Mkutano mkuu wa tisa wa jumuiya ya wazazi CCM Taifa

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau,
Mkutano Mkuu Wa Taifa Wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi unaendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

TBC wapo Live muda huu

Mzalendo namba moja Mh Rais John Pombe Magufuli atafungua Mkutano huo.Tayari wajumbe wameshaingia ukumbini huku burudani zikiendelea. Mwenyekiti wake Chama atawasili muda wowote kuanzia sasa ili kufungua Mkutano.

Mh JPM tayari ameshaingia ukumbini.
Utambulisho wa vyama rafiki
1.TADEA 2.UDP 3.AFP 4. ANRA 5. CCK 6.T.L.P 7.CUF 8.UMD 9.DP 10.MAKINI

Idadi ya Wajumbe Wa Mkutano Mkuu Wa Wazazi Taifa 815.

Malengo ya Mkutano

1.Kuchagua viongozi wakuu

2.Kufanya tathmini ya Jumuiya kwa miaka mitano iliyopita

3.Kutoa uelekeo wa Jumuiya kwa miaka mitano ijayo.

Wanachama wapya waliosajiliwa takribani 800, 000

Fedha zilizopo kwenye akaunti ya Chama Tshs Bilioni 2.1

Baadhi ya vitega uchumi vya Jumuiya

Chuo cha Mifugo Kaole Bagamoyo kinachotoa Diploma na Certificate. Kina uwezo wa kuchukua Wanafunzi 600

Jengo la ghorofa lenye thamani ya Billion 8. - 9

Wanaopewa Zawadi

1. Mh Rais John Magufuli.2.Mama Janeth Magufuli 3.Mh. Abdalah Bulembo 4 Maalimu Seifu,5.Walimu Wakuu wa Shule 6 za Sekondari za Jumuiya zilizofanya vizuri kitaaluma Same, Shaulitanga, Mombo, Sangu na Ivumwe.

More updates.
Mwenyekiti wa Chama JPM sasa anazungumza na Wajumbe wa Mkutano
JPM anampongeza sana kwa msisitizo mwenyekiti anayeondoka Ndg Abdallah Bulembo kwa kazi nzuri sana aliyoifanya kwa CCM. Anamfahamu vizuri sana na alizunguka naye wakati wa kampeni za uchaguzi.

Wajumbe kutokea Jumuiya ya Wazazi wataongezwa kwenye Bunge baada ya ombi la Ndg Bulembo.Utaratibu utafanywa ili kuwe na uwiano wa wajumbe katika Bunge. Kwa sasa UVCCM inatoa wabunge 5 wakati Umoja wa Wazazi unatoa mbunge 1 tu!

JPM amesema Jumuiya ya Wazazi haitafutwa wakati wa kipindi chake
Ameagiza Shule ambazo Jumuiya imeshindwa kuziendesha wazirudishe Serikalini na Serikali itawalipa fedha.

Wajumbe wasikubali mtu awachagulie mtu.
Amewaomba wajumbe kabla ya kupiga kura wamtangulize Mungu kwanza.
Wajumbe wachague mtu atakayewatetea.

JPM amesema kuwa hana mtu katika wagombea waliopo bali atakayechaguliwa ndiyo atakuwa mtu wake.

Wachague mtu atakayesimamia vizuri miradi ya Chama.
Wachague Viongozi watakaotetea Chama, Umoja wa nchi yetu na kusimamia vema shughuli za Chama.

Ameagiza kuwa Viongozi watakaochaguliwa waendelee kufanya tathmini ya mali za Jumuiya pamoja na kuziendeleza.

Aidha ameagiza Jumuiya ikemee ukiukwaji wa maadili nchini na ametoa mfano kwenye uchezaji wa muziki hasa kwa baadhi ya wasichana.

Wasimamizi wa maadili wapo wapi? TCRA, Wizara ya Habari n.k
JPM ametoa Tshs 250 million kwa ajili ya Mkutano. Aagiza hela hizo zitolewa mara moja kwa Jumuiya ya Wazazi.

Wakasimamie vizuri masuala ya Elimu.
Anamshukuru Mama Maria Nyerere na Mama Karume.
Wasichague kwa kuangalia sura, ukabila au dini. Wachague Mtu atakaesimamia jumuiya iweze kusimama vizuri

JPM amemaliza kutoa hotuba.
Utambulisho unafanywa na ndugu Bulembo kwa Wanachama wapya ambao ni Ndg Msando, Ndg Machali, Ndg Katambi, Ndg Mtulia na Ndg Kafulila.

Mwenyekiti anaondoka ukumbini baada ya kuagana na wajumbe ili kuendelea na shughuli nyingine za kitaifa.

NB: Tutwaletea matokeo ya uchaguzi huo baadaye Leo.

Karibuni.
 
Wadau
Mkutano Mkuu Wa Taifa Wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi unaendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.
*TBC wapo Live muda huu*
Mzalendo namba moja Mh Rais John Pombe Magufuli atafungua Mkutano huo.Tayari wajumbe wameshaingia ukumbini huku burudani zikiendelea. Mwenyekiti wake Chama atawasili muda wowote kuanzia sasa ili kufungua Mkutano.
Karibuni.
Mzalendo hafanyi mambo gizani.... mzalendo wa kweli hachukii kukosolewa na mzalendo wa kweli hupenda watu wote!
 
Badala ya kuweka live mambo ya maana wanaweka haya ya kipuuzi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wadau
Mkutano Mkuu Wa Taifa Wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi unaendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.
*TBC wapo Live muda huu*
Mzalendo namba moja Mh Rais John Pombe Magufuli atafungua Mkutano huo.Tayari wajumbe wameshaingia ukumbini huku burudani zikiendelea. Mwenyekiti wake Chama atawasili muda wowote kuanzia sasa ili kufungua Mkutano.
Mh JPM tayari ameshaingia ukumbini
Karibuni.
Bunge live hawataki ila mambo yao ya chama wanakuwa live tena vyama vingine hata coverage hawawapi, hii Tanzania unaweza pata mpaka magonjwa ya stress
 
Tumechoka na hiyo mikutano yao isiyoisha, mikutano isiyokuwa na tija hata kidogo kwa ustawi wa nchi hii zaidi ya kujazana ujinga, chuki, visasi na roho za mauaji dhidi ya wakosoaji wa serikali!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom