Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

ila Namuomba mkuu wa kaya amrudishe Magufuli katika wizara hiyo.

Mkuu Gembe,

Heshima mbele bro, hivi unajua ni kwa nini aliondolewa hapo miundo mbinu in the first place? Muwe basi mnauliza kwanza huyo anafaaa huko huko kwenye kitoweo!
 
Mimi sioni mantiki ya kurudisha wAtu wale kwa wale mawizarani.

Hivi ndo tuseme hakuna mtu mwengine anayeweza kufanya kazi hiyo ila wale wale waliokaa madarakani miaka iliyopita?

Tusijifunge kimawazo sana, tuwe open kujaribu na vichwa vipya pia
 
mimi sioni mantiki ya kurudisha wtu wale kwa wale mawizarani.
hivi ndo tuseme hakuna mtu mwengine anayeweza kufanya kazi hiyo ila wale wale waliokaa madarakani miaka iliyopita?
tusijifunge kimawazo sana, tuwe open kujaribu na vichwa vipya pia

Hata Mkuu wa kaya alishakuwa kiongozi toka 1975,Mbona ameendelea kurudi kuwa kiongozi??Raila Odinga alikuwa kiongozi katika kipindi cha Moi na sasa karudi tena kuwa kiongozi..Je tungeweka damu mpya??vya kale ni dhahabu.Tusiwe na mawazo mgando ya kupend avbitu vipya tu,tunahitaji kuwa na vitu vya zamani ili tuwe na mchanganyiko ulio bora.

Hizi sio Kampeni ila ni kujaribu kuangalia hatma ya barabara zetu na nchi yetu.Toka Magufuli ametoka Wizara ya Miundombnu zamani Ujenzai na Mawasiliano,hakuna mradi mpya wa barabara ulioanzishwa.
 
Mkuu Gembe,

Heshima mbele bro, hivi unajua ni kwa nini aliondolewa hapo miundo mbinu in the first place? Muwe basi mnauliza kwanza huyo anafaaa huko huko kwenye kitoweo!

Mkuu hebu nimbie ni kipi alikiharibu zaidi ya yey kutekeleza sera mbovu ya chama cha mapinduzi ya kujiuzia nyumba??

hii sera sijui nani aliiwekea??hawa ndio wakina mzee Ruhinda tu..na wale wote walioshindwa kujijenga toka zamani wakata mambo ya bure bure
 
Mkuu Gembe,

Heshima mbele bro, hivi unajua ni kwa nini aliondolewa hapo miundo mbinu in the first place? Muwe basi mnauliza kwanza huyo anafaaa huko huko kwenye kitoweo!

Mkuu Heshima mbele

Mi naomba kuuliza alifanya nini hapo miundo mbinu hadi akaondolewa? si vibaya kujua si unajua tena JF ni darasa...
 
Tupo Chuo kujifunza jinsi ya kutetetea maisha Ya watanzania ambao wengi ni masikini tunaomba mtuunge mkono kwani bila msaada wenu hatutaweza...
Mwnakijiji ,
n.b nimetumia hapa maana sijui jinsi ya kuiweka front page....

Ole,naomba uitoe hii hapa na uipeleke kunakoshusika,KWanz antie Wanafunzia wa siku hizi mmekuwa wanafiki tu,Masuala ya Msingi yanayolihusu Taifa hamyapi kipaumbele mnakuja kugomea uchaguzi wa Urais.

kaeni msome ,mamlize shule..kila Mwaka Mgomo tu,inawasaidia nini??kaeni chini mtumie diplomacy na watu wawe na nidhamu hasa kijana mdogo mtatiro.hana busara kabisa,haangalii jinsi Rais wake anavyotumia Busara kuzungumza??
 
