Mkuu wa mkoa Mtwara awatembelea watengenezaji wa pombe ya Gongo, afurahishwa na kuahidi kukirasimisha kinywaji hicho

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,145
Mkuu wa mkoa wa Mtwara amewatembelea vijana wenye mitambo ya kienyeji ya kuzalisha pombe ya gongo kwa kutumia mabibo.

RC huyo amefurahishwa na ubunifu wa vijana hao na kuchukua sampuli ya gongo hiyo yenye madaraja matatu kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara.

Endapo wataalamu wa maabara wataipitisha basi gongo mkoani Mtwara itarasimishwa na vijana hao watawezeshwa na taasisi za kifedha ili waweze kujenga viwanda vidogo.

Source Channel ten

Maendeleo hayana vyama.

=====

1583311195679.png

1583311249882.png
1583311268525.png

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa ametoa wito kwa wananchi wanaojihusisha na utengenezaji wa pombe aina ya gongo ya mabibo kujitokeza ili watambuliwe na bidhaa hiyo iweze kuboreshwa na kuingizwa sokoni.
 
Attachments

  • 1583311242781.png
    1583311242781.png
    25 KB · Views: 1
Mhe. RC kwa mbaaaali anaunga mkono juhudi za Mzee Lyatonga, Wale wakongwe wenzangu mtakua na kumbukumbu miaka ile 1995 hii ndio ilikuwa kete yake kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kuhakikisha Gongo ina halalishwa. Tusubiri tuone hatma ya Wanakuchele ktk hili.
 
k vant is more alcoholic than gongo.. but still k vant is not banned
Kinachofanya Gongo iharamishwe siyo wingi wa alcohol uliopo kwenye kinywaji. Gongo imeharamishwa kwa sababu haizalishwi, kuuzwa na kunywewa kwenye mazingira bora na yaliyokuwa monitored na mamlaka. eg. Kuwa na standard alcohol content inayoeleweka, ubora na usalama wa mali ghafi inayotumika kutengeneza, usafi wakati wa kuzalisha, mazingara ya uuzaji na unywaji kutokuwa rasmi na ugumu katika kufuatilia uzalishaji na unywaji wake. Vipengele vyote hivi vinasababisha mambo kufanyika kiholela na upatikanaji na bei kuwa rahisi na mwisho inaleta madhara kwa afya ya watumiaji wake.
 
Ni kweli, kwa mfano gongo ya maranda ya mbao ni hatari sana kwa afya!
 
Back
Top Bottom