I won`t resign -MagufuliHAO DAILY NEWS KWA NINI WANAANDIKA HABARI NUSU NUSU? Tunawaomba waandike maswala yote yanayohusu hili eneo, sio kuandika vitu namna hii.
Kwa sababu bado sikubaliani na sentensi kama ishirini za hapo juu za lawama kwa waziri Magufuli. Hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, kama kweli John Pombe Magufuli waziri amekosea kwa nini madiwani wa Kinondoni wasifungue kesi ili kumshitaki yeye binafsi na wizara husika.
Hata mimi napata picha nyingine Lakini unajua hata waandishi wetu wanatupotosha sana Sasa kwanini magufuli alipotoa ufanunuzi huo jana hawakumuuliza wakati wa ile Press conference pale pale kuhusu hili ambalo wamekuja kuliandika baada ya Press Conference ambapo waandishi wote walikuwa na nafasi ya kuuliza hata hili waliloliandika?Hapa kuna kitu hakipo wazi kwetu wote,Ngoja liendelea hili sakata ukweli dhahiri utajulikana.Inaonyesha Madiwani na Halmashauri wana waandishi wao na kinachonifanya niseme hili ni ile hali ya kuwa na fursa ya kuuliza swali kama hili na kumueleza Waziri kinagaubaga kwamba unapotosha umma swala liko hivi na ushahidi ni huu kwani waliacha hiyo nafasi ili hali walikuwa nayo wakati wa Press Conference yake?KM,
Nimesoma hiyo habari hapo juu nakuelewa kwanini Magufuli analalamikiwa kama Magufuli. Kumbe hati ya kiwanja cha RG ilipatikana mwaka jana tu, basi kweli tunao viongozi.
Haihitaji mtu kuwa engineer kujua kwamba sehemu kubwa ya bar ya RG ipo ndani ya hifadhi ya barabara, na hivyo uhalali wa kutaka iondolewe.
Hata hivyo, swali la kujiuliza ni Je, baada ya hii bar kuvunjwa nini kitafanyika hapo kwenye kiwanja husika????
Kama hiyo bar imesurvive miaka yote bila madhara kwa jamii, basi kwanini ivunjwe sasa????
Kuna nyumba kadhaa katika barabara hii ambapo wenye nyumba wameweka mbele ya nyumba zao (ktk eneo la hifadhi ya barabara) makontena ya biashara za bar, kuuza nguo, salons n.k., Je na hawa nao watavunjiwa maeneo yao ya biashara sambamba na RG, maana wapo eneo moja na wote wanavunja sheria????
Isije ikawa mambo ya kuwanyanyasa wawekezaji wadogo wazawa kwaajili ya kuserve interests za wawekezaji wakubwa wakigeni.
Hii issue ni ya kufuatilia mpaka kieleweke.
kwa watoto wa mjini wanaovinjari pale ROSE GARDEN wanajua rose garden imekuwepo tangu zamani pale nje ya uzio wa karakana za posta na simu...miaka ya karibuni lile eneo limenunuliwa na bwana ZK ambaye anataka kina MLATIE watoke pale nje ya eneo alilonunua ili aweze kujenga mradi mkubwa wa mamilioni ya dola utakaoajiri watu 3,000.
sasa huu ugomvi umezusha tag of war kati ya watu wanaomtetea MLATIE na wapambe na marafiki wa ZK...hakuna anayetaka kushindwa,sasa naona hawa manispaa wanamtetea ZK offcourse wanayo sababu ,huyu ni mmoja wa chanzo chao kizuri cha mapato kupitia mrahaba na kodi za mabango anazowalipa kila mwezi,pili amewashawishi kwa business plan na artistic impression aliyowapa ya kuendeleza hilo eneo....na lazima hapa mkumbuke kuwa uhusiano wa ZK na manispaa umepanuka hadi wamempa kile kituo maarufu kipya CHA MWENGE akiendeshe kibiashara ili awalipe mrahaba.