Heshima Mbele Wakuu,

Baada ya Mhe. Chenge kushindwa kujenga hata barabara moja toka achaguliwe kuwa waziri wa Miundombinu,......Mhe. Magufuli alijitahidi sana kujenga barabara kwa kiwango cha Rami mpaka nchi ikaanza kupendeza,mojawapo ya kazi ambazo ninamsifu ni ujenzi wa barabara za Mwanza mjini ambapo hapo kabla kulikwua hakuna barabara za kiwango cha rami.aliweza kujua barabara zote kwa jina na kujua ni wapi panatakiwa papewe kipaumbele....

Binafsi nina matatizo sana na viongozi wanaopenda sana kupata attention ya media muda wote.... Kina magufuli, lowasa, mrema etc. Wanafunika udhaifu wao kwa kutumia media.
Hivi Magufuli kajenga (au hata kufikiria kuzijenga) barabara ngapi za Rukwa, Kigoma ama Tabora? Lakini vipi kuhusu Kagera au hata jimboni kwake? Mmesahau pia kwamba wabunge (wakiwa katika kikao cha ushauri cha mkoa wa kagera) walilalamika upendeleo wa wazi kwa matengenezo ya barabara jimboni kwa Mhe. JPM?
Pia naomba Mkuu FMES nitoe tongotongo kuhusu sababu zilimfanya JPM akaondolewa Ujenzi (Miundombinu ya sasa)...inawezakana kuna mengine nisiyoyajua.
 
Heshima Mbele Wakuu,

Baada ya Mhe. Chenge kushindwa kujenga hata barabara moja toka achaguliwe kuwa waziri wa Miundombinu na kwa kuwa imedhihirika kwamba tuhuma alizonazo ni nzito na amekubali kuwajibika kwa manufaa ya umma.

Huu ni wakati muafaka wa kupendekeza ni nani anafaa kuchaguliwa kuwa Waziri wa Miundombinu. Kipindi cha Awamu ya tau Mhe. Magufuli alijitahidi sana kujenga barabara kwa kiwango cha rami mpaka nchi ikaanza kupendeza, mojawapo ya kazi ambazo ninamsifu ni ujenzi wa barabara za Mwanza mjini ambapo hapo kabla kulikuwa hakuna barabara za kiwango cha rami aliweza kujua barabara zote kwa jina na kujua ni wapi panatakiwa papewe kipaumbele.

Mie nadhani kuna haja ya yeye kurudishwa ili akamalize ahadi yake ya kuweka rami barabara ya Mtwara mpaka Mwanza.

Najua chaguo la Muungwana linaweza kuwa Ezekiel Maige kwa silimia 70, ila Namuomba mkuu wa kaya amrudishe Magufuli katika wizara hiyo!

Mkuu Gembe,

Rais amkabidhi kijana mwingine hiyo nafasi. Haya mambo ya kung'ang'ania na watu wale wale ambao pamoja na kwamba ni nafuu kuliko wengine lakini hakuna la maana kubwa walilolifanya, mimi naona ni kama kupiga mark time hnapo hapo.

Tuiwe tayari kuwajaribu watu wapya ili waje na mawazo mapya ya kuijenga nchi yetu.

Najua JK amewapa vijana nafasi nyingi, hilo ni jambo jema. Inabidi aendelee, pamoja na kwamba kuna wengine wameharibu, lakini watakuja kizazi kipya ambacho kinataka maendeleo na kipo tayari kuchakarika.

Challenge ya 2010 ni kwa vijana wanaotaka maendeleo, kuamua kufanya kweli na kuwa tayari kuchukua uongozi wa nchi kwenye sehemu mbalimbali. Naamini wana JF wengi tu wanaweza wakafanya mengi mazuri kuliko viongozi wengi tu tulio nao sasa.
 
Mi naona hakuna haja ya kuiziba nafasi ya chenge, iachwe waiz tu kwa sababu nadhani atakayekuja na yeye atatoka miongoni mwao ambamo nimebaini kuwa hawataleta mabadiliko yoyote.
 
Najua JK amewapa vijana nafasi nyingi, hilo ni jambo jema. Inabidi aendelee, pamoja na kwamba kuna wengine wameharibu, lakini watakuja kizazi kipya ambacho kinataka maendeleo na kipo tayari kuchakarika.

