Moto wafukuta ndani ya CCM Sitta kushitakiwa NEC

Tatizo kubwa ni unafiki wa huyu mzee sitta kila wakati atakuwa kwenye hii hali, ukiamua usafi ni kwa asilimia 100, yeye analaumu tu kila kukicha, hili hali wengine ideology zetu ni 'no one is clean in ccm' aondoke tu ccm atafute sehemu nyingine, akishindwa akae kimya!!!!! yeye hana usafi wowote ule kutaka tu publicity, aacha upropaganda wake. unalaumu weee unabaki humo humo, akili hizo!!

Sidhani kama ni unafiki tu wala sidhani kama Sitta hajui kama wapo wengi wanaojua kwamba na yeye si safi. Tatizo kubwa ni kwamba hivi sasa kuna ombwe kubwa la uongozi ndani ya chama (CCM) na serikali yake kiasi kwamba watu kama akina Sitta wanapata jeuri ya "kumwaga mboga au ugali" wanapojisikia bila wasiwasi wa kuwajibishwa. Nisahihishwe. Kinachoonekana ni kwamba uongozi wa chama umegubikwa na "shaka kubwa la ukosaji" (guilty conscious) kiasi cha kukosa ubavu wa kuwawajibisha wale wote wanaokitia kidole machoni. Ni kama vile Sitta anawaambia "mtanifanya nini?" Kazi kwenu wana-CCM! :party:
 
Yaani post zako ndio zile zile zinazo assume kuwa Kikwete ni SAFI, na kuwa Kikwete na hao mafisadi hawana mawasiliano, nani kawaroga nyie?? There is no way ukamtaja EL, RA JK asiwemo katika hii three cord company, no..way, tuache kudanganyana.

Logic ndogo tu, kama JK angeamua awaondoe mafisadi anaweza, aidha kawashindwa au yuko pamoja nao, na kama ameshindwa basi sio rais kuna rais wa siri!! ni hizo possibility mbili tu, HAWAWEZI AU YUKO NAO!! na kama hawawezi na kuna rais wa siri basi Sitta asingepewa hata uwaziri kwa mujibu wa post yako. TUAMKE JAMANI hizi logic zenu zimekufa na wala hazilipi kabisa, inakuwa kama mateja wanasimuliana bwana

Rais Kikwete ni dhaifu, hana ubavu wa kuwashughulikia mafisadi, inawzekana nae ni mmoja wao ama la ananufaika na ufisadi huo ama la anawaogopa.
Lakini pia Rais Kikwete ni smart kwa kuwa anaweza kuwakumbatia makundi yote ndani ya ccm; mafisadi, wapinga ufisadi na wale wengine akina popo.
Kwahiyo sitta amepata nafasi ya kuingia kwenye cabinet kwa sababu ya usmart wa Rais JK ili kuwakumbatia makundi yote ndani ya chama akidhani atafanikiwa kuvunja makundi na kurudisha mshikamano ndani ya chama lakini akasahau kwamba hawa watu wake katika amkundi yote wamegundua udhaifu wake hana ubavu wa kuchukua hatua, ndio maana unaona wanaendelea kuparurana kila siku kila mmoja akitafuta ushindi.
 
Jambo la sitta linaweza kuchukuliwa ni issue kubwa ccm kuliko hao mafisadi rostam, chenge na wengineo hii ccm hii
 
MGEJA BADALA YA KUPELEKA KESI KWA ROSTAM AZIZI NA LOWASA, KAMNYANGANYE TU KADI YA CCM KWANI NI MZIGO MKUWA SANA KWA SITTA HIYO

Eti napeleka hoja binafi kwenye kikao cha Sisiem ambacho waamuzi wake ni Edward Lowassa na Rostam Aziz. Ndugu amka kumekucha acha kuvuta blanketi kweupe tayari Tanzania hadi vijijini!!! Hadanganywi mtu hapa tena!!!

Mgeja kama kweli wewe MUISLAMU SAFI na unayetambua kwamba maana ya UISLAMU ni SALAMA au AMANI, kwanza chukua hizo hatua zako kuelezea umma wa Tanzania juu ya USHIRIKI WAKO KWENYE KUPANGA NJAMA ZA KUWAIBIA KURA ZAO kwenye kikao chenu cha siri Hotel Lakairo huku ukijua fika kwamba kufanya hivyo ni kuliweka taifa katika HATARI kubwa kwa makusudi kabisa na pia kukiuka maana halisi ya imani hii zuri kwetu.

Nje ya hapo usitupigie kelele kwani HUMO NDANI YA SISIEM YA SASA KUNA WABUNGE WETU (Nguvu ya Umma) kibao ambao hawakubaliani na MAFISADI ktofauti na jinsi ulivyoukumbatia wewe. Cha msingi kazipitieni kadi zao za uanachama CCM ambayo kwa sasa si dili tena na kesho yake utaona VIJANA WENYE UCHUNGU tukiwachagua siku inayofuatia.

