Mnaotamani Mbowe aachie uenyekiti, mnaweza kuja kumkumbuka ikitokea anarithiwa na kiongozi mwingine ambae hatokubali kuvumilia uonevu huu unaondelea

We jamaa hujielewi
Chama cha democrasia halafu hamtaki kuachie wengine.
Mkiambiwa ni chama cha undugu mtakataa. Wachaga bwana.
Baadhi ya watu wa chama cha kijani wanatumia nguvu kubwa na muda wao mwingi kufanya kila waliwezalo kuhakikisha Mbowe harudi madarakani iwapo ataamua kugombea tena uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Binafsi watu hawa nawasikitikia sana kwani huenda hawajui walitendalo mithili ya wale Wyahudi waliomsulubisha Yesu msalabani ambao nao walikuwa hawajui walitendalo.

Na vita hii dhidi ya Mbowe bila shaka ina baraka za watu wakubwa tu walioko katika chama cha hawa wenzetu na pengine wana lengo la kutaka kutumia uchaguzi huo kuweka pandikizi lao katika nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kwa masilahi yao ya kisiasa kama wanavyotuhuimiwa kuweka mapandikizi katika baadhi ya taasisi au vyama na kuzifanya taasisi au vyama hivyo kuwa ni taasisi butu/mfu.

Mimi nawashauri watu hawa wajue tu kuwa ikitokea Mbowe harudi madarakani kwa yeye mwenyewe kutogombea au vinginevyo, huku jitihada za kuweka mwenyekiti pandikizi zikifeli na badala yake CHADEMA wakafanikiwa kupata mwenyekiti mpya atakaekuja na misimamo na mitazamo tofauti katika kuiongoza CHADEMA ikiwamo kukataa kuvumilia uonevu huu unaoendelea dhidi ya wana-CHADEMA na upinzani kwa ujumla,basi watu wa chama cha kijani wajue tu wanaweza kuja kukumbuka sana Mbowe na wanaweza kuja kujuta na kusema bora Mbowe angebaki tu kuiongoza CHADEMA.

Busara na uvumilivu wa Mbowe, hamtaweza kuviona sasa mpaka pale mtu mwingine atakapochukua nafasi yake ingawa teyari Spika hivi karibuni alikiri kuwa Mbowe ni mtaratibu akimlinganisha na Lissu aliemuoma ni mtu mkorofi/mwenye kiburi.

Turejee maneno ya wahenga: "mtoto akililia wembe,mpe".
 
Je Magufuli akitaka kuongeza muda kwa kubadili katiba mtakataa wakati Mbowe alibadili katiba ili asizuiwe.
Acheni kudanganya watu Wakati ninyi hamna demo crasia.
Siwezi kukupinga unayoyasema,ila nawakumbusha watu wa chama cha kijanii kuwa uvumilivu huu unaoendelea kwa sehemu kubwa ni matokeo ya Mbowe kama mwenyekiti kutotaka kuongoza kwa style ya kulipa visasi ila wajue tu akipatikana kiongozi mwingine atakaekuja na mbinu tofauti za kujibu mapigo na kutafatu haki zinazominywa,basi ni hawa hawa ambao leo hii wanataka Mbowe aondoke ndio watakuwa wa kwanza kusema CHADEMA imepata kiongozi anaetaka kuvuruga amani ya nchi na ni afadhali Mbowe.

CHADEMA ikipata mwenyekiti wa tofauti na kwa haya yanayoendelea,basi yale ya Aquilina yanaweza kuja kuwa ni ya kila siku kama sio ya kila wakati.

Time will tell.
 
Hata Magufuli ni rRaisi mzuri nashauri katiba ibadilishwe kama ilivyofanyika ya chadema ili asije Rais mbaya.
Njia mbadala zinafahamika ila siku akiingia kiongozi mwingine wa CHADEMA na atakaeamua liwalo na liwe,basi hizo mbinu zitakuwa wazi hata kwa vipofu na viziwi.
 
