Mkutano wa kimataifa wa kutokomeza ukeketaji 09- 11 Okt, 2023 Dar, JNICC

Dkt. Gwajima D

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
543
3,575
Ndugu Wanajukwaa, nawasalimu kwa Jina la JMT.

Kwa heshima tafadhali pokeeni ujumbe huu wa Wizara yenu ya Jamii, Ili twende Pamoja kwa Maendeleo na Ustawi wa Jamii.

Kesho 9 hadi 11 Okt 2023 tunaanza Mkutano wa Kimataifa wa kutokomeza Ukeketaji.

1. Mkutano huu utaenda sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo huwa ni tarehe 11 Okt kila mwaka.

2. Kuhusu ukeketaji kwa watoto wa kike; takwimu za Afya, Idadi ya Watu na Viashiria vya Malaria mwaka 2015/16; Ukeketaji umepungua kutoka 30% mwaka 2010 hadi 10% mwaka 2015. Mikoa yenye takwimu za juu ya wastani; Manyara (58%), Dodoma (47%), Arusha (41%), Mara (32%), Singida (31%) na Tanga (14%).

3. Kutokana na utekelezaji wa Sheria ya kuzuia vitendo hivi, baadhi ya jamii imekuwa ikikeketa watoto wadogo na wachanga ili isifahamike na kushtakiwa. Imetungwa Sheria ya Kanuni ya Adhabu kifungu 169A na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 na pia, Serikali na Wadau wanatoa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii kuhusu madhara ya ukeketaji ili waachane na mila hiyo.

4. Kwa Afrika, jitihada za pamoja zinahitajika. Hivyo, Tanzania ilishiriki Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Kutokomeza Ukeketaji nchini Burkina Faso mwaka 2018 ulioazimia kila Kanda Afrika ianzishe ushirikiano wa kupambana na mila na desturi ya ukeketaji ikiwemo kudhibiti mipaka ya nchi kuzuia mwingiliano wa mila.

5. Umoja wa Afrika umeichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Kutokomeza Ukeketaji ambao umepangwa kufanyika tarehe 9 hadi 11 Oktoba, 2023 DSM, Ukumbi wa JNICC. Mkutano huo utakutanisha Washiriki 900. Kaulimbiu ni “Mabadiliko katika kizazi kimoja kwenda kingine ni muhimu katika kutokomeza vitendo vya ukeketaji”.

6. Sambamba na mkutano huo, kutafanyika pia Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike tarehe 11 Oktoba. Kaulimbiu ni "Haki Zetu ni Hatima Yetu; Wakati ni Sasa”. Aidha, Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike Tanzania itaadhimishwa pia mikoa yote chini ya uongozi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya.

7. Kwenye kipindi hiki pia kutakuwa na mkutano mwingine wa Ajenda ya Wasichana wenye Kaulimbiu Mimi ni Nani?: Kubadili Tamaduni na Mazoea ili kujenga Kizazi cha Wasichana Wanaojiamini’’ ambao utafanyika tarehe 11 Okt, 2023 ukumbi wa Mlimani City Jijini DSM, 3.00 asubuhi.

Mikutano yote 3 inashabihiana kimkakati.

Ahsanteni sana, naomba kuwasilisha.

Yes, You're Honestly Madame Minister.
Vipi hukusu mwaliko?

Sasa huo ukeketeji mnajua vizuri mikoa iliyo kipaumbele kwenye hiyo tabia.

Why don't you meet kwenye hiyo mikoa.

The place where you can get evidences na pia kuongea na hao ngariba na kuwapa mafundisho of what they're doing.

But anyways, wish you all the best.
 
Ahsante Sana kwa maoni yako, baada ya mkutano huu, huu ushauri tutauweka kwenye mipango kazi yetu na kuweka Kambi huko huko kwenye mikoa na wilaya zilizoathirika

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Asante hata kwa kujibu.

