rosemarie
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 6,887
- 3,412
Wakuu wangu naombeni kwa moyo mmoja kabisa mnisaidie kwenye hili,siku hizi hatupati zile tv za ITV na Star tv, na nyinginezo, tuinapata TBC na radio zao peke yake.
Kasa tumeonyeshwa huyu mkuu akiwa anahojiwa na baadhi ya watangazaji mahiri wa Tbc ambayo tunatazama bila kupenda! Mkuu huyu alihojiwa kwenye ofisi yake iliyosheheni mavitabu ya kila aina yakiwemo ya sheria na hadith mbalimbali.
Kwa bahati nzuri au mbaya huyu mkuu nimeishi naye jirani maeneo ya mianzini pale Arusha na ulitokea ugomvi kati yake na mpangaji mwenzake nafikiri yalikuwa mambo ya mademu,alifukuzwa nyumba ile na kutia timu maeneo ya sakina ambako sikumwona tena mpaka nilipokuja kustuka kumwona bungeni!
Wakuu naombeni mwenye cv ya huyu kiongozi anipatie kwa sababu nimepatwa na maswali kutokana na stahili yake ya kukusanya mavitabu mengi na kupiga picha mbele yake,haya niliyaonaga kulele CNN wanapohoji wazito kama wakina baraka obama au bill clinton wanatokea mbele ya mavitabu kibao
Naombeni wakuu wangu nijue elimu ya huyu kiongozi mahiri kabisa anayekuja na stahili ya watazamaji kujiuliza mara mbili mbili.