Hivi karibuni nilipata malazi yaliyonifanya nimtafute daktari mtaalamu pale Agha Khan Hospital. Nilichoshangazwa nacho ni utaratibu mpya nilioukuta pale. Baada ya kupokelewa nilitia sahihi ktk karatasi mbili tofauti. Moja ilionyesha malipo ya Tsh. 40,000 na nyingine Tsh. 29,000/=
Baada ya kuzisahini nilirudishiwa ile ya 40,000 na nyingine ikabakia pale. Baada ya kumwona Dkt aliniandikia dawa za mwezi mzima. Ktk dirisha la dawa nilipewa dawa za juma moja tu, maelezo ni kuwa bima yetu hakubali dawa za kiasi hicho kutolewa kwa pamoja. Nikapewa ushauri wa kurudi hospitali mara dawa ziishapo.
Dawa zilipokwisha nikarudi. Yaliyojitokeza; Ili kumuona dkt ye yote asiyemtaalamu ili aweze kuniandikia mwendelezo wa dozi Nilisahini kiasi cha Tsh. 20,000 karatasi moja na Tsh 19,000 karatasi nyingine, jumla Tsh.39,000!!!
Ajabu ni hivi dawa zenyewe zinazochukuliwa ni Vitamini C!!! Za siku saba tu.Ambazo kama nikinunua duka la dawa haifiki Ths 1,000/= La kusikitisha ni kuwa mchezo hata NHIF wanaujua kuwa AKH wanafanya hivi kwa wagonjwa bila kujali ugonjwa na umri wa mtu, lakini hakuna hatua yoyote inachukuliwa hata NHIF wanalijua jambo hili kuwa AKH wanafanya hivi kwawagonjwa bila kujali ugonjwa na umri wa mtu, lakini hakuna hatua yoyote inachukuliwa.
Lakini nilipofanya uchunguzi wa haraka haraka nikagundua kuwa ikiwa dkt wa mf. Mwananyamala Hosp akikuandikia kiasi hicho hicho cha dozi na ukienda ktk famasi zilizohakikiwa na NHIF, basi unapewa dozi kamili bila ya kukatwa katwa kama hapa AKH.
Pia hata NHIF wanalijua jambo hili kuwa AKH wanafanya hivi kwa wagonjwa bila kujali ugonjwa na umri wa mtu, lakini hakuna hatua yoyote inachukuliwa. Je, huu si mradi ndani ya mradi? Naomba maoni yenu