Kupitia jf utapata elimu kubwa ya hizo tohara.

Naamini hata ngariba wengine wapo humu humu.
Ukeketaji ni ritualistic social and cultural event. Haiwezi kuondoka tu ghafla hat kwa mauaji ya alaiki. Organization nyingi zinaendesha jitihada kuiondoa hii lakin kazi BDo nzito.

Gwajima aweke mkakati wa community engagement ambao hutakuwa pragmatic. Pia ukeketaji ukiungalia unefubgamana sana na jamii za wafugaji. Mwanamke anaekeketwa analipiwa mifugo mingi sana. Kula mwanamke anataka aolewe na thaman ya juu. Mm nina idea moja
 
Kwanza wizara ilikuwa na mradi wa snaujata. Nimefatilia sana lakini sioni tathmini yoyote y maendeleo yake ikiwa wazi mama yetu gwajima. Where we go should reflect our move and assess our progress. Kesi nyingi zinapatikana ngazi ya watu wanaojitoleaaa katika Kijiji. Je ni kesi ngapi mpaka leo za Ukatili zinafatiliwa na mradi huko mamlakani?
 
Hivi hao wanaokeketwa wako wapi?

Je, huko hosp wanakozalia huwa kuna takwimu gani? au wote wanazalia kwa wakunga wa jadi?

Hao wanaume waliobahatika kuoa hao waliokeketwa nao wanasemaje kuhusu furaha ya hao wanawake kwenye tendo la ndoa ?

Hao wanaume je are they enjoying ?
 
Mm mwenyewe nimemsikia Mzee mtu mzima nilienda ziara saiti huko kipunguni akisema, ilibidi aoe mke ambaye hajafanyiwa hivyo kutokana na changamoto ambazo alizielezea mubashara ambazo pia sayansi imeziielezea. Mfano kutokana na makovu yanatokea huko, zile tezi zinazozalisha lubricant zinakuwa zimeharibiwa hivyo wanakuwa very dry, na kinachopokelewa wakati wa penetration yoyote ni maumivu hivyo, wanakuwa na tabia ya kutopenda na kutotoa ushirikiano. Lakini pia, nerve endings zinazo ratibu tendo lile kuwa liwe ni furaha zinakuwa zimeondolewa hivyo kuongeza tatizo lingine jipya la hisia za furaha kupotezwa. Mwanaume hapo sijui sasa yy anafurahia nn.

Shida zingine ni maambukizi ya kila Leo maana zile tissues kuharabiwa vile maana yake na mifumo ya ulinzi nayo inavurugika. Bado damu kupotea, bado wakati wa kujifungua hayo mabadiliko ya jiografia ya eneo hilo husababisha uzazi pingamizi.

Lingine, saikolojia sasa pale akijitambua muathirika, inaongeza shida ingine.

Shida zote hizi humfanya muathirika asijiamini, hana ushirikiano nk sasa hapo mwenza wake akipata mwenye ushirikiano huko nje ndiyo mtikisiko wa ndoa sasa huanzia hapo. Haya nimesikia mwenyewe kutoka ushuhuda wa yule Mzee na clip iliwahi kwenda viral sana. Lakini wamama nao wako ambao wamewahi kushuhudia. Na tafiti za kisayansi nazo zipo za kutosha na kesho mtasikia.

Hospitalini huwa wanaenda wengi tu....

Ahsante Sana kwa mchango wako wa swali zuri sana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza wizara ilikuwa na mradi wa snaujata. Nimefatilia sana lakini sioni tathmini yoyote y maendeleo yake ikiwa wazi mama yetu gwajima. Where we go should reflect our move and assess our progress. Kesi nyingi zinapatikana ngazi ya watu wanaojitoleaaa katika Kijiji. Je ni kesi ngapi mpaka leo za Ukatili zinafatiliwa na mradi huko mamlakani?
Hbr za mchana. SMAUJATA siyo mradi bali mtandao wa wanaojitolea kubeba ajenda za kuhamasisha jamii pale walipo, yaani kuanzia kwenye familia zao na kisha wenye uhitaji wanaelimishwa kuwa wafike huduma za ustawi wa jamii ambazo wengi awali wala walikuwa hawajui. Ni sawa tu na mtu aende kwenye jamii ambayo hawaamini kwenye huduma za zahanati au hospitali wao ni ramli tu.