Na vilevile Mgeja, mauaji ya ajabu ajabu nchini kichinichini hatutaki kuyasikia tena hapa nchini. Na ukayafanyie kazi haya maneno vizuri kwani yeyote atakayevumishwa hata kidogo tu kuhusika na kifo cha Mtanzania yeyote tunaye ama ukoo wake jicho kwa jicho. Uchonganishi hatutaki tena.

Watanzania tuwaombee sana tena sana Dr Hosea wa PCCB (japo kafungwa mikono kufanya kazi zake kwa uhuru zaidi, ni mpambanaji wa uhakika), tumuombee Samuel Sitta na wapiganaji wetu wengine wengi mle ndani ya Sisiem ambao hatuna haja ya kuwataja majina. Na tangu sasa muangalie sana mienendo ya akina Mgeja hawa dhidi yao.

Ukiangalia Dr Hosea anachodaiwa kusema hakuisema ili apate utajiri wowote bali ni kwamba ALIUSEMA KWA UCHUNGU jinsi anavyoshindwa kufanya kazi ambayo kwa uhakika anajua fika ufanyike vipi na kwa ufanisi zaidi. Na huyo Mhadhiri wa UDSM aliyeonekana kumchochea moto Dr Hosea asisubiri kuomba radhi baada ya mambo mabaya kutokea. Ni unafiki mkubwa!!

JK mwenyewe aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akionyesha kuwagwaya MAFISADI kwamba wengine wao ni wa hatari zaidi na kwamba vita dhidi yao yahitaji UMAKINI zaidi sasa hili la Wikiliki ndio ije ionekane nongwa leo??? Sembuse yeye tumempa mamlaka yote juu ya vyombo vyetu vyote vya ulinzi na usalama na akadai hivyo je afisa wa chini tu kama Hosea anapokosa ushirikiano kwenye kazi yake aseme nini??? Tuache unafiki!!


huy jamaa ni mingoni mwa wale waliokuwa wakimlilia MNAFIKI SITTA pale KANISANI. Eti Badala ya wapiga kura wa pale Urambo kumlilia , wanamlilia WAUMINI Pale kanisani?. KUMBE KAKOSA DONGE KWA AJILI YA KANISA LAKE NA BADO ANALILILIA. POLE SITTA MBUNGE WANGU.

SITA EE! KATUJENGEE BARABARA NZURI INAYOUNGANISHA URAMBO NA KONDAMOYO. AU YA VUMILIA HADI NKOKOTO BILA KUPITIA KIJIJI CHA UHURU!!!! aaaahhh wapi! Miaka yote umekuwa mbunge hata barabara ya kutoka Tabora - Urambo umeshindwa kuweka lami seuze hizo za vijijini.
 
Mgeja ni nani katika hii nchi, kwa sitta yeye ni kama sisimizi tu hebu tupeni shule yake kwani tunaweza kumlaumu kumbe ndo upeo wake umefika mwisho kama wa makamba
 
Hili li-Mmbu Sugu linaonekana ni lichambuzi, huenda likawa na undugu wowote na yule Malaria Sugu kweli??? Moderator I & II au Rev Masanilo hebu tusaidieni kidogo hapa.

Sina nia ya kumtetea Sitta linapokuja suala la uwajibikaji wa pamoja ndani ya chama chochote, kwa mfano kauli za Zitto pia zimeonekana kukikwaza chama chake cha chadema lakini natofautiana na Mgeja kuongea suala hilo na vyombo vya habari.Badala ya kuongea na vyombo vya habari, Mgeja angelipeleka suala hilo ndani ya chama chake kwanza au kuwajulisha viongozi wake wa kitaifa kwanza juu ya kusudio lake hilo.

Hapa ni kama anarumbana na Sitta hadharani bila kujua msimamo wa chama chake juu ya suala hilo na njia ya kufanya namna ya kumshauri bwana Sitta.

Pili, Mgeja ameongea na vyombo vya habari kuhusu ajenda ambayo pengine angetakiwa kuongea katibu mkuu wa chama Yusuf Makamba ili kukiepusha chama na malalamiko kwamba kila mtu siku hizi anataka kuwa msemaji wa chama bila kuzingatia taratibu. Njia hii mara nyingi husababisha marumbano kwenye vyombo vya habari kati ya wanachama kama kila mmoja ataamua kuongea na vyombo vya habari kuelezea msimamo wake juu ya matamshi ya Sitta au jambo lingine lolote.
 