Challenge ya 2010 ni kwa vijana wanaotaka maendeleo, kuamua kufanya kweli na kuwa tayari kuchukua uongozi wa nchi kwenye sehemu mbalimbali. Naamini wana JF wengi tu wanaweza wakafanya mengi mazuri kuliko viongozi wengi tu tulio nao sasa.

Mtanzania,
in maana unamsupport Ezekiel Maige apewe hiyo wizara??coz huyu ndiye mkulu alitaka kumpa wizara hiyo kipindi kile baada ya kuvunja baraza la mawaziri.

Na wewe unamuona Magufuli kama mtu asiyefaa??
 
heshima kwanza;
Magufuli huwa ana vision fulani akipewa kutekeleza kazi fulani; huweka plan na kujaribu implementations; ila unajua amezungukwa na watu wachafu; so hawezi; pia kumbuka kashfa dhidi ya JPM zilichongwa makusudi (tusisahau tulikotoka sera za ben na CCM ndi alikuwa anatekeleza). So nadhani walau magufuli anaweza kupiga hatua kaisi fulani ktk anaiwezea; wengine wataleta chai tu pale-
 
Karibu Malunde,

Mie nimeeleza ila nadhani na wewe u have said it again,Mzee FMES uko wapi??
 
Magufuli ndiyo kweli ali initiate ujenzi wa barabara nyingi kwa kuwatumia contractors kutoka China. Matokeo yake ni ujenzi mbovu na kuongezeka kwa costs za kujenga barabara hizo na pia kuvunja mikataba na kutafuta contractors wapi.
 
Mtanzania,
in maana unamsupport Ezekiel Maige apewe hiyo wizara??coz huyu ndiye mkulu alitaka kumpa wizara hiyo kipindi kile baada ya kuvunja baraza la mawaziri.

Na wewe unamuona Magufuli kama mtu asiyefaa??

Mkuu Gembe,

Simjui vizuri huyo kijana mwenzetu lakini ampe tu kama ana uwezo.

Magufuli kama ana uwezo si afanye mabadiliko makubwa huko huko aliko? Wizara yake ya mifugo na uvivu ni wizara muhimu mno, tuna maziwa na mito lakini bado smaki ni haba na aghali kwa sehemu mbalimbali. Ahangaike huko
ili kuongeza uzalishaji hasa kwenye uvuvi na pia kuongeza ubora wa mifugo yetu.

Mimi namkumbuka Mrema, hata umpeleke wizara gani, bado alikuwa anapata mambo
ya kuyapigania.

Magufuli ni nafuu kuliko mawaziri wengi ila bado kuna watu wengi tu ambao wanaweza kuchapa kazi kuliko yeye.
 
Magufuli ndiyo kweli ali initiate ujenzi wa barabara nyingi kwa kuwatumia contractors kutoka China. Matokeo yake ni ujenzi mbovu na kuongezeka kwa costs za kujenga barabara hizo na pia kuvunja mikataba na kutafuta contractors wapi.

WAchina wamekuwa wakipewa barabara kutokana na Bei zao kuwa Za chini na ambazo tunaweza kuhimili,ila sio barabara zote zilijengwa na wachina,kuna kampuni nyingi tu zimepewa barabara ambazo si za kichina na zimefanikisha suala hilo.
 
Heri, karibu Jamvini Mkuu..... Mkuu hapo kidogo nadhani tunakosea kulaumu JPM ku initiate ujenzi wa barabara sababu eti makandarasi tuliowapata ni Chinese.... Mkuu, mtake radhi mzee wa watu... Kumbuka yeye sio technical person, alichofanya ni kuondoa ukiritimba na kuweka mambo powa na kuweka maamuzi ikiwemo kupitisha ushauri wa "technical personnel" pale wizarani.... Nani alipata kazi zile sio kosa lake wala halimhusu JPM hapo muulize Katibu Mkuu na wahandisi wake kwa kile walichokiona kwa hawa waChina na kuwapa contract na kutulipa madudu.....

