Mkurugenzi Mkuu ATCL: Hatuwezi kuweka wazi idadi ya abiria waliokata ticket za Dreamliner kwa sababu za kibiashara

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,034
144,387
Siku tatu kabla ya kuzinduliwa kwa safari za ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi amesema maandalizi yote yamekamilika.

Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 262, itaanza kupasua anga ya Tanzania Jumapili Julai 29, 2018 kwa safari za Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza.

Akizungumza na MCL Digital leo Alhamisi Julai 26, 2018 Matindi amesema kwa siku ndege hiyo itafanya safari mbili, moja asubuhi na nyingine jioni.

Kuhusu idadi ya abiria waliokata tiketi hadi sasa kwa ajili ya kusafiri na ndege hiyo ya kisasa, amesema jambo hilo haliwezi kuwekwa wazi kwa sababu za kibiashara.

Soma Zaidi:

Ukarabati uwanja wa ndege Mwanza mbioni kuanza

“Hayo hayawezi kusemwa kwa sababu najua wapinzani wetu nao wanasubiri kusikia hilo. Subirini siku hiyo mtashuhudia,” amesema Matindi.

“Ni ndege yetu na shirika hili ni la umma lakini hiyo haibadilishi sheria za mchezo, kwenye biashara sheria zinabaki vilevile. Nia yetu ni kufanya vizuri kwenye soko.”
Ndege hiyo iliyopewa jina la Kilimanjaro Hapa Kazi Tu iliwasili nchini Julai 8, 2018 saa 11:29 jioni na kupokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais John Magufuli.

Dreamliner inafanya idadi ya ndege ambazo zimeshanunuliwa na Serikali kufikia nne kati ya saba ambazo zinatarajiwa kununuliwa kwa lengo la kuifufua ATCL iliyokuwa na ndege moja pekee yenye uwezo wa kubeba abiria 51.

Ndege zingine tatu zilizowasili nchini ni aina ya Bombardier Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja.
 
Dar - Kil - Mza masaa 2.30 kwa nini wasifanye route 2 kwa siku?
 
Watu weusi uwa tunamatatizo sana kila kitu usiri. Unasikia waziri anasema tukitamka nyongeza ya mshahara kutakuwa na mfumuko wa bei, wachezaji wakisajiriwa napo usiri, madini hawataki ya kaguliewe na CAG napo usiri, ndege kusema idadi ya abiria napo usiri ngozi nyeusi tunamatatiza sana
 
Back
Top Bottom