GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,736
- 109,328
Mwekezaji wa Simba SC Mo Dewji usichokijua pamoja na utajiri wako ni kuwa 90% ya Wajumbe wa Bodi ya Simba SC ni wapigaji watupu na wengi wao ni wasaliti kutokana na kutumika kwao kutoka upande wa pili.
Mo Dewji baada ya wewe kumsifia mno vile Kocha Mgunda na kuahidi kuwa ungekutana naye Ili mzungumze na ikiwezekana umpe yimu (Simba SC) moja kwa moja, hapa ndipo uliharibu.
Mo Dewji watu wanaokuzunguka ndani ya Simba SC hawataki Mgunda apewe timu moja kwa moja kama unavyotaka kwani wanajua Mgunda akiwa Kocha Mkuu wao hawatapata ile 10% yao na isitoshe Kocha Mgunda ni mzawa na mjanja (mtoto wa mjini) hivyo wanajua kuwa atawakatalia tu.
Hivyo basi Mo Dewji tambua ya kuwa hata matokeo ya jana (Simba SC kufungwa na Azam FC) ni sehemu ya mkakati wa kimafia na kihujuma kutoka kwa hao wana Simba SC (Wazee wa 10%) ili Kumharibia Kocha Mgunda na uondoe imani naye.
Na mchakato wa kumpata na kumleta Kocha Mkuu wa kigeni ufanyike na kama kawaida yao akija wao wapate (wale hiyo 10% yao), ambayo ndiyo inawaweka mjini pamoja na zile 10% wanazozipata kutoka kwa wachezaji mizigo wa kigeni na hata wa kizawa.
Mo Dewji kama kawaida yangu GENTAMYCINE bingwa wa kupata taarifa ngumu na za ndani kabisa ambazo kwa 99.9% huwa ni sahihi (kweli) ni kwamba, hata katika mechi ya Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar FC kama hakutokuwa na umakini mkubwa na kukabiliana na hawa mafia na wasaliti kuna uwezekano mkubwa Simba SC ikafungwa tena au kutoka sare/Suluhu Ili tu kuendelea kumharibia Kocha mzawa Mgunda kisha aje Kocha wa kigeni (hasa Mzungu) na ule utamaduni wao wa kula 10% uendelee na maisha yao yaendelee.
Kazi kwako tu sasa kuyafanyia kazi!