Mkuu wa kazi anapokuwa mwanamke kwanini aitwe 'mama'?

bhageshi

JF-Expert Member
Jul 24, 2010
264
101
Katika kushughurikia maswala yangu katika ofisi za umma na katika mabenki nimebaini kuwa baadhi ya wafanyakazi nilio wasikia wanatumia neno "MAMA" wakimaanisha mkuu wao wa kazi, awali ilinipa shida kuelewa ana maana gani katika ofisi fulani lakini baada ya kwenda ofisi nyingine nikakutana tena na msemo huo, nimefika mapokezi nikakutana na mfanyakazi wa kiume nakueleza shida yangu, naye akamuuliza mfanyakazi mwenzake wa kike eti "mama" yupo kuna mteja hapa anashida naye. sasa nikaanza kujiuliza kulikoni mbona mkuu wa ofisi akiwa mwanamme sijasikia akiitwa "BABA" badala yake wanatumia zaidi neno Boss au MKUU. Binafsi imenikera sana tena sana kwani kwangu mie mama ni mama tu na wala mtu mwingine hawezi vaa wasifu huo tena kwa mtu asiye hata na udamu na mama yangu. Au ndio ni aina fulani ya Rushwa ya unyenyekevu maofsini ili mtu kunufaika malupulupu kwa haraka. Nawaulizeni nanyi wanaJF kuitwa "mama" kwa kiongozi mwanamke maofsini je ni sawa kwenu?
 
Facilitator, mie sio mwanaharakati kama unaona sawa kwa upande wako basi kuwe na usawa kote na wakuu wa ofisi wanaume nao waitwe BABA kama haina shida

 
Facilitator, mie sio mwanaharakati kama unaona sawa kwa upande wako basi kuwe na usawa kote na wakuu wa ofisi wanaume nao waitwe BABA kama haina shida

Kwani wewe shida yako nini haswa?? Mbona kama kuna agenda ngumu sana hapa?? Unasumbuliwa na vitu vidogo namna hii??



 
@ Facilitator, shida yangu hilo neno si busara kutumika. lakini wewe mwenyewe unahisi kuna agenda ngumu wakati huohuo unaita vitu vidogo sikuelewi. kilichonikera zaidi hata umri wa huyo anaitwa mama ukilinganisha na anayemwita ni mdogo. Na nadhani hapa wanaoita wanaathiriwa na tamaduni za kuiga toka ng'ambo.
 
Maboss wa kike wanapenda ukuu uliotukuka..na usipomwita "mama" inaweza ikaku cost vitu vingi sana. Inategemea umeshika upande gani wa makali.

Sisi wengine hata mtu kumwita Boss ni vigumu..tunatumia tu majina yao...John, Mary, Sofia n.k

Aakinuna, akikasirika shauri yake...
 
Maboss wa kike wanapenda ukuu uliotukuka..na usipomwita "mama" inaweza ikaku cost vitu vingi sana. Inategemea umeshika upande gani wa makali.

Sisi wengine hata mtu kumwita Boss ni vigumu..tunatumia tu majina yao...John, Mary, Sofia n.k

Aakinuna, akikasirika shauri yake...

Kumbe ni aina fulani ya kum-fool boss wa kike ajione yuko juu kumbe ni mbwiga tu au ni nidhamu ya uoga wa baadhi ya wafanyakazi. mie nakuunga mkono kuwaita majina yao
 
Mfumodume-limbwende.

Angalia hata Wamalawi wanamuita rais wao "President Mrs. Banda"

Sasa sijui itakuwaje kama mkuu wa kazi mwanamke halafu hajaolewa wala hana mtoto, sijui atakuwa mama au dada?
 
Ngoja nao wakija watatuambia wanaopenda kuitwa hivyo na wanaowaongoza kuwa yakitokea uliosema lipi litumike

Mfumodume-limbwende.

Angalia hata Wamalawi wanamuita rais wao "President Mrs. Banda"

Sasa sijui itakuwaje kama mkuu wa kazi mwanamke halafu hajaolewa wala hana mtoto, sijui atakuwa mama au dada?
 
Majina ya staha ni kuwa: Mwanamke = MAMA; Mwanamme = MZEE. Na hivyo ndivyo mambo yanavyofanyika.

Nakubaliana nawe lakini je kuyatumia mahali pa kazi wewe binafsi unjisikiaje. MZEE yupo jamani ofisin mwake, inaweza ikasababisha akawa Mzee wa kiukwelikweli mahali pa kazi
 
wengi wao wanajikweza sana, wanajiona miungu watu, hawapendi kukosolewa hata wanapombolonga, mm wananikera sana sitaki hata kuwaita jina hilo tukufu la mama( Mzazi pekee mwenye uhakika wa kutuzaa).Naomba nieleweke siyo wote.
 
Bosi wangu namuita kwa jina lake tena la kwanza bila tatizo, nadhani inategemea na mazingira. Sijasikia mtu akiitwa bosi, mama au mzee. Awe she/he tunamu-address kwa jina lake.
Kama alivyouliza mdau hapo juu kumwita mtu mama ilhali hana mtoto inaweza kuwa inamuumiza pia kimoyo moyo.
 
Mi nashindwa kuelewa tatizo liko wapi. Shida yako maneno "mama"/"mzee" unayatumia kama dhana ya kizungu badala ya ile ya kiafrika. Kwetu waafrika au niseme watanzania maneno "mama" au "mzee" ni mapana sana. Hayana maana ya mama mzazi tu au mzee (baba) mzazi tu bali yana maana ya mtu yeyote mwenye umri mkubwa sana kwako au pia kama ulivyosema kwenye mada yako yanaweza kutumika kwa mtu mwenye cheo kikubwa au wadhifa, yaani bosi wa mahali. Hizi ni maana zilizonyambulishwa. Kwetu watanzania hatuna shida na hizo dhana.

Sasa je ni sahihi kutumia maneno/majina hayo maofisini? Mi nasema: Ndiyo ni sahihi. Yanaonesha heshima. Lakini pia yanaonesha aina ya solidarity au mshikamano uliopo kati ya wafanyakazi na bosi wao, wanakuwa kama familia moja chini ya kiongozi (bosi) wao ambaye ndo huyo wanayemuita "mama" au "mzee". Mi hapo sioni kujikomba unakokudai au ubaya wowote. Na kimsingi bosi akiielewa vizuri hiyo title ya kuitwa "mama/mzee" na kuichukulia kichanya anaweza kujenga mahusiano mazuri na wale walio chini yake; tena ataona aibu hata kuwanyanyasa. Kwa kifupi atajiheshimu na kuwaheshimu hao wanaomwita "mama/mzee".
 
Yaani afadhali umesema! Hii inanikera mimi kuliko maelezo.
Sasa imagine naongea na mwanaume mtu mzima na yeye anamuongelea 'mama'. I get confused manake is he talking of his mother? Aaaaaghh!
 
Mbona kitu cha kawaida hicho.hata kwenye mila zetu kinatumika.mfano kabila moja huko kanda ya ziwa mtu mzima yeyote aliyekuzidi/unayemheshimu ukita kumuita lazima utangulize prefix flani kwenye jina lake yenye maana ya mama au baba mfano. Jina Mukandara lazima useme TaMukandara au kwa mwanamke Tibaijuka lazima useme MaTibaijuka.prefix Ta ni kifupi cha Tata kwa maana ya baba na Ma ni kifupi cha Mawe yaani mama. Kwa hiyo kumuita mtu Mama ni heshima tu kwa mtu huyo na haikupunguzii chochote.
 
Back
Top Bottom