Basi anayejua ambaye ni sehemu ya jamii huwaelimisha kuwa jamani huyu mtoto anahitaji mfano chanjo mbona hata hajawahi pata? Basi watu wale wakisikia simulizi hizi hushawishika kwenda huko kwenye mfumo rasmi. Hii ndiyo engineering ya SMAUJATA na wala siyo mradi.

Na wanafanya kwa ushirikiano na mifumo iliyoko huko mfano kamati za Ulinzi wa Wanawake na watoto, madawati ya Ulinzi shuleni, mabaraza ya watoto, maafisa ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii. Ni activists wa ajenda za ustawi na maendeleo ya jamii.

Kwa kufanya hivyo, fuatilia taarifa za walioenda kuripoti Polisi kuhusu ukatili wa watoto na wanawake waliongezeka kati ya 2021 na Jan Dise 2022. Maana yake Sasa elimu inasambaa Sana na watu wanajua sasa kuna wizara na kuna huduma za ustawi wa jamii.

Labda kama unahitaji ufafanuzi zaidi karibu.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Ukeketaji ni ritualistic social and cultural event. Haiwezi kuondoka tu ghafla hat kwa mauaji ya alaiki. Organization nyingi zinaendesha jitihada kuiondoa hii lakin kazi BDo nzito.

Gwajima aweke mkakati wa community engagement ambao hutakuwa pragmatic. Pia ukeketaji ukiungalia unefubgamana sana na jamii za wafugaji. Mwanamke anaekeketwa analipiwa mifugo mingi sana. Kula mwanamke anataka aolewe na thaman ya juu. Mm nina idea moja
Ahsante Sana kwa maoni yako.

Mkakati upo na umeandaliwa na wadau wote kwa data za kitafiti. Hivyo, kwenye mkakati sidhani kama ni shida. Nitaupandisha siku moja hapa.

Changamoto ninayoiona mimi ni utayari wa mtu mmoja mmoja kubadilika na kujiona sehemu ya mkakati, hasa sisi ambao tumejaliwa mwanga fulani hivi, je huko tunakotoka kwenye jamii zetu tunaona ni jukumu letu hili kama tunavyofanya kwenye kuunda vikundi vya kijamii vya VICOBA, jumuiya na mijadala ya events mbalimbali au tunaona haya hadi serikali ije na matamasha rasmi?

Unaenda mtaani unaulizwa maswali na jamii, unasema mbona hapa kuna waelewa tu na wana vikundi mbalimbali vya maendeleo? Je hii ajenda kwa nn isiwe sehemu ya kutazamwa kwa jicho la maendeleo? Majibu hakuna....

Ukiuliza vipaumbele vyao utasikia maji, afya, barabara, mifugo, umeme, elimu, nk... lakini haya ya ukatili wao siyo issue... ila wanalalamika Sana....

Hebu naomba maoni, lini tutabadilisha mawazo na kumiliki ajenda za changamoto za kijamii sisi wenyewe? Mfano wewe ndugu yangu unajiunga na SMAUJATA, FAGDI, SAWATA, MALEZI network.. maana huku wote walioitikia wito wako huku... au unaanzisha network yako ya elimu kuanzia ulipo na walipo Wana network...

Karibu kwa majadiliano tafadhali, maoni yako ni muhimu...