Unauhakika kuwa Mbowe sio pandikizi?
Badilika ndg. Achana na uchaga utawaua
Mapandikizi wanatengenezwa na hawana tofauti na wale walioasi upinzani kwa kisingizio eti cha kuunga mkono juhudi hivyo kila kitu kinawezekana as long as mna pesa za kununua watu au kuwapa vyeo na madaraka.
 
Kamanda akubali tu kuwaachia wengine nao waendeleze pale alipoishia. Hakuna asiyetambua mchango wake ndani ya chama hasa enzi za JK akishirikiana na makamanda wenzake. Ila kwa sasa mabadiliko ndani ya chama, hayakwepeki.

Anaweza akabakia tu kuwa mlezi/mzee wa chama. Nb:Mh.Sumaye naye hana sifa ya kumrithi ingawa amejipambanua kupigania demokrasia nchini.
 
Wachaga huwa hamuamini makabila mengine ndio maana mnaona Mchaga mwenzenu ndio sahihi.
Maduka yote ya wachaga wanaajiri wachaga wenzenu kisa tu makiasaka hamuwaamini.
Loooo
Watakupinga, lakini ndio ukweli. Sasa hivi matukio ya uvunjifu wa amani mitaani no ajabu kuwa yanaratibiwa na chama tawala tofauti na ilivyo zoeleka nchi nyingi kuwa chama kikuu cha upinzani ndio huratibu matukio machafu kupinga utawala.
Kwa nini? Ni kwa sababu kiongozi mkuu wa upinzani kajawa hekima, moyo usio wa kisasi na kukulia mazingira ya kistaarabu yenye kujali utu wa mtu.
Sasa Mbowe atoke kisha uenyekiti apewe kamanda Heche kwa mfano, sio kuwa Heche sio mstaarabu bali asili ya kwao neno kuvumilia ujinga halipo mnategemea nini?
Kama kwenye mkutano wa hadhara anapandishiana na rais Magufuli hadi ananyang'anywa mic unadhani wa mchezo huyo akiwa ofisini peke yake? CCM mnalitafuta jini lililo kwenye chupa kwa kusuka mipango ya kumtoa Mbowe.
Sio kwamba mbinu zenu zitafanikiwa, lahasha Bali Mbowe kama binadamu na mwenye familia yake anaweza kuchoka akajisemea bora nika jipumzikie.
 
Hata Magufuli ni mzuri kama vipi aongezewe muda WA miaka 10 zaidi.
Acheni ubinafsi nyie wapinza I hamtafika popote
Hawa jamaa wana vichwa vibovu/vizito na zaidi huwa hawaoni mbali until it is too late!!

Dunia itawafunza na watajua kuwa upole na uvumilivu wa Mbowe ndio ulikuwa msingi wa amani na utulivu tulionao leo hii kisiasa.
 
Chadema kilikua kwa sababu ya udhaifu wa Raisi alietoka kutokana na ufisadi Tu.
Kwa sasa huyu aliepo ni kazi tu na wananchi sio wajinga wanaona ujue.
Mbowe kafanya makubwa sana. Anastahili heshima na pongezi kwa aliyoyafanya.

Lakini wana- CHADEMA mnatakiwa kutambua kuwa binadamu anaweza kufaa sana kwa mazingira fulani kwa kazi fulani kwa wakati fulani lakini siyo lazima afae wakati wote kwa mazingira yote. Na siyo sahihi kwa sababu kiongozi alifanya vizuri sana wakati fulani aendelee wakati wote hata kwenye mazingira na nyakati asizozimudu kama shukrani kwa mazuri aliyoyafanya.

