Mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari waua watu watatu na kujeruhi wengine sita Mogadishu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
1578480271749.png

Bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari limelipuka katika eneo la makutano lenye shughuli nyingi mji mkuu wa Somalia na kusababisha vifo kwa watu 3 huku wengine 6 wakijeruhiwa kulingana na mkuu wa huduma ya uokoaji ya Mogadishu.

Gari lilikokuwa na vilipuzi lililipuka katika kituo cha ukaguzi eneo la Sayidka, Mogadishu eneo lililo karibu na majengo ya bunge.

Magari ya kubebea wagonjwa na zima moto walielekea katika eneo la tukio ambalo pia limezingirwa na vikosi vya serikali. Hali hiyo inatia wasiwasi na huduma za uokoaji zinaendelea.

Msemaji wa utawala Salah Hassan Omar - Banadir amesema, "Leo, karibu saa tatu asubuhi, katika kituo hiki cha ukaguzi ambacho ni lango la kuingia makazi ya rais yanayolindwa, limevamiwa na gari lililokuwa limejazwa vilipuzi.

Ulikuwa ni wakati ambao watu ni wengi kila mmoja akiharakisha kuelekea kazini. Watu watatu wameuawa na wengine 6 wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini. Tunatarajia kwamba katika kipindi cha saa moja ijayo, hali itakuwa imerejea kama kawaida".

Hata hivyo, hadi kufikia sasa hakuna aliyedai kutekeleza shambulio hilo ambalo lilitokea karibu na majengo ya ofisi za serikali.

Shambulio sawa na hilo

Siku kumi zilizopita shambulio kama hilo la bomu lililotegwa kwenye gari lilitokea katika eneo la makutano na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 90 huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa.

Mlipuko huo ulitokea katika kituo kimoja cha kukagua magari katika eneo la makutano ya barabara mjini Mogadishu.

''Mlipuko huo ulikuwa mbaya mno na naweza kuthibitisha kwamba zaidi ya raia 20 waliuawa , huku wengine wengi wakijeruhiwa'', afisa wa polisi Ibrahim Mohamed alinukuliwa na kituo cha habari cha AFP akisema.

Wengi kati ya waliouawa katika shambulio hilo lililotokea mwishoni mwa mwaka jana, wanadaiwa kuwa wanafunzi wa chuo kikuu waliokuwa wakipita katika eneo hilo wakati wanasubiri basi lao.

Vilevile hakuna aliyekiri kutekeleza shambulio hilo lakini kundi la Al-Shabab, linaloshirikiana na kundi la kigaidi la Al-Qaeda limekuwa likitekeleza mashambulizi kwa zaidi ya miaka 10. Kundi hilo lilifurushwa kutoka mji mkuu wa Mogadishu 2011 lakini linadhibiti baadhi ya maeneo ya taifa hilo.


Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom