Ushauri: Mama mdogo anamsema vibaya mchumba wangu kumbe anajihusisha naye kimapenzi!

Nothing4good

Senior Member
Feb 19, 2011
180
55
Wandugu naomba msaada. Mimi nina mchumba wangu tuko katika mchakato wa harusi. Alishanitambulisha kwao na nikakubalika.

Mimi ninaishi na mamdogo. Mamdogo ndiye aliyenilea so ni kama mamangu kwahiyo nilimpeleka mchumba wangu kwanza kwa mamdogo kumtambulisha kabila ya hatua nyingine na mamdogo ndiye aliyewaambia ndugu zangu wengine na akasema kuwa atagharamia kichen party na send off kwa kuwa mimi ni kama mtoto wake.

Ndugu zangu karibu wote wanamjua huyo kijana, sasa cha ajabu mamdogo ameanza kunikatisha tamaa. Ananiambia mbona huyo mwenzako anaoneka hajatulia? Ni mzuri tu wa sura hana kingine hakufai mwanangu. Tafuta mwingine mbona wanaume wako wengi? Na maneno mengine mengine kibao.

Mimi nikamjibu nampenda hivyo hivyo alivyo mamdogo. Baada ya kuona sielekei kumwacha akaanza kumwaga upupu kwa ndugu zangu wote kwamba yule kaka hanifai. Ndugu zangu wakaanza kumchukia huyu kijana. Cha kushangaza naona mamdogo yuko karibu sana na mchumba wangu nikimuuliza anasema wanashughulikia mambo ya ndoa yetu.

Siku moja mawifi zangu (ukweni) wakaniita na kuniuliza hivi huyo ni mamdogo wako kabisa? Nikawajibu ndio; yeye na mamangu ni wa tumbo moja. Walishangaa na kusema mbona sasa anafanya mambo ya ajabu vile? Nikawauliza mambo gani hayo wakasema nisubiri niolewe kwanza ndo wataniambia sababu wanaogopa kuuvunja uhusiano wetu(mimi na kaka yao).

Katika chunguza yangu nimegundua mamdogo ananichukulia mchumba wangu. Nimuachie mchumba wangu au nifanyeje??
 
heee,pole mamii,kitendo anachokifanya mamaako mdogo ni kichafu,na huyo mchumba ako hajatulia,na hana aibu,juu ya yote,uamuzi ni wako,maana ndoa ni safari ndefu,ukiwa nae huyo mtu ujue pressure zitakuwa juu juu,maana hatotulia,ata hangaika tu.pengine ni heri yako,mungu amekuonyesha mapeema huyo mchumba ni wa aina gani.jee umemwambia maako mdogo?na yeye anasemaje?.w.me sijui wakoje jamani,wewe ndio wenye uamuzi wa mwisho.muulize mchumba kulikoni na kwa nini anafanya hivyo?inavyoonyesha hakupendi,asingekufanyia hivyo.
 
Mweleze mamdogo ucimfiche anachofanya c kizuri kabsaa!

Na huyo mchumba mueleze ajue kosa lake then chukua hatua
 
kweli huyo jamaa hajatulia kama alivyokwambia mamako mdogo. nimeipenda hiyo,kaanza na yai kamalizia na kuku. kweli vice versa is true.
 
Huyo Mchumba wako namlaumu sana. Kama mamamdogo kamshawishi angekwambia kama kweli anakupenda lakini naona huyo mchumba wako nae hajatulia piga chini wote. Utapata mwanaume wa kukufaa huyo hafai kabisa hata kidogo anatembea na mama yako??? Maana mamamdogo ni mamayako tu.

Natamani nimtukane vilee .***** zake kabisa hana adabu
 
faster sana achana nae huwezi kushare penzi na mama yako mdogo kwani ni kama mama yako mzazi kabisa so plz achana nae:hand:
 
Hivi ni wewe au nimesahau kuwa wiki iliyopita ulikuwa hapa unatafuta mpenzi wa muda( wa mkataba)? leo huyu unaye miaka miwili?

ulikuwa unatafuta mwingine wa nini?
 
Hivi ni wewe au nimesahau kuwa wiki iliyopita ulikuwa hapa unatafuta mpenzi wa muda( wa mkataba)? leo huyu unaye miaka miwili?

ulikuwa unatafuta mwingine wa nini?

Michelle hizi huwa tunazipotezea tu kama hatujaziona vileee
 
Du kizunguzungu kumbe wiki iliyopita ulikuwa unatafuta mchumba sasa unataka kuolewa na mchumba uliyekuwa nae miaka 2 iliyopita fafanua tukusaidie usilete jokes
 
Huyo Mchumba wako namlaumu sana. Kama mamamdogo kamshawishi angekwambia kama kweli anakupenda lakini naona huyo mchumba wako nae hajatulia piga chini wote. Utapata mwanaume wa kukufaa huyo hafai kabisa hata kidogo anatembea na mama yako??? Maana mamamdogo ni mamayako tu.

Natamani nimtukane vilee .***** zake kabisa hana adabu

DA nimeshindwa kusoma hii kiarabu au !
 
Hivi ni wewe au nimesahau kuwa wiki iliyopita ulikuwa hapa unatafuta mpenzi wa muda( wa mkataba)? leo huyu unaye miaka miwili?

ulikuwa unatafuta mwingine wa nini?
I wonder some people like to degrade their credibility
 
Hii ni mbaya lakini Dena wangu,kuna watu watakosa ushauri kumbe wanauhitaji kweli.....!!! am out....!!

Hiyo ni kweli lakini huyu alitakiwa afanyiwe kama not enough thread zake zote zilichanwa live mpaka kakimbia jamvi
 
Back
Top Bottom