Mlimani City sasa hivi: Kero hii haikubaliki!!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,331
24,216
Sasa hivi ninavyoandika nimetokea njia ya Sam Nujoma, Ubungo kwenda Mwenge. Pale Mlimani City nilitaka kuingia na gari ili niingie benki.

Kwanza nikakuta foleni kubwa toka mataa ya kuingia Sinza.

Pili baada ya dakika 15 sikuweza kuingia Mlimani City kwa vile nimekuta polisi wengi na geti limefungwa.

Geti la pili kule kuelekea Survey ndio foleni tena ya kufa mtu.

Nikauliza nikaambiwa Mh Waziri Mkuu yumo ndani kuna function ya sijui kitu gani. Kwa akili ya kawaida najiuliza hivi waandaaji wanatumia akili kweli?

Utafungaje access ya business premises kwa ajili ya matukio ambayo yanawaathiri watu wengi na wasiohusika?

Hapo Mlimani, benki zinakosa wateja,
- Maduka ya aina yote yanakosa wateja
- Maduka ya simu na mawasiliano yanakosa wateja
- Migahawa inakosa wateja

Sijui tunafikiri kutumia nini?
 
Japo Waziri mkuu ni VIP lakini kuna kila sababu ya hawa event planners wetu kuwapeleka Trainings nje ya nchi walau Waende wakaone Logistics za VIP motorcade mazingira ni tofauti kweli ila itawajenga sana na watarudi na kitu ambacho kitasadia hizi events na motorcade zisile muda wa watu bure niliwahi kukaa sehemu masaa mawili nangoja msafara upite, Ilibidi nipuuze Team yote iliyo plan kublock izo intersection yani ukiwaona na Radio call mpaka unasikia aibu kuwa je hawa watu hawafanyi mawasiliano kujua msafara ulipo
Mostly Events haziko well organized wala Coordinated, Nashauri Waanze kwenda Japan kuona jinsi VIP events na motorcade zinavyokuwa Planned haswa incase ikitokea zitachangamana na Shughuli za kawaida za watu au barabara
Kwa jinsi tu hizi shughuli zinavyoendeshwa nachelea kusema nina mashaka hata na ulinzi wa hayo maeneo
Na kwa sasa dunia iko ahead kweli kwa majiji kama dar mamalaka ilipaswa tayari iwe na Local app za ku update hali ya foleni na kuwe na multiple options ya kuchagua njia ili kusave time ku relay on Google map still haitupi uhakika mana kama kungekuwa na Local app hapo tayari watumiaji wa barabara na hio Compound ya mlimani city wangekuwa notified na kupewa suggestion, Time is money

Wakuu nisiwachoshe Magufuli mitano tena
 
Unalalamika nini wakati unajua kabisa hii nchi ni UTOPOLO.

You need to either help changing the system or get used to it.
Hata kulalamika ni sehemu ya kupashana habari na kukataa mabaya katika kubadilika.

Kuna watu wanakubali linalolalamikiwa kuwa ni jambo la kawaida.

Safari ndefu huanza na hatua moja.

Ili kutatua tatizo, jambo la kwanza ni kukubali hili ni tatizo.

Kuna watu bado hawajaelewa nankukubali kwamba hilo linalolalamikiwa ni tatizo. Wanaona ni kawaida tu.
 
Tena utopolo daraja la kwanza, Nina ndugu yangu yupo Tanga ni mtumishi wa serikali nimewasiliana naye muda si mrefu anasema wapo uwanja wa ndege wanamsubiri Majaliwa tangu saa tatu asubuhi.
Hayo mambo mengine yanafanywa makusudi kukuonesheni tu nani mkubwa.

Ni namna ya kisaikolojia kukufanya ujione dhaifu.

Mambo mengine ni wapambe tu wanajimwambafy, hata bila kuagizwa.

Mambo mengine ni utamaduni wa hofu tu tuliojijengea wenyewe wananchi.

Nani kafungua kesi mahakamani kupinga mambo kama haya? Angalau kupata hukumu ya mahakama tu na sehemu ya kuanzia?

Unawafungulia kesi mahakamani waliofunga biashara yako kwa siku bila sababu ya msingi, unawadai faida ya siku hiyo.

Hata ukishindwa kesi, Waziri Mkuu mwenyewe akisikia, siku nyingine akipangiwa kuja hapo, kama ana busara, ama ataomba watu wake wawe fair kwa wafanyabiashara, ama ataomba venue tofauti.

After all, na yeye ni mwanasiasa anayeangalia popularity yake.

Tatizo watu wamekubali na wanaishia kulalamika chinichini.
 
Back
Top Bottom