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Mwamko unahitajika sana katika mikoa tajwa ,nasikitika sana kuona mkoa wangu wa Mara ukiwa miongoni mwa mikoa yenye takwimu hizo..
Hakika inasikitisha, lazima Wana Mikoa hii wenyewe ambao wametambua ukweli basi wawe na utayari wa kukaa pamoja na kujadili vipi wafanye Ili kusaidia wengine. Iko mikoa hiyo ukienda kwa wazazi nasikia ukasema hizi habari utawaashiwa moto hadi utatengwa, ww mtoto wao mwenyewe, je akienda wasiyemjua? Hivyo hapa inatakiwa wote tuungane bila kuogopa na kwenda na elimu tukianza na tuliomo humu pia tutoke humu twendeni makwetu kuelimisha. Kama ni content ya kusema na vipeperushi na fact sheets, hiyo sasa ni kazi ya wizara.

Ahsante Sana. Tuendelee kujadiliana

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Mm mwenyewe nimemsikia Mzee mtu mzima nilienda ziara saiti huko kipunguni akisema, ilibidi aoe mke ambaye hajafanyiwa hivyo kutokana na changamoto ambazo alizielezea mubashara ambazo pia sayansi imeziielezea. Mfano kutokana na makovu yanatokea huko, zile tezi zinazozalisha lubricant zinakuwa zimeharibiwa hivyo wanakuwa very dry, na imesikia mwenyewe kutoka ushuhuda wa yule Mzee na clip iliwahi kwenda viral sana. Lakini wamama nao wako ambao wamewahi kushuhudia. Na tafiti za kisayansi nazo zipo za kutosha na kesho mtasikia.

Hospitalini huwa wanaenda wengi tu....

Ahsante Sana kwa mchango wako wa swali zuri sana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Ni hatari saana, na pia tunaambiwa mwanamke alie keketwa huwa malaya ni kweli?
 
Ni hatari saana, na pia tunaambiwa mwanamke alie keketwa huwa malaya ni kweli?
Sijui Sana ndugu yangu, ila labda baadhi hujikuta katika kutafuta walau hiyo pleasure labda wataipata labda pale na pale? Na kama ni hivyo, hatuoni kuwa kuwaita jina hilo HATUWATENDEI HAKI? Baada ya sisi jamii kuwatengenezea tatizo la msingi kisha sasa tunatengeneza lingine? Mm sijui ila nakataa... hiyo tabia kama ipo tutafute Sababu tuchambue.

Ahsante kwa maoni, ndiyo tunajifunza hivyo shida zilizoko huko kwenye jamii.

Dr naomba ile formula ya dawa ya kujifukiza ya COVID 19.
 
Ndugu Wanajukwaa, nawasalimu kwa Jina la JMT.

Kwa heshima tafadhali pokeeni ujumbe huu wa Wizara yenu ya Jamii, Ili twende Pamoja kwa Maendeleo na Ustawi wa Jamii.
Mheshimjwa
Ninapinga ukeketaji. Ukeketaji ni ukatili dhidi ya wasichana na wanawake

Lakini jamii na serikali inapaswa kutambua kuna mafunzo mengine kwenye unyago yanafaa kwa wasichana wanaokua. Suala la ukeketaji lisifute mila na desturi zingine ambazo hazina madhara.

Basi serikali ije na mpango mkakati wa kuelimisha mabinti wanaoingia rika la ujana bila kujali elimu au wajihi wao.
 
Ahsante Sana, mpango upi unaitwa Kuwekeza kwenye Maendeleo na Afya kwa Vijana Balehe. Ukirejea hotuba yangu ya Bajeti 18 Mei 2023 kuna data za kutosha za utekelezaji. Na serikali inaongelea Mila zile Hasi tu siyo chanya. Na hizo Hadi zinapambanuliwa kwa takwimu zinaozoonesha athari za kiafya, kiuchumi, na kisekta zingine.... usipofanya hivyo kwa data, huwezi wekeza hela za serikali kutekeleza kitu hakina mizania ya faida na hasara. Ahsante Sana kwa maoni yako, barikiwa

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom