Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi za SADC - Dar Es Salaam Tanzania

Sasa mbona anasifiwa sana Magufuli utafikiri yeye ndio amefanya mkutano huu ufanyikie Tanzania
Wasifiaji ni watanzania, angalia kwenye forums/social media kwenye nchi nyingine kama wanamsifia ila kwa mgeni kumsifia mwenyeji mara nyingi huwa ni given
 
MKUTANO WA SADC WAFUNGULIWA RASMI

Mkutano huo unaozihusisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC) umeketi leo jijini Dar es salaam

Marais na viongozi mbalimbali kutoka nchi wanachama wakiongozwa na mwenyeji wao Rais Magufuli wametoa hotuba zao

Katika mkutano huu, Rais Magufuli atakabidhiwa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo
View attachment 1183645
Marais wastaafu wa Serikali ya Tanzania wamehudhuria Mkutano Mkuu wa 39 unaofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kushuhudia Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli akikabidhiwa Uenyekiti wa jumuiya hiyo.

Katika mitandao ya kijamii baadhi ya watu wasiokuwa na njema walikiwa wakizusha kuwa Dk.Magufuli amesusiwa mkutano huo na watangulizi wake.Hata hivyo uzushi wao umekosa mashiko kwani viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo marais hao wote wastaafu wamehudhuria mkutano huo wa kihistoria.

Marais wastaafu ambao wamehudhuria ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye ni Rais ww Serikali ya Awamu ya Pili,Benjamin Mkapa ambaye ni Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu,Jakaka Kikwete aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne na kwa upande wa Zanziabar Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Amani Karume.


Mbali ya wastaafu hao kuwemo kwenye mkutano huo ambao pia wametambulishwa kwa wageni mbalimbali kutoka nchi 15 za jumuiya hiyo,pia viongozi wengine wa Serikali ya Tanzania waliohudhuria ni Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Balozi John Kijazi,mawaziri, viongozi wa ngazi mbalimbali wastaafu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda.Pia wamehudhuria watu mashuri wa ndani na nje ya Tanzania.

Pamoja na shughuli mbalimbali ambazo zinaendelea kwenye mkutano wa jumuiya hiyo ambao utafanyika kwa siku mbili,tukio ambalo linasubiriwa na Watanzania wengi ni kuona Rais Dk.Magufuli anakabidhiwa Uenyekiti wa SADC.

Nafasi hiyo ya Uenyekiti wa SADC kwa Tanzania mara ya mwisho ilishikiliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa miaka 16 iliyopita na sasa anakwenda kukabidhiwa Rais mchakazi Dk.Magufuli.

Hata hivyo nchi mbalimbali za jumuiya hiyo zimeonesha matumaini na imani kubwa kwa Rais Magufuli hasa kutokana na utendaji wake tangu akiwa Rais ambaye anaamini katika wananchi kufanya kazi na nchi kujitegemea.

Pia amekuwa na kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda ambayo itaipeleka nchi uchumi wa kati.Kwa nchi za SADC moja ya mkakati wao ni kuhamasisha viwanda kwa nchi wanachama kazi ambayo Rais Magufuli ameianza kabla ya kukabidhiwa uenyekiti,hivyo nchi za jumuiya hiyo zinaamini akiwa Rais Magufuli atawafikisha kwenye nchi ambazo uchumi wake utatokana na viwanda.




Mkuu naomba kuuliza.. wamehudhuria marais wangapi mkutano huu
 
Nataka kujua idadi ya marais walio hudhuria huu mkutano
Marais wa nchi 11 wamehudhuria mkutano wa kilele wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) unaofanyika jijini Dar es Salaam, Nao ni:

John Magufuli (Tanzania),
Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini),
Azali Assoumani (Comoro),
Danny Faure (Shelisheli),
JoaoManuel Goncalves (Angola).
Edgar Lungu (Zambia),
Felix Tshisekedi (DRC),
Andry Rajoelina (Madagascar),
Emerson Mnangagwa (Zimbabwe),
Filipe Nyusi (Msumbiji) na
Dk Hage Geingob (Namibia).
 
Marais wa nchi 11 wamehudhuria mkutano wa kilele wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) unaofanyika jijini Dar es Salaam, Nao ni:

John Magufuli (Tanzania),
Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini),
Azali Assoumani (Comoro),
Danny Faure (Shelisheli),
JoaoManuel Goncalves (Angola).
Edgar Lungu (Zambia),
Felix Tshisekedi (DRC),
Andry Rajoelina (Madagascar),
Emerson Mnangagwa (Zimbabwe),
Filipe Nyusi (Msumbiji) na
Dk Hage Geingob (Namibia).
Watano wana udhuru etiee
 
Haya mambo nayasikia tu huko kwa wengine hebu ngoja tuone safari ikianza kwa driver kuingiza gear.
 
Tulia Hapa Hapa Utaipata


Usisahau Pia
Hotuba Nzuri Sana Ya Mheshimiwa Mpya Wa SADC
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Ambaye Anataka Kuibadili SADC Iache Urasimu Usio Na Sababu Hasa Kwenye Upande Wa Kukimbilia Ulaya, Asia Kununua Vitu Vinavyopatilana Kwenye Nchi Wanachama Wa SADC


Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Yupo Vema
Nahitaji sana soft copies za hizo speech (Ya Dr. Tax na Dr. Magufuli)
 
Write your reply...SADC ni genge la majambazi tu ...sema viongozi wake wanavaa suti na kulindwa na mitutu
 
Magufuli anawaongoza maRais wa nchi zaidi ya kumi
Hakika tumepata mchapa kazi
Magufuli oyeee for the next 40 years. Jamani tuwe wakweli. Nchi ilikuwa inanuka uozo. Huyu jamaa anajitahidi sana kufagia. Hata hivyo there is so much dirty, it will take 30 years to clean. that is why we need John for the next 40 years.
 
Back
Top Bottom