Ni kama CCM, ilitufaa wakati fulani kwa kazi fulani za wakati huo lakini kwa mazingira ya sasa haitufai tena. Ndiyo maana unakuta watu kama akina Kabudi, hata wakipewa nafasi ya kuongea, wanakazania kuongelea historia tu. Ni kwa sababu walionekana ni wasomi wazuri nyakati hizo lakini kwa nyakati hizi, wakiongea wanaonekana ni watu wasiojua kitu na waliopitwa na Ulimwengu uliopo.

Kwa mazingira ya sasa na kwa wakati huu, kwa kuyatazama mazingira ya siasa ya sasa, na hali ya CCM kwa sasa na uongozi wa CCM na serikali uliopo sasa, tunahitaji sana mbinu mpya, mtazamo mpya, fikra mpya na pengine viongozi wapya wenye ujasiri mpya.

CCM haitufai tena kwa mazingira ya sasa lakini kuiondoa kunahitajika mipangilio mipya kabisa. Siyo ile ya kale.
 
Wachaga huwa hamuamini makabila mengine ndio maana mnaona Mchaga mwenzenu ndio sahihi.
Maduka yote ya wachaga wanaajiri wachaga wenzenu kisa tu makiasaka hamuwaamini.
Loooo
Unanipaje kabila sio langu? Kwa hiyo hata wewe ukidhaniwa ni mhutu ni sawa?
 
Ficha upumbavu wako, onyesha hekima! That's all you should be told.
Sasa kama ccm wanatuchoma madole washindani wao, busara na hekima za mbowe zinatuelekeza tuwageuzie na tako la kushoto wachome vizuri mana yake hatuna cha kuwafanya na mbowe akiendelea kuwepo na uwepo wa ccm utaendelea kudumu.
 
Kiukweli kwa hali iliyopo chadema mwenyekiti either lisu , au heche ndo wanafaa, ningesema lema ila lema hapana lumumba watakimbiana, halafu katibu mkuu mnyika aisee
 
Upuuzi mtupu ulioongelewa humu
Baadhi ya watu wa chama cha kijani wanatumia nguvu kubwa na muda wao mwingi kufanya kila waliwezalo kuhakikisha Mbowe harudi madarakani iwapo ataamua kugombea tena uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Binafsi watu hawa nawasikitikia sana kwani huenda hawajui walitendalo mithili ya wale Wyahudi waliomsulubisha Yesu msalabani ambao nao walikuwa hawajui walitendalo.

Na vita hii dhidi ya Mbowe bila shaka ina baraka za watu wakubwa tu walioko katika chama cha hawa wenzetu na pengine wana lengo la kutaka kutumia uchaguzi huo kuweka pandikizi lao katika nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kwa masilahi yao ya kisiasa kama wanavyotuhuimiwa kuweka mapandikizi katika baadhi ya taasisi au vyama na kuzifanya taasisi au vyama hivyo kuwa ni taasisi butu/mfu.

Mimi nawashauri watu hawa wajue tu kuwa ikitokea Mbowe harudi madarakani kwa yeye mwenyewe kutogombea au vinginevyo, huku jitihada za kuweka mwenyekiti pandikizi zikifeli na badala yake CHADEMA wakafanikiwa kupata mwenyekiti mpya atakaekuja na misimamo na mitazamo tofauti katika kuiongoza CHADEMA ikiwamo kukataa kuvumilia uonevu huu unaoendelea dhidi ya wana-CHADEMA na upinzani kwa ujumla,basi watu wa chama cha kijani wajue tu wanaweza kuja kukumbuka sana Mbowe na wanaweza kuja kujuta na kusema bora Mbowe angebaki tu kuiongoza CHADEMA.

Busara na uvumilivu wa Mbowe, hamtaweza kuviona sasa mpaka pale mtu mwingine atakapochukua nafasi yake ingawa teyari Spika hivi karibuni alikiri kuwa Mbowe ni mtaratibu akimlinganisha na Lissu aliemuoma ni mtu mkorofi/mwenye kiburi.

Turejee maneno ya wahenga: "mtoto akililia wembe,mpe".
 
