Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Hahaaaaaaa,Mwanakijiji..Umenikumbusha mbali sana ndugu yangu,umenikumbusha vipindi vya Jambo na Mchana Mwema(Pokea Salamu) pale Radio Tanzania bila kusahau kipindi cha usiku cha Kijaruba cha Abdallah Mlawa,hivi vilikuwa ni vipindi maarufu sana vya salamu...Ilikuwa ukisikiliza vipindi hivi ni lazima utakutana na majina haya

1.Issa Hasssan Madjeshi

2.Chidi Chidi Chitenda

3.Chivalavala wa Chivalavala

4.Limonga Justin Limonga

5.Duwa Wajadi

6.Wajadi Fundi

7.Mohammed Kassim Saibaba

8.Jai Sikinde

9.Maalim Shabani Uledi

10.Boko Man Mwana wa Mkongoman

Umemsahau Muungwana Zomboko alikuwa maarufu sana enzi zile
 
mkuu umenikumbusha mbali sana nikiona hayo majina ya akina wajadi fundi wajadi,chivalaval nk bt wakuu kuna huyu pia naona kasahaulika Makumbuli Ismail Makumbuli wa Ligula Hospital Mtwara
 
husein makabureta!!!
Huyu wa juzi juzi huyu.

Unamkumbuka CHIVALAVALA S. CHIVALAVALA? enzi za salaaam mkulima, na vipindi vinginevyo vya salaam alikuwa anasikika na kuvuma. angekuwa leo hii bado yupo basi jamaa zangu (CCM) wanaopenda watu maarufu wanaokubalika basi wangemuaprochi agombee ubunge....
 
Kati ya hawa wote ni yupi tumtunze.. ningependa tumpate mmoja au wawili wao.. tuweze kuzungumza nao "live"..
 
Ila wewe Mzee Mwanakijiji ni kiboko, unajua unaweza kuwanyambulisha wote waliochangia hii thread na kuweza kujua ni watu wa umri gani ukijumlisha na kutoa 2 to 4 years difference!.
 
Hahaaaaaaa,Mwanakijiji..Umenikumbusha mbali sana ndugu yangu,umenikumbusha vipindi vya Jambo na Mchana Mwema(Pokea Salamu) pale Radio Tanzania bila kusahau kipindi cha usiku cha Kijaruba cha Abdallah Mlawa,hivi vilikuwa ni vipindi maarufu sana vya salamu...Ilikuwa ukisikiliza vipindi hivi ni lazima utakutana na majina haya

1.Issa Hasssan Madjeshi

2.Chidi Chidi Chitenda

3.Chivalavala wa Chivalavala

4.Limonga Justin Limonga

5.Duwa Wajadi

6.Wajadi Fundi

7.Mohammed Kassim Saibaba

8.Jai Sikinde

9.Maalim Shabani Uledi

10.Boko Man Mwana wa Mkongoman
Umemsahau Alfonse Maji ya Pwani.
 
Zacharia Ndemfoo wa Babati, Issa Hassan Majeshi wa Ukonga, Abdallah Mpanjinji wa Kilongwe -Mafia
 
Bwana huwezi kuongelea watuma salaam bila kumweka Zackaria Ndemfoo yeye kila mara 'safarini kuelekea ...' huyu jamaa alivuma sana 70's na 80's cha kushangaza juzi juzi kama bahati nikasikia jina lake akitumiwa salaam.
 
Jamani, mbona sijasikia mkimtaja:

1) Zeyana Seif wa Zanzibar (Marehem)

2) Bambe Hussein Bambe (Bingwa wa Mabingwa)
 
Kati ya hawa wote ni yupi tumtunze.. ningependa tumpate mmoja au wawili wao.. tuweze kuzungumza nao "live"..

si vibaya wakachaguliwa wanne na mmoja wao atayeibuka kindakindaki kwa mapendekezo ya wengi ndo afanyiwe mazungumzo ya moja kwa moja.
wafuatao ndo nawapendekeza.....
bokoman mwana wa mkongoman
limonga justine limonga
wajadi fundi wajadi
chivalavala wa chivalavala!
 
Na zile salaam club nilikuwa nikizisikia sana lakini sijawahi kuona hata bango moja linaloonesha hapa ndio salaam club, jee zilikuwepo kweli au kimaneno tu?
 
Nakumbuka wale watuma salamu wa nyanda za juu kusini, maneno kamaa yeeh baba, eeh baba, eeh mama yalikuwa hayakoseni. Kwakweli ilikuwa burudani. Ndio facebook za kipindi icho lakini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom