Mkuu wa Wilaya Vs Kamanda wa Polisi

Kuna kesi miaka ya nyuma ilitokea kuhusu wizi wa mbolea,watu walibomoa ghara la mbolea na kuiba,wakaenda kuweka hiyo mbolea kwenye mashamba yao,baadae upelelezi ukafanyika na wakagundulika na kukamatwa woote na kutiwa ndani, baadae mwl nyerere akawa ziarani hilo eneo,akaisikia hiyo hbr,alichokifanya ni kuamuru watolewa ndani hao wezi mala moja,na mabwana shamba waliokuwa wakihusika na kugawa hiyo mbolea woote akaamuru watiwe ndani kw kuchelewesha kuigawa hiyo mbolea wkt wakulima wanaihitaji,
Nyerere hakuwa DC, alikuwa Rais!!! Mwenye nguvu za kusamehe hata wafungwa
 
Stori ni hivi?
Baada ya jeshi la polisi kukamata mbolea ya ruzuku iliyokuwa inatoroshwa na wafanya biashara kwenda Malawi..Mkuu wa Wilaya akaamua kuzigawa kwa wananchi..
Kumbuka hyo mbolea ni kielelezo au ushahidi mahakamani unaohitajika kwenye kesi..Kikosi cha polisi kikatumwa kuzikamata tena hizo mbolea..Mkuu wa wilaya amekasirika ameamua kumuita kamanda wa polisi ofisini ajieleze..
Wajuzi hapa nani anakosa?

KICHWA CHA MWENDAWAZIMU
 
Sasa huyo kamanda si ange muweka mahabusu dc au alikuawa
Amemtaadharisha mara nyingi kuwa hiyo mbolea ni vielelezo. Hata Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Songwe amefafanua kuwa haiwezekani mbolea kugawanywa bila kibali cha mahakama. DC hahusiki na maamuzi hayo
 
hapo ndo patamu DCs kiufupi hawanaga kazi kabisa ni are ghosts in government payrolls... hata ukimuuliza kama ni mwanasiasa au mtumishi wa umma haelewi....hapo naona DC yupo sawa na hayuko sawa inategemeana na sababu ya kukamata mbolea...kama wahusika walenda mahakamani...ila DC anamwajibisha OCD coz ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya...anawasimamia makamanda wote wa wilaya wanaohusika na ulinzi.....mimi huwa napenda nikisikia DC akimkurupusha mkurugenzi unaona wanaangaliana tu mwisho wa siku Dc anavyata mkia anaendelea kupiga tumba........kazi zao ni issues za utoro wa wanafunzi, uzururaji na nyingine kama hizo ...hawaderve bendera kwenye gari zao kabisa

.....mimba,afisa gani anatamba aidha kwa vizibo bar au totoz, au anabadili mandinga kila kukicha....hapo sasa ma DC hawa kizazi kipya ni wivu na mapovu....
 
Hapo Polisi wana kosa la nidhamu na wanapaswa kuwajibishwa, Mkuu wa Wilaya ni sawa na raisi katika Wilaya, maamuzi yake OCD hapaswi kuyapinga hata kama kakosea. Huyo ni boss wake na anapaswa kutii pasipo kuhoji. OCD ni Mwakilishi wa IGP na DC ni Rais.

...DC wajibu wake ni kusimamia sheria na sera ktk wilaya....mengine wanajichomeka
 
Ni watu wawili wanaofanya kazi kwa sheria tofauti, tatizo siasa au tamko za kisiasa ndo mnaziona ndo sheria,
Ocd akifanya kazi inayoweza kumsababishia ashtakiwe kwa maagizo ya RC au DC atashtakiwa kwa mujibu wa taaluma yake. Wanaojielewa wanafuata sheria sio kauli za wanasiasa.
 
