Hii njemba labda ilipata mfadhaiko wa akili. Ngoja tuzione picha za huyo binti ambazo nadhani zitatoka hivi karibuni ili tuweze kujua sababu hasa ya kumfanya huyu jamaa afadhaike na kufanya aliyoyafanya.
Hii inasemwa kwamba ni moja ya mbinu za mchezo mchafu unaofanywa na raisi wa France Nicolas Sarkozy ambae umaarufu wake umezidi kudorora kuelekea uchaguzi wa rais nchini humo.
Bwana Dominique Strauss-Kahn ambae ana umri wa miaka 62 anatarajiwa kugombea uraisi nchini Ufaransa unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Strauss-Kahn alipata sifa mwaka 2008 kwa kuliongoza vema IMF kupita kwenye wakti mgumu kiuchumi na baade kwenye mwanguko mkuu wa kuchumi duniani "global recession".
Pia hivi karibuni mzee huyo mtaalam wa uchumi alibuni mpango wa kuzinusuru nchi kadhaa za Ula kama Ireland na Greece kuepukana na kufilisika kiuchumi kwa kuchangisha fwedha za kuweka uwiano unaoridhisha kwenye uchumi wa Ulaya.
Lakini huyu mzee ambae ameoa na ana watoto wanne, anapenda mabinti na pale binti yoyote anapoonesha dalili za kuvutiwa nae mzee huweweseka na ndio inasemekana mtego ukawekwa hapo.
Raisi Sarkozy aliposhinda uraisi alimpigia debe mzee huyu ili apate kazi IMF ikiwa ni kumuondoa kwenye ulingo wa siasa nchini Ufaransa.
Strauss-Kahn ambae aliwahi kuwa mhadhiri wa uchumi ni mjamaa na ni mwanachama wa chama cha Socialist na amewahi kuwa meya wa mji wa Sarcelles ambao umejaa wahamiaji. Pia amewahi kuwa waziri kwenye serikali ya raisi Francois Mitterrand.
hakubisha hodi ama kumjulisha ujio wake?maana ni VIP huyu...au aliingia kama guest zetu za uswaz??
Historia inatuleza, pindi unapokwenda kinyume na Masilahi ya wakubwa, kusukiwa zengwe huwa ni silaha mojawapo ya kukumaliza!!!, hususan zengwe hili la ngono ni tego gumu kweli kulivuka kwa wanaume Wengi!!!. anyway sijui A wala B ya hiyo ishu ya huyo jamaa, lakini usije ukakuta jamaa wamemlia timing kummaliza!.
Mwanaume kama unatembea umeishikilia mkononi vitu kama hivi lazima tu vitokee. Huyu mtu hakuna cha kusingiziwa wala nini, kwani ilishawahi kumtokea nyingine mwaka 2007.
Nyambala bolebole?
Kwa kweli inasikitisha sana kwa nchi kama tz kuweka uchumi wetu chini ya watu wenye poor judgement kama huyu bosi wa IMF namna ya kuendesha uchumi wetu badala ya watanzania wenyewe ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakipuuzwa na kuonekana hawana uwezo na watu wa IMF kuonekana kuwa ndio mwarobaini wa matatizo yetu ya kiuchumi. i hope kwa hili lilotokea Newyork labda huenda likawaamsha uzinginizini watu kama akina kikwete ambao wamekuwa wakiwategema sana judgement za watu kama hawa. wakati mtu akituhubiria namna ya kumsaidia mtu maskini wakati yeye mwenyewe analala kwenye hoteli chumba $3000 per night kwa pesa za walala hoi. kwa wale mnaotilia shaka mashtaka haya muelewe kuwa hii siyo mara yake ya kwanza kukamatwa na ishu kama hii na afadhali mara hii amefanyia USA kwa maana kama angefanyia unyama huu TZ angeweza ku get away with it easily na binti wa kitanzania angetukanwa hadharani tena LABDA na JK mwenyewe.
Mhhh!!! Bit strange and dodgy as well