Bumpkin Billionare
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 1,332
- 621
Nani kakwambia anguko la CHADEMA limeshindikana? Kuanguka kwa chama is a process, mwaka 1995 nani aliamini kuwa NCCR ya Mrema ingeangukia pua? Miaka michache iliyopita nani aliamini kuwa CUF itasambaratika?
It is only a matter of time hasa pale kampuni litakapokataa kubadili uongozi wake wa juu waliojihakikishia kuwa wao ndio wamiliki wa kampuni la CHADEMA.
Mr vag nal, kuanguka kwa itikadi kunategemea na nini ni msingi wa hiyo itikadi. Huwezi kulinganisha CUF, NCCR na CDM. NCCR ilikuwa ni mlipuko wa ushabiki, chama kilianzishwa na kukurupukiwa na wengi kwa ushabiki wa Mrema mrema mrema. CUF ni mkusanyiko wa watu wenye itikadi ya kidini na sera za kujaribu kubalasisha jambo fulani ambalo wao wanaamini haliko sawa, kilianza na kupigiwa chapuo na kuwa kipenzi cha watu duni wasio na uelewa.
CDM kwa upande mwingine ni genge la wasomi na wanaharakati ambao itikadi yao ni mageuzi. Kwa ulinganifu wa kiitikadi wa vyama hivi huwezi kukadiria anguko linalofanana kwani mawazo ya uasisi wake hayafanani.