Morgan Tsvangirai alazwa hospitalini Afrika Kusini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Morgan Tsvangirai alazwa hospitalini Afrika Kusini.jpg


Kiongozi wa chama cha MDC chenye upinzani mkubwa nchini Zimbabwe, ambaye aliwai kuwa waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai, amelazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini akipewa matibabu ya saratani ya utumbo .

Chama cha MDC kimekua kikibana habari hizi kikisema kiongozi wao Morgan Changarai anasumbuliwa na machofu lakini jana Bw Changirai mwenye umri wa miaka 64 alitamka rasmi kuwa amekutikana na maradhi ya saratani ya utumbo (Colon Cancer) na kwamba ameamua kutoa habari hiyo kuhusu afya yake kwa sababu ni mtu maarufu katika jamii.

Kwa sasa Bwana Tsvangirai wiki hii imeanza rasmi kupewa matibabu ya mionzi ya saratani aina ya Chemotherapy katika Hospitali moja nchini Afrika Kusini ambayo haikutajwa jina lake .

Tetesi za kuumwa kwa Bwana Tsvangirai zilianza kuzagaa pale aliposhindwa kuhudhuria mkutano wa chama kuwahutubia wafuasi wa chama chake cha MDC, na baadaye ikaripotiwa kuwa amekuwa akiwahutubia wafuasi wake kupitia simu ya mkononi ilioyoambatanishwa kwenye kipaza sauti.
chanzo.Morgan Tsvangirai alazwa hospitalini Afrika Kusini - BBC Swahili
 
simwombei mabaya but colon canser ni mbaya kwa uhai wa binadamu, kupona kwake ni 1/20 #canser ni hatari#
 
Kuna utafiti wa waingereza ambao unasema Mugabe hatakufa....naona tsvangirai anamuacha babu anadunda
 
Morgan Tsvangirai
Ndio anaondoka masikini kidogo kidogo Afrika hakuna haki ya Kidemokrasia.....

Kweli watu mna akili kubwa wapinzani wakiumwa tatizo ni ukosefu wa demokrasia ila akiumwa Mugabe uzee unamsumbua.Tumekuwaje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom