DOKEZO Mkurugenzi wa RITA shughulikia kero ya Huduma kuchelewa na majibu mabaya ya Maafisa wako

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nimekuwa nikipata shida sana kupata baadhi ya Huduma kutoka kwa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini – RITA (Insolvency and Trustee Registration Agency).

Mfano, wanasema baadhi ya huduma zinafanywa online, kila ninapojaribu kufanya maombi kwa njia ya mtandao inachukua muda mrefu kupata mrejesho na hata ukiwatafuta kwa ajili ya ufafanuzi maafisa wao wamekuwa wakitoa majibu mabaya.

Moja kati ya huduma nilizojaribu Kudhibitisha Wadhamini (Trustees), inacheleweshwa sana, mimi naishi mkoani, nilipofanya jitihada ya kwenda Dar napo nikazungushwa kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Huduma nyingine ni “Search ya Ndoa”, hii inachukua muda mrefu pia, unaweza kulipia lakini isifanyike kwa zaidi ya miezi mitatu.

Ukiwatafuta wanakuwa wakali na hawakusaidii, niwe mkweli sijawahi kuombwa Rushwa ila kero yangu nu ucheleweshwaji ulikithiri, inawezekana wanatengeneza mazingira ya hivyo lakini hilo sina uhakika nalo.

Uongozi wa RITA kuanzia kwa Mkurugenzi Mtendaji hii ni aibu kwenu mmeshindwa kuifanya RITA kutoka Huduma kwa wakati.

Huduma nyingine kama utoaji wa vyeti vya kuzaliwa angalau hazisumbui japo huko nako kuna malalamiko mengi. Tafadhali, naomba tulipoti hili suala ili liwafikie wahusika, binafsi nipo tayari kutoka ushahidi.

===

1705994107269.png
 
Hiyo changamoto mimi siyakutana nayo mtandaoni, bali nmekutanana palepale kwenye jengo lao la Rita tower,mtaa wa simu, dar es salaam, kiufupi baadhi ya watumishi haswa wa kike hawana majibu ya kuridhisha unapohitaji utatuzi wa changamoto unayokutana nayo. Nakumbuka mwaka 2022 nliend kufuatilia pale.

Tupo mstari ilipofika zamu yangu nmeenda kwa mtumishi anachezea ty simu takribani dakika 10 anaongea na simu na rafki yke,wanacheka na kupiga story Kana kwamba hakuniona pale, licha ya kumsalimia na kusisitiza anihudumie kwanza ila bado alijifanya kiziwi. Mpka alipojiskia ndipo nkapata huruma.

Jamani watumishi wa umma mna dhamana kwa wale mnaowahudumua na sio kuonesha dharau wala kujibu majibu mabayaa. Ile siku kwakweli nilijihisi vibaya sna
 
Back
Top Bottom