Moshi: Mama wa Kizungu Ambae ni Mwekezaji Alia Mbele ya Makonda,Aomba Asaidiwe Baada ya Kuzulumiwa Pesa na Benki

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Makonda anazidi kukiwasha huko Moshi baada Mama wa Kizungu anaeitwa mama Sakila ambae ni Mwekezaji wa Hoteli (Sunrise Lodge) kumuomba amsaidie kupata pesa zake baada ya kuingia kwenye mgogoro na Benki ya Barclays/Absa na kwamba licha ya kesi mahakamani Bado hajapata Haki yake.

View: https://www.instagram.com/reel/C2cRCU1sPVO/?igsh=OGZvNHQwdDhubjY1

My Take
Hadi Wazungu wanajua kwamba Msaada wao ni Makonda 😂😂😂😂

View: https://youtu.be/3MjArqzE-n4?si=BFbnpYm4MACpaGsC

Hao ni Wazungu wa Kichagga.

Wapo wengi sana. Kuna baadhi wamezaliwa humo.

Wengine wapo Mji wa Elerai uliopo Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara
 
Hata wazungu kwa sasa wanajuwa kuwa Mheshimiwa Paul Makonda ndiye Rais kuanzia mwaka 2030.

Mungu mbariki sana Mheshimiwa Makonda na umlinde ,kumpigania na kumtetea wakati wote. Chochote kibaya kisiweze kujiinua mbele yake. Hila za shetani zishindwe .umpitishe na kumvusha popote pale apitapo. Maadui zake wanaomfuatilia wakapate kuangamia kama ulivyo liangamiza jeshi la pharao katikati ya bahari.
 
Kwahiyo Makonda Yuko juu ya mahakama? Na tunapowaambia kuwa mifumo yetu imeoza mbona huwa mnashupaza shingo? Yeye Makonda atapitia madai yake kwa njia ipi, au atatoa maagizo bila kujua uhalisia wa hayo madai yake?
All over Duniani Viongozi wa siasa ni kimbilio,by the way ndio watetezi wa Wananchi.

Mtendaji anafuata sheria na sheria hazina busara
 
Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani. Nakumbuka kuna watu walikuwa wanaenda kwenye mikutano ya dhalimu magu enzi za siasa za kiki, wakajifanya wanafunguka, baada ya hapo walijikuta kwenye matatizo zaidi ya mwanzo. Mfano mama mmoja huko huko Tanga anaitwa mama Shoshi, alimwaga kilio na mbwembwe zote, lakini lile tatizo lake halikutatuliwa na akageuka adui wa wote aliosema walishiriki kumnyima haki, akiwemo RPC wa Tanga.

Unafuata viongozi wa kisiasa wakusaidie, kisha baada ya kupata kiki kupitia ww unatakiwa urudi kwa wale wale waliokunyima haki halafu wanakuambia hawafanyi kazi kwa kufuata maagizo ya majukwaani! Wajinga ndio waliwao. Nakumbuka huyo Makonda akiwa Mwanza aliagiza maiti iachiwe baada ya kuzuiwa na akaagiza maiti zisiwe zinazuiwa, na Ummy Mwalimu amekuwa kila mara anatoa porojo za majukwaani kuwa maiti zisizuiwe, lakini jana muhalifu Makonda si amekutana na hayo hayo?
 
We chawa wa Mbowe kabebe bango huko 😂😂
20240123_183939.jpg
 
Back
Top Bottom