Military-army, navy, air force( they are addressed first by their ranks -Capt, Lt, Gen, Private etc( yeyote ambaye jina lake hutamkwa kwanza kabla ya rank au kama vile bwana au bibi fulani siyo military ila anaweza kuwa paramilitary)
Armed forces-army, navy, air force, para military forces including intelligence services, police, prisons, immigration, idara ya wanyamapori etc Wote wanabeba silaha na wanaweza kuwa mobilized kwa ajili ya national defense and security operations
 
Hapo Polisi wana kosa la nidhamu na wanapaswa kuwajibishwa, Mkuu wa Wilaya ni sawa na raisi katika Wilaya, maamuzi yake OCD hapaswi kuyapinga hata kama kakosea. Huyo ni boss wake na anapaswa kutii pasipo kuhoji. OCD ni Mwakilishi wa IGP na DC ni Rais.
Huyo boss anatakiwa awe na mawasiliano mazuri na wenzie. Vurugu zingetokea ktk ugawaji angehitaji msaada wa hao wadogo kwake.
 
Mkuu wa wilaya anafanya maamuzi kwa mzuka...nimewaonea huruma wananchi maana walishajitwika viroba vya mbolea kichwani kabla ya kushushwa kwa mabomu ya machozi.
yaleyale ya sukari ilifichwa kuigawa kwa raia
 
Military-army, navy, air force( they are addressed first by their ranks -Capt, Lt, Gen, Private etc( yeyote ambaye jina lake hutamkwa kwanza kabla ya rank au kama vile bwana au bibi fulani siyo military ila anaweza kuwa paramilitary)
Armed forces-army, navy, air force, para military forces including intelligence services, police, prisons, immigration, idara ya wanyamapori etc Wote wanabeba silaha na wanaweza kuwa mobilized kwa ajili ya national defense and security operations
Polisi wanaitwaje? Wanaitwa bwana na bibi? Mfumo wa Rank na majina ya Rank yanatokana na mfumo mnaotumia. Wengi wanaotumia mfumo wa Uingereza majina ya vyeo vya polisi yatakuwa Constable, cpl, sgt.... Inspectors, superitendents au Commisioners mpaka Inspector General. Hakuna Polisi anayetajwa bila cheo chake.
 
Nitashangaa kama wapo watanzania wanaodhani Mkuu wa Wilaya ni sawa na Rais kwa Jeshi la Polisi, kumbuka Jeshi la Polisi halipo chini ya Serikali ya Wilaya bali Amiri Jeshi Mkuu mmoja tu. Vitabu vya Polisi vinasema zipo Rank ambazo zinawajibika kuwapigia saluti ma-DC na sio zote. Kwa hiyo ukikuta OCD anapiga saluti hiyo is just ofa tu
Ofa kivipi ?
 
Naomba uelewe kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ipo kwenye Sheria ya Tamisemi ambayo Polisi wanaingia kama washauri kupitia Polisi Jamii na sio vinginevyo. Polisi hawatakiwi kupewa amri za moja kwa moja au maelekezo toka kwa viongozi wasio askari wa Polisi. JESHI LA POLISI LINAONGOZWA NA POLICE GENERAL ORDERS AMBAZO HAITOI MAMLAKA YEYOTE OVER POLISI KWA MWANASIASA YOYOTE ZAIDI YA AMIRI JESHI MKUU. Ukiona Polisi wanapokea maelekezo ya wanasiasa wanafanya hivyo kistaarabu tu.
Ok ndio maana kigangwallah wakamndia ?
 
Ofa kivipi ?
Saluti inapopigwa ina sababu, ni salamu kwa askari aliyevaa uniform kamili na kofia. Sio ishara ya kuonyesha kila anayepigpiwa ni bosi. Inspekta wa Polisi kwenda juu anapigiwa saluti bila mipaka nchi nzima, lakini DC atapigiwa na rank nilizozitaja hapo juu kwa lazima akiwa kwenye eneo lake la kazi tu na sio vinginevyo. Hiyo ya kusema weka huyu ndani ipo kwa kila mtu ikiwa aliyekamatwa kafanya jinai. CPA 12- 21. Ukisoma vifungu hivyo utaelewa mtu yeyote ( sio DC tu) ana uwezo na mamlaka ya kukamata akiona kosa
 
Mwanzo kabisa walipozikamata nakuelewana kwamba wazigawe kwa wanachi ndio kosa lilipofabyika, na polisi ndio wakishindwa kufanya kazi yao hapo maana polisi walitakiwa wabaki na kizibiti kwa ajili ya kesi
 
Back
Top Bottom