Rudi shule uongeze uelewa hata zile za ngumbaru
Kwa maana nyingine tofauti na Mbowe wengine wote wana elements za kuwa mapandikizi?

Kumbe hata hamuaminiani!

Mbowe hana busara na uvumilivu wowote sema kadhibitiwa tu,hata Slaa na Mamvi mlikuwa mnajifaragua hivihivi.

Hata Mangestu Haile Mariam alikuwa anapiga propaganda hizihizi kwamba bila yeye hakuna Ethiopia alipokuja Zenawi Ethiopia ikastawi kuliko wakati wote.

Hizo ni porojo tu za kuhalalisha kung'ang'ania madaraka na madikteta wote hufanya hivyo.

Hakuna jipya hapo.
 
Mbowe akiachia ngazi, chadema itakufa haraka sana, akiendelea na uongozi chadema itakufa taratibu, tunavhtaji wapinzani halisi sa hv waigizaji tumewachoka
In fact amefanya kazi nzuri sana kwa wakati wake. Cha muhimu sasa na yeye apumzike
 
Baadhi ya watu wa chama cha kijani wanatumia nguvu kubwa na muda wao mwingi kufanya kila waliwezalo kuhakikisha Mbowe harudi madarakani iwapo ataamua kugombea tena uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Binafsi watu hawa nawasikitikia sana kwani huenda hawajui walitendalo mithili ya wale Wyahudi waliomsulubisha Yesu msalabani ambao nao walikuwa hawajui walitendalo.

Na vita hii dhidi ya Mbowe bila shaka ina baraka za watu wakubwa tu walioko katika chama cha hawa wenzetu na pengine wana lengo la kutaka kutumia uchaguzi huo kuweka pandikizi lao katika nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kwa masilahi yao ya kisiasa kama wanavyotuhuimiwa kuweka mapandikizi katika baadhi ya taasisi au vyama na kuzifanya taasisi au vyama hivyo kuwa ni taasisi butu/mfu.

Mimi nawashauri watu hawa wajue tu kuwa ikitokea Mbowe harudi madarakani kwa yeye mwenyewe kutogombea au vinginevyo, huku jitihada za kuweka mwenyekiti pandikizi zikifeli na badala yake CHADEMA wakafanikiwa kupata mwenyekiti mpya atakaekuja na misimamo na mitazamo tofauti katika kuiongoza CHADEMA ikiwamo kukataa kuvumilia uonevu huu unaoendelea dhidi ya wana-CHADEMA na upinzani kwa ujumla,basi watu wa chama cha kijani wajue tu wanaweza kuja kukumbuka sana Mbowe na wanaweza kuja kujuta na kusema bora Mbowe angebaki tu kuiongoza CHADEMA.

Busara na uvumilivu wa Mbowe, hamtaweza kuviona sasa mpaka pale mtu mwingine atakapochukua nafasi yake ingawa teyari Spika hivi karibuni alikiri kuwa Mbowe ni mtaratibu akimlinganisha na Lissu aliemuoma ni mtu mkorofi/mwenye kiburi.

Turejee maneno ya wahenga: "mtoto akililia wembe,mpe".
Ndicho wanachokitafuta ili wahalalishe mauaji na mateso kwa wapinzani
 
Pandikizi Ni Sumaye

Ila Mbowe Apumzike Inatosha.

Umbogo Wa Mbowe Ndio Umetufikisha Apa Tulipo.

Kuna Watu Makini Ndani Ya Chadema Tundu Lissu, John Heche Na Wengine Wasio Na Makando Kando Ya Tuhuma !

Magufuli Anahitaji Mtu Aina Ya Lissu.
Nje ya mada: Hivi kwanini huwa unakuwa unapotea sana mara kwa mara. Hivi unajua napenda sana comments zako! Usiwe unapotea sana mkuu, na miss madini yako
 
Back
Top Bottom