More from WikiLeaks: Tanzania and the Fight to Stop Airbus Sale

David Mattaka baada ya kuboronga ATCL, si TISS walimvet na akapewa sinia lingine la Ubwabwa NIC na Mkwere..? Sasa kama Mkwere alijua awali jamaa anachombeza 10% kwa nini akampa "ulajui" wa ziada ATCL?

Sasa rudini kufukua archives za PPF mtajinogile!
 
Mie sioni tatizo ila jamaa wa espionage ana report anayoyaona yeye hapo, labda hilola Mataka, jee bado yupo kazini? Tazama Kikwete alivyokuwa incensed! Hapendi upuuzi, hii inaonyesha credentials za Kikwete. Best ever. Hata wa Merekani wamemsifu.
 
Watu wengine bwana, hizo ndio espionage wanazofanya wenzetu! kuna mtu humu JF aliwahi kuuliza, sisi, tunafanya nini?
Muulize ndugu yako Dr.Dr.Dr. Dr. Luteni kanali alhaji Mh. Rais wa NEC Jakaya Mrisho Kikwete eboooooooooooo??????????
 
Nafikiri Julian Asanage should be the Man of the Century...! Huyu jamaa ametufungua macho kwa kiasi kukubwa sana...!

Haya ni machache tu ambayo yaligusa interest za Wamarekani, je tukifuatilia mengine yanayohusu interests za China? Tupate a theory behind hii misaada isiokwisha kutoka China...! Walai tunaweza tukafa kabla siku zetu kwa presha...!

Long live Jilian Asanage...!
 
Mie sioni tatizo ila jamaa wa espionage ana report anayoyaona yeye hapo, labda hilola Mataka, jee bado yupo kazini? Tazama Kikwete alivyokuwa incensed! Hapendi upuuzi, hii inaonyesha credentials za Kikwete. Best ever. Hata wa Merekani wamemsifu.
Kamsifu wapi bana? wewe kichaa nini? hiyo statement inaonyesha kuwa alikuwa anaambiwa na walaji wanaoshirikiana na Kikwete bana "The presidential advisor later got back to the DCM, telling him that President Kikwete was "incensed" upon learning that senior Air Tanzania officials might be intending to profit personally from the deal." Sasa angalia alivyowamaliza hapa "(Comment: "Agents" and steep "commissions" have been at the heart of several corruption scandals here, including a BAE radar deal in which the GOT paid a 31 percent commission to a Tanzanian agent, much of which ended up in Swiss bank accounts, according to a UK Parliamentary investigation. Despite the fact that the UK shared this evidence with Tanzania's corruption board, no evident action has been taken. End Comment.)"
Wewe nini bana, Dr.Dr.Dr. Dr. Luteni kanali alhaji Mh. Rais wa NEC Jakaya Mrisho Kikwete akishirikiana na Mattaka walipanga deal hilo. Ndio sababu alipoona wamarekani wamebana ulaji kamsukuma PPF uko lazima watu walie tu na vipensheni vyao vitaliwa mpaka wakome.!
 
Nakubaliana na maneno ya Dr. slaa kuwa, kuendelea na Kikwete miaka nyingine mitano nikujitakia mahafa!!! Kikwete achia ngazi.
 
"3. (C) Subsequent to meetings with Faye, the DCM raised the issue of Air Tanzania's dealings with Boeing and Airbus in conversations with a close advisor to President Jakaya Kikwete. The DCM specifically noted Air Tanzania Managing Director and CEO, David Mattaka's unusual "suggestion" that Faye should contact a wealthy South Asian hotelier, who subsequently suggested to Faye that he would3. (C) Subsequent to meetings with Faye, the DCM raised the issue of Air Tanzania's dealings with Boeing and Airbus in conversations with a close advisor to President Jakaya Kikwete. The DCM specifically noted Air Tanzania Managing Director and CEO, David Mattaka's unusual "suggestion" that Faye should contact a wealthy South Asian hotelier, who subsequently suggested to Faye that he would need his services to need his services to"

Hivi huyo Mdosi ni nani? WhiteSands?
 
Yaani our leaders ndiyo wanakuwa wanainsist uwepo wa mamidomani?????? Lakini tunarudi palepale JK was aware of what was going on na hakuwachukulia hatua yeyote wateule wake ( Mattaka, Chenge etc.). Walikodi hiyo airbus na sasa tunadaiwa kwa mtindo ule ule wa Dowans.

Masuala yoote haya JK IS THE PROBLEM!

Not only is JK the problem, CCM is the problem and only the New Costitution that we are crying for would resolve all this!
 
Mtandao wa WikiLeaks wamlipua Mattaka

Tuesday, 04 January 2011

airtanzamataka.jpg

Mr David Mattaka

Mwandishi Wetu

Mtandao wa habari za kiuchunguzi wa WikiLeaks, umeendelea kuanika siri za ufisadi nchini na mara hii umemlipua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka.

Taarifa hizo kupitia WikiLeaks zimekuja karibu wiki mbili tangu kutolewa hadharani kwa taarifa nyingine zinazohusu Mkururugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk Edward Hoseah, akidaiwa kufichua siri za Rais Jakaya Kikwete kwamba kiongozi huyo wa nchi asingependa vigogo serikalini kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.

Lakini juzi taarifa zilizoripotiwa na mtandao huo na kunukuliwa na gazeti la New York Times zimedai kuwa Mattaka anatumia mpango wa serikali wa kulifufua upya shirika hilo kwa kununua ndege mpya, kujinufaisha.


Habari zimeeleza kuwa katika kufanikisha hilo, Mattaka anadaiwa kutaka kumtumia mfanyabiashara wa Kiasia ambaye anajihusisha na biashara za hoteli kuwa wakala wa ununuzi wa ndege hizo baina ya ATCL na Kampuni ya Boeing ya nchini Marekani.


Tuhuma hizo dhidi ya Mattaka ziko kwenye taarifa za siri za mawasiliano za ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam, zilizoripotiwa na mwanadiplomasia wa Marekani, Dk Purnell Delly.


Delly pia ndiye aliyetajwa katika taarifa za awali na mtandao wa WikiLeaks kwamba alifanya mazungumzo na Dk Hosseah.


Jana Mattaka alikiri shirika hilo kukubali kununua ndege za kampuni ya AirBus ya nchini Ufaransa, lakini akapuuza madai ya kutumia wakala kwa nia ya kujinufaisha.


"Huu ni upuuzi. Sikumbuki kufanya jambo hilo na tuhuma hizo hazina mashiko," alisema Mattaka alipokuwa akizungumza na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen.


Taarifa hiyo inamnukuu Delly akituma taarifa nchini kwake inayoilalamikia Tanzania kwamba ilikuwa na mbinu chafu ziliokuwa zikipangwa kuhakikisha kwamba ATCL inanunua ndege kutoka Kampuni ya Airbus ya Ulaya badala ya Boeing ya Marekani, hasa baada ya uongozi wa Boeing kukataa kutumika kwa mawakala.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, Kampuni ya Boeing iliwasilisha mapendekezo yake kwa ATCL sambamba na yale yaliyowasilishwa na kampuni ya Airbus, lakini wanalalamika kwamba kulikuwa na mpango wa makusudi wa upendeleo ambao unaashiria kwamba kulikuwa na "harufu ya rushwa".


Taarifa hiyo imedai kuwa ushauri wa Mattaka kumtaka Rob Faye, ambaye ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Kanda ya Afrika wa Boeing kuwasiliana na mfanyabiashara na tajiri wa Kiasia ili aweze kumsaidia kufungua milango ya biashara hiyo kwa serikali ya Tanzania "haukuwa wa kawaida".


"Faye aliukataa ushauri huo kwa malezo kwamba kampuni ya Boeing haitumii mawakala katika biashara zake, siyo tu Tanzania, bali katika nchi yoyote duniani," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza:


"Mawakala na malipo ya kamisheni ni kiini cha vitendo kadhaa vya rushwa ikiwemo ile ya rada ambayo Serikali ya Tanzania ililipwa asilimia 31 ya gharama kama kamisheni".


Kwa mujibu wa taarifa za mawasiliano baina ya uongiozi wa Boeing, ATCL na Ikulu, Rais Jakaya Kikwete "hakufurahishwa" na taarifa kwamba baadhi ya maafisa wa ATCL walitaka kujinufaisha wenyewe na mpango huo wa ununuzi wa ndege.


