Mmiliki wa Interchick

C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,070
3,718
Kwa muda mrefu nilikuwa naiona hii kampuni ya interchick inakua mpaka kufikia leo hii... Sasa hapa jamvini watu wengi wana plans za kufuga kuku na mayai na vifaranga
Hapa mjini wa akina mama wengi wanafanya biashara ya kuku wa nyama na mayai ila ukiangalia kwa undani biashara hii imekuwa kama second option yaani katika familia mke wa nyumbani ndio anasaidia kuingiza kipato cha nyumbani as second option ila first option ni shuguli anazofanya mzee (sijui mmenielewa hapa)
Ila kwanini kuku isiwe the first business kwanini kuku isiwe biashara ya kwanza ambayo mtu anaingiza na ikamfanya awe bilionaire??
Mfano interchick.
Je kuna mtu yeyote anajua jinsi jamaa mwenye interchick alivyoanza??
Jinsi alivyoendesha biashara yake
Na mmiliki wake profile kiujumla
Natanguliza shukrani
 
Nimependa mtazamao wako, hasa uliposema, kwa nini kufuga kuku kusiwe option A na sio option B. Nchi yetu ipo ktk mpito wa kuachana na mfumo wa kale wa uchumi na maisha ya familia.

Siku chache zilizopita, plastic za maji ya kunywa zilikuwa kero, leo ni kazi za watu rasmi za kuokota na kuuza na wengine kufanya recircling. Hata hili la kuku limeanza tayari, mifano ya waliofanikiwa ipo mingi,labda nikupe mmoja ulio nivutia zaidi kuliko huo.

Vijana wa zamani wanamfahamu AMADORI, akiuza kuku wa kufa mtu pale Kariakoo, alikuwa na shamba pale Mwandege ambapo baadae ndipo kilipo kiwanda cha AZAM COLA baada ya kuuza eneo lile. Jamaa kahamia huko ndani sana na kupata eneo la kutosha kabisa na anaendeleza kuku.

Ninajua wengi wetu tunaona aibu kuwaambia jamaa zetu kuwa tuko mjini tunafuga kuku, yaani mtu na degree yako ufuge kuku? Bora niwe misheni town.
 
Hao jamaa wa interchick wako kwenye next level, infact issue yao kubwa sio mayai, deal ya mayai is less than 10% of what they do. Wanadeal na kuku wa nyama ambao huwa-pack vizuri na kuuza kwenye big bness na zaid export. Ila in a very high quality. So wana tengeneza vifaranga wenyewe kwa ajili ya partners wao na pindi hao partners wanawakuza huwauzia hao kuku baadae kwa ajili ya kuwa sliced and packed. Nadhani wanamiliki waitaliano. Its other sister company iko kenya na ni kampuni kubwa sana.
 
Interchik wamejipanga sana wale wakenya, sio wa kujifananisha nao...ila pia ni changamoto kwetu watz kujipianga kufikia level zao kama wao wameweza na sisi pia tunaweza, cha msingi ni kuwa na malengo
 
Kwakweli Interchick namkubali na nimemuweka kama role model kwangu, lakini licha ya kuwa ameifanya hii ni main source of income ninafikiri pia ni aidha a family or company with more than one shareholders.
Yuko juu kwasababu anafata quality kuanzia vifaranga wao ni bora, chakula ameanza kutengeneza mwenyewe muda, sanitation ni safi, anafugia jirani na makazi ya watu lakini mazingira yake bila kuuliza huwezi kujua kuwa anafuga kuku wengi. Tofauti na wengine ni kawaida kukuta katupa mizoga ya kuku na harufu kusumbua watu jirani, pia kuuza vifaranga bila kuwapa chanjo kama Mareks hivyo kuwasababishia hasara wafugaji wanaonunua.
Nadhani tuna kitu kikubwa cha kujifunza kwa hawa wenzetu
 
Kila kitu kinategemea unakichukulia kwa mtazamo gani siku zote ukiwa na mtazamo chanya utaona kila business ni business kubwa sana kuanzia kulima hadi kufuga kosa kubwa tunalofanya kizazi cha leo ni kuendeleza mtazamo wa wazee wetu/kizazi kilichopita kwa mfano kuku wa kienyeji wamekuwa wakichukuliwa kama ni kuku wa kufuga kwa ajili ya kula tu lakini ukifikiria kuwa na kuku zaidi ya 2000 wanathamani ya karibu 30M your life will be different.Nafurahia kuona mtizamo kama wakina CTU
 
Watanzania sisi wa ngozi nyeusi inakuwa ngumu kufikia level hizo kwakuwa haya mambo ni magumu kufanya mtu peke yako kama individual hadi muunganishe nguvu muwe 2 ,3 ,5,10 nk . Sasa sisi tukishakuwa watu wengi lazima kutatokea kutokuelewana ndio maana kila mtu anafanya kidogo kidogo. Juzi niliangalia Habari TBC nikaona jamaa wameunganisha nguvu huko Bukoba wanafanya ufugaji mkubwa wa ng'ombe mafanikio waliyopata kwa kweli its amazing!!!
 
Mtindo wa kuunganisha nguvu ndio njia mbadala kwa wenye mitaji kidogo,la msingi ni kupata timu nzuri.
 
Duuh mimi huwa naagiza tu Vifaranga wa mayai naona box zimeandikwa interchick kwa kuwa kuku wananipa mazao bomba huwa siwafutilii kumbe ni bonge la kampuni ngoja nianze kuwafutilia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom