Mkuu wa demokrasia Tanzania

Mangaline

JF-Expert Member
May 19, 2012
1,045
221
Kila mtu aweza kuwa na mapungufu katika maisha yake. na vilevile kila mtu aweza kukumbukwa kwa moja au mawili, katika kipindi cha utumishi wake. Katika wakuu wa kaya wa awamu zote, Mkuu wa kaya wa awamu hii, namsifu sana kwa kuwa mkuu pekee katika awamu zote, ambaye kwa kweli na kwa dhati, ametoa uhuru wa kutosha kwa wananchi wake, kwa vyombo vya habari na kwa jamii yote kwa ujumla kuwa huru kutoa maoni au mawazo bila kubugudhiwa. kwa ujumla wake, ni kamanda wa DEMOKRASIA TANZANIA.
Ni kutokana na sababu hii, wananchi sasa wameweza kupata habari kwa urahisi, hatimaye sasa uelewa na uhuru wa wananchi kujiunga na vyama vya siasa umeongezeka, hali ambayo imepelekea cdm kufahamika na kuvuna wanachama wengi kuliko wakati mwingine wowote.


WAZO LANGU
jamii itambue mchango wa mkuu wetu wa kaya katika kukuza uhuru wa kidemokrasia wa kutoa maoni, uliopelekea cdm kujengeka, hadi kukaribia kuteka nchi, na nyinyiemu kupoteza mvuto kwa jamii.

MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA
 
Back
Top Bottom