah siyo sahihi labda ulitaka kusema Sadr city, eneo la mji wa bagdad ambako Ma shia chini ya uongozi wa muqtada al sadr wanatawala.
 
Back
Top Bottom