Agosti 9, 2007, Faye alikutana na aliyekuwa Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk Maua Daftari na Mkurugenzi wa Usafirishaji na Mawasiliano, Dk Bartholomew Rufunjo,ambao walimpa matumaini kwamba kusingekuwa na upendeleo katika mchakato wa ununuzi wa ndege hizo.


Baadaye Agosti 10, Mattaka, alimhakikishia Faye kwamba ATCL haikutumia mawakala katika ununuzi wa ndege zake, kauli ambayo Mattaka aliirudia mara kadhaa wakati wa kikao baina ya Bodi ya Wakurugenzi wa ATCL na Faye.


Faye alinukuliwa akisema kuwa huenda kumekuwa na mwasiliano baina ya Ikulu na Wizara ya Miundombinu ili kuhakikisha kwamba hakuna "mtu wa kati" katika mchakato huo.


Hata hivyo, Mattaka anadaiwa kumwambia Faye kwamba kulikuwa na shinikizo kutoka ubalozi wa Marekani nchini ili Boeing wapewe nafasi ya kuuza ndege zake ATCL.


Wasiwasi kwamba hakukuwa na uwazi katika mchakato huo unatokana na tangazo la aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge la Septemba 2, 2007 lililonukuliwa na vyombo vya habari kwamba Tanzania iko katika mpango wa kununua ndege mpya kutoka kampuni ya Airbus.


Kauli hiyo ya Chenge ilitolewa saa 48 tangu aliyekuwa balozi wa Marekani nchini, Michael Retzer kuondoka kurejea nchini kwake baada ya muda wake wa kukaa nchini kumalizika.


Hata hivyo, Chenge anadaiwa kukana kauli yake kwa kusema kwamba alinukuliwa visivyo na vyombo vya habari Septemb 7, 2007 katika kikao chake na Pully pamoja na ofisa wa uchumi katika ubalozi wa Marekani.
 
Haya sasa, kumekucha!

Shida ni kwamba Wikileaks wa watu wanajitahidi kuweka hadharani mambo machafu, lakini yakifika kwa akina Mkulu yote yanawekwa kabatini...
Mataka amebobea kwenye uzandiki, and he is kinda untouchable, naamini hakuna atakayemuuliza neno...huh!
 
Mtandao wa WikiLeaks wamlipua Mattaka Send to a friend Tuesday, 04 January 2011 10:40 0diggsdigg

Hata hivyo, Chenge anadaiwa kukana kauli yake kwa kusema kwamba alinukuliwa visivyo na vyombo vya habari Septemb 7, 2007 katika kikao chake na Pully pamoja na ofisa wa uchumi katika ubalozi wa Marekani.

Huyu Andrew Chenge mbona anahusishwa na scandal chafuchafu sana, is he credible?
 
nashindwa kuelewa kwa namna bongo za viongozi wetu zilivyo na utando wa kutoelewa waseme nini wanapokuwa na nani, hasa unapozungumza na agent wa US embassy (CIA) kutokana yanayojitokeza katika WikiLeaks.
 
Vita vya biashara hivyo na mikakati ya kawaida ya wabongo kujibufaisha.

Boeing are expensive to buy but chepaer to maintain while airbus are cheapr to buy but expensive to maintain. Mchina ndo aliyetoa fedha za kununua hizi Dash8-Q300 na ndio anayewajengea terminal 3 JNIA.

Mchina ana assembly plant ya Airbus pale Tianjin na kwakuwa yeye ndo mtoa fedha,piga ua Boeing washapigwa bao hapa ngoma zitatengenezewa China hizo ila ni hasara kwa namna flani fikiria kwenda kutrain mapilot, engineers, cabin crew kwenye completely a different aircraft si mchezo kama hela yenyewe ni ya kubabaisha.

Kingine kibaya ni suala la kwamba airbus zinamatatizo katika override ya auto-pilot ..usiombee iwe kwenye out uko hewani halafu ghafla itokee shida kwenye system na ijiambie kwamba wakati wa kutua ndo sasa. Mmekwisha hapo
 
Back
Top Bottom