Sita

  • Amegundua na anatumia udhaifu wa JK- Kama kina chenge, alishidnwa kuwaweka pembeni mhhh
  • Ameanza Kampeni za 2015ni
  • Ana uchu wa madaraka hajardhika na nafasi aliyomegewa
  • Sitta ni mwanasiaa anataka afukuzwe uwaziri ili nyota yake kisiasa kizidi kung'aa 2015
But wataka mabadiliko wote tunapenda ndani ya CCM wawepo kina Six wengi ili wayumbe

HIi CCM imefikia pabaya Yaaani wanaona nafuu Sitta awe subject ya Kikao na sio Chenge, Rostam etc

Kwenye urais bado, siyo rahisi kuupata iingawa ni mpiganaji kwa maendeleo ya taifa
 
Sita

  • Amegundua na anatumia udhaifu wa JK- Kama kina chenge, alishidnwa kuwaweka pembeni mhhh
  • Ameanza Kampeni za 2015ni
  • Ana uchu wa madaraka hajardhika na nafasi aliyomegewa
  • Sitta ni mwanasiaa anataka afukuzwe uwaziri ili nyota yake kisiasa kizidi kung'aa 2015
But wataka mabadiliko wote tunapenda ndani ya CCM wawepo kina Six wengi ili wayumbe

HIi CCM imefikia pabaya Yaaani wanaona nafuu Sitta awe subject ya Kikao na sio Chenge, Rostam etc

Mgeja atakuwa ametumwa nadhani! Nadhani Mgeja ndo alikuwa mmoja wa viongozi wa CCM waliompongeza Bw. Chenge huko Bariadi hata baada ya Chenge kutuhumiwa Ufisadi na yeye akidai VIJISENTI.

Bw. Mgeja simlaumu kwani hajui alitendalo; wanaolijua alitendalo Mh. huyu, ni wale waliomtuma!

Bw. Sitta naye ni mnafiki pia. Kama kweli alijua Dowans na Richmond ni miongoni mwa watafuna nchi hii, mbona aliuzima mjadala husika mwishoni mwa Bunge lililopita?

Ubatili mtupu!
 
Mkianza kuongelea Mgeja mimi huwa nahisi kama mnataka kuanza kutumia treni inayoendeshwa kwa kuni wakati hii ni karne nyingine kabisa. Angejua anyamaze maana ccm ilimsaidia yeye lakini si wakati huu. R.I.P Mgeja
 
Hebu fafanua kidogo haya maoni yako hapa ndugu. Kama kuna ujumbe mzito unataka kutufahamisha juu ya JK lakini mada ikatitia kidogo kiajali ajali hivi. Ulikua unasemaje hasa kati ya JK na sisi Wananchi huku ukielekeza macho yetu kwa MAFISADI wa Yaradua vile???

Jk sio mjinga kiasi hicho (kwenye red) Anajua yaliyomkuta Umar Yaradua wa Nigeria alipopambana na mafisadi. Lakini mwaka huu kama mngempa sapoti ya kutosha basi angefanya hivyo, lakini mlichofanya ni kumhujumu ambapo ilipelekea kusaidiwa na hao mafisadi tena kuingia ikulu, sas haina haja ya kulalamika, na JK kula zako good time ikulu kwani watu wenyewe hawana shukurani hata ungefanya nini, na ikiwezekana nenda zako kabembee huko Trinidad and Tobaco. Waache waendelee kurap.
 
Tatizo kubwa ni unafiki wa huyu mzee sitta kila wakati atakuwa kwenye hii hali, ukiamua usafi ni kwa asilimia 100, yeye analaumu tu kila kukicha, hili hali wengine ideology zetu ni 'no one is clean in ccm' aondoke tu ccm atafute sehemu nyingine, akishindwa akae kimya!!!!! yeye hana usafi wowote ule kutaka tu publicity, aacha upropaganda wake. unalaumu weee unabaki humo humo, akili hizo!!

Ungekuwa unayasema haya wakati anayofanya kipenzi chako Zitto hayatofautiana na haya ningekuelewa...sasa nimeamini unaweka u friend mbele ukweli badae..mana hapa umefyatuka safi kabisa....fyatuki kwa ngozi hiihii wakati zitto akiongea nje ya vikao sio unageuka geuka haueleweki....acha mapenzi ya popo
 
Huyu sita angekuwa serious angejiondoa SISI M!

Kwa taarifa yako tu, wako watu wengi sana sana tena sana ambao WATAJIONDOA KABISA CCM ila tu ni kwamba MUDA WA KUFANYA HIVI BADO SI MUAFAKA.

Vuta kidogo subira mzee wala usipate taabu katika hili!!!!
 
Jk sio mjinga kiasi hicho (kwenye red) Anajua yaliyomkuta Umar Yaradua wa Nigeria alipopambana na mafisadi. Lakini mwaka huu kama mngempa sapoti ya kutosha basi angefanya hivyo, lakini mlichofanya ni kumhujumu ambapo ilipelekea kusaidiwa na hao mafisadi tena kuingia ikulu, sas haina haja ya kulalamika, na JK kula zako good time ikulu kwani watu wenyewe hawana shukurani hata ungefanya nini, na ikiwezekana nenda zako kabembee huko Trinidad and Tobaco. Waache waendelee kurap.

Umar alikuwa mgonjwa hata kabla ya kuchaguliwa. Sasa kufa kwake unasemaje kinahusiana na ufisadi Nigeria?? Hicho ni kichekesho. Nyie ndiyo mtakuja siku kutuambia kuanguka kwa JK ni kwa ajili ya mafisadi. Hosea kisha toa siri sasa sijui kwa nini bado watu mnataka tuamini kuwa JK bado anafight na ufisadi nchi hii.
 
Back
Top Bottom