Mkuu wa kituo cha Himo ondoa huyu askari mwenye nyota moja na trafiki walipo barabara ya Marangu karibu na mwanzo wa katani

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Ni sikitiko na masikitiko makubwa askari ambaye ana nyota moja yupo hapo barabarani akiwa amevalia kiraia na trafiki mmoja aliyevalia sare za kitrafiki, wanakamata magari yote yanayotoka Marangu Mwika, pamoja njia panda. Trafiki anasimamisha gari, hakagui gari, anachukua namba na leseni za madreva na kuwaagiza washushe abilia na kuwafata.

Kwa wenye cash wanatoa rushwa kesho kwa askari polisi mwenye nyota na kijana mmoja ambae nina imani nae ni askari polisi. Wasio na pesa wanaambiwa warudi hapo hapo walisha shusha abilia Ili wajisalimishe.

Hakuna gari inayokaguliwa, kila dreva anakaguliwa leseni basi, baada ya hapo unapewa kibano. Ni jambo la aibu askri polisi, afisa kabisa mwenye nyota moja kutongoza kundi la askari wasio na vyeo kwenda kufanya uhalifu.

Yote haya ni kwa sababu TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro, na hasa wilaya ya Moshi Vijijini hawatimizi wajibu wao ipasavyo. Hivi vitendo vya huyu askari sio leo wala jana walipunguza speed alipo wasema Kinana ila ni mwezi umeisha sasa upuuzi umerudi tena barabarani.

Angalizo mkuu wa kituo cha Himo, nina kusihi mkuu, Kilimanjaro hasa hapo. Sisi hatuwezi endelea kuona vijana wetu wanaonewa na askari wageni hao, wambie waache rushwa wafanye kazi kwa mujibu wa sheria. La sivyo tutalaumiana, hatuwezi ishi na mijizi inayo lipwa mshahara na tunao lipa mijizi iliyovaa gwanda ni sisi hapa.

Mimi dereva haice Mwika-Moshi, nimeandika kwa hasira sana.

Mkuu wa kituo ukitaka ushahidi nipo tayari maana hata picha nimepiga.
 
Yaaani huwezi kuwatenganisha Askar na rushwa ata iweje imagine kuna day askar 2 walitukamat watu weng t ikiwemo me pikipiki yng haijapass ikabidi tuende kituoni kufika kule anatupa ngonjer mwanae kakamatwa na chomb amepandish mahakaman amepigwa faini ya 250k akawa anasema live izi mtazilipa nyinyi hakuna mwengine akwa anaita mmoja mmoja ndan mankubalia kias gan utoe ukimpa hela anakuachia imagine mambo ayo yanafanyika kituon ndan kbs kufika zamu yng wakanambia niwape 30k 😂😂 nikawambia sina hela iyo mim piki piki yng kama mnavyoiyona ile pale mbov ila nimeshindwa kuitengenez nikawambia nawapa 5k wakawa wanazingua nikampigia cm ocd apo apo wakanipa chombo yng ila ile 5k niliwapa na wakaichukua 😀😁😂
 
Sisi hatuwezi endelea kuona vijana wetu wanaonewa na askari wageni hao, wambie waache rushwa wafanye kazi kwa mujibu wa sheria. La sivyo tutalaumiana,
Hapo ndipo ninavyotaka na iwe kwa vitendo haraka sana! Hii mijambazi inatakiwa ifunzwe kivitendo sasa! Mobilize abiria na madreva wenzako piga sana! halafu wakashtaki Learned friends tupo!!
 
Uliposikia namba wani anawaambia wale mawaziri wale kulingana na urefu wa kamba zao, unadhani askari hawakusikia?

Na wao wanakula kulingana na urefu wa kamba zao.

All in all,waboreshewe makazi na maslahi, labda itapungua hiyo hali.
 
Ni sikitiko na masikitiko makubwa askari ambaye ana nyota moja yupo hapo barabarani akiwa amevalia kiraia na trafiki mmoja aliyevalia sare za kitrafiki...
Safi sana.

Ikiwezekana wekeni Car DVR Camera iwe inarekodi matukio ya njiani kwenye njia gari inakopita.

Mimi kwenye magari yangu nimeweka hizo Camera hata traffic akinisimamisha anaiona na anaongea na mimi kwa heshima. Sipati usumbufu wowote toka kwao tofauti na kipindi kabla sijaweka, ilikuwa shida, mara naomba pesa ya lunch nk.
 
Ni sikitiko na masikitiko makubwa askari ambaye ana nyota moja yupo hapo barabarani akiwa amevalia kiraia na trafiki mmoja aliyevalia sare za kitrafiki, wanakamata magari yote yanayotoka Marangu Mwika, pamoja njia panda. Trafiki anasimamisha gari, hakagui gari, anachukua namba na leseni za madreva na kuwaagiza washushe abilia na kuwafata.

Kwa wenye cash wanatoa rushwa kesho kwa askari polisi mwenye nyota na kijana mmoja ambae nina imani nae ni askari polisi. Wasio na pesa wanaambiwa warudi hapo hapo walisha shusha abilia Ili wajisalimishe.

Hakuna gari inayokaguliwa, kila dreva anakaguliwa leseni basi, baada ya hapo unapewa kibano. Ni jambo la aibu askri polisi, afisa kabisa mwenye nyota moja kutongoza kundi la askari wasio na vyeo kwenda kufanya uhalifu.

Yote haya ni kwa sababu TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro, na hasa wilaya ya Moshi Vijijini hawatimizi wajibu wao ipasavyo. Hivi vitendo vya huyu askari sio leo wala jana walipunguza speed alipo wasema Kinana ila ni mwezi umeisha sasa upuuzi umerudi tena barabarani.

Angalizo mkuu wa kituo cha Himo, nina kusihi mkuu, Kilimanjaro hasa hapo. Sisi hatuwezi endelea kuona vijana wetu wanaonewa na askari wageni hao, wambie waache rushwa wafanye kazi kwa mujibu wa sheria. La sivyo tutalaumiana, hatuwezi ishi na mijizi inayo lipwa mshahara na tunao lipa mijizi iliyovaa gwanda ni sisi hapa.

Mimi dereva haice Mwika-Moshi, nimeandika kwa hasira sana.

Mkuu wa kituo ukitaka ushahidi nipo tayari maana hata picha nimepiga.
Mkuu abilia=abiria
 
Mkuu wa kituo cha Himo usipokee ushauri hovyo fanya kazi yako usisikilze ya watu wasio mapolisi. Usipokuwa makini unaweza kufanyia kazi ushauri wa wahalifu,
Mtu mwwnyewe unaitWa @ sexless?mwarifu babako kaka wewe ni afande na upo himo jiandaeni ubatizo wa moto unakuja ni balaaa
 
Yote haya ni kwa sababu TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro, na hasa wilaya ya Moshi Vijijini hawatimizi wajibu wao ipasavyo. Hivi vitendo vya huyu askari sio leo wala jana walipunguza speed alipo wasema Kinana ila ni mwezi umeisha sasa upuuzi umerudi tena barabarani.
Takukuru nao siku hizi hawana tofauti na wale waliokuwa wakisemwa kule ZNZ na Raisi Mwinyi! nao wamekuwa sehemu ya tatizo!
 
Back
Top Bottom