Jiulize:
1. Ina maana wahandisi ujenzi hawakujua waChina ni mabomu? (hapana angalia SIETCO na ile barabara ya Mwanza)
2. Nani alifanya technical evaluation? (kumbuka unafungua financial proposal "mambo ya bei" baada ya kumpitisha kandarasi kuwa anajua kazi)
3. usimamizi wa kazi ulikuwa bora? (kuna consultants, na pia kuna MoW counterpart engineers kweny kila mradi)

sasa ukishajiuliza hayo hapo nieambie JPM angewezaje kuingilia wakati hayo ni all technical??

Mkuu, JF tunajitahidi (to the largest extent) kuangalia pande zote za shilingi........

Naomba kuwakilisha!!
 
WAchina wamekuwa wakipewa barabara kutokana na Bei zao kuwa Za chini na ambazo tunaweza kuhimili,ila sio barabara zote zilijengwa na wachina,kuna kampuni nyingi tu zimepewa barabara ambazo si za kichina na zimefanikisha suala hilo.

Makampuni ya Tanzania yako wapi kwenye huo ujenzi wa barabara? Sitashangaa miaka 100 kuanzia sasa bado tutakuwa tunatumia wageni kutujengea barabara.

Kinachotakiwa sasa ni ubia kati ya makampuni yetu na hayo ya kigeni. Kuwe na transition period, ambapo lengo litakuwa ni technology transfer. Watu wetu wanafanya kazi kwenye level zote kuanzia za chini mpaka juu ili baada ya muda waweze kuendesha hiyo miradi wenyewe.

Haya ya Wachina mara Wajapani, kama hakuna technology transfer basi tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu.

Serikali inatakiwa kutengeneza strategy au vision ya nchi kwenye mambo ya ujenzi ili miaka 10 ijayo, tuwe na makampuni makubwa ya Watanzania ambayo yana sifa na uwezo wa kujenga barabara zetu kwa gharama nafuu lakini with high quality.

Inasikitisha sana unapoona miaka na miaka tunafanya kazi na wageni lakini hakuna technology transfer. Kazi za Watanzania ni zege na kuwa foremen. Kwa mtindo huu hatuna chetu. Sisi tutaendelea kuwa makuli kwenye nchi yetu.

Tunataka waziri mpya ambaye atakuwa na vision mpya na kuipa technology transfer kipaumbele.
 
Kwa walioko TZ

Hivi yule dada wa UDSM sheria, mwenye RAV4 aliekuwa anakaa MABIBO hostel ameshaolewa na MAGUFULI ? , kwa maana alikwa anajishau kuwa anazimaliza pesa za BARABARA zetu kipindi kile Mh. yuko Miundombinu.
 
Ant RU,mambo yanayohusu maisha ya Viongozi ambayo ni binafsi ,tusiyaguse,kila mtu ana mapungufu yake na ana uwezo wa kumuoa mtu yeyote na kuwa na mahusiano na mtu yeyote.
 
Ant RU,mambo yanayohusu maisha ya Viongozi ambayo ni binafsi ,tusiyaguse,kila mtu ana mapungufu yake na ana uwezo wa kumuoa mtu yeyote na kuwa na mahusiano na mtu yeyote.

Mkuu Gembe,

Ufisadi wowote unaanzia kwenye mambo binafsi. Ni ngumu kutenganisha masuala ya wanasiasa na mambo binafsi.

zaidi ya asilimia 50 ya wanasiasa waliondolewa madarakani kwa kashfa, matatizo yao yanatokana na mambo binafsi.

Ukiingia kwenye siasa ni kwamba unaruhusu mambo yako binafsi kuanikwa.

Nafikiri unaelewa uhusiano wa money, power and sex. Hivyo vitu vitatu huwezi kuvitenganisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom