Mkurugenzi huyu ameshindwa kazi!

PMNBuko

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
967
154
Kwa takribani siku 2 Mji wa Bukoba hauna usafiri wa Hiace kutoka na kuingia mjini.

Wenye magari hayo ya abiria wamegomea ushuru wa Tshs 2000 wanaotozwa kila gari linapopakia abiria stand.

Wanataka kulipa fedha mara moja tu, stand iboreshwe kwa kuweka huduma na miundombinu muhimu. Madai yao haya ni halali. Pia, sumatra nao hawakwepi hili kwa kutoibana Manispaa kutatua mgogoro huu.

Wananchi wanaingia gharama ya kukodi magari na hata kutembea kwa miguu kwa umbali wa kati ya km 3 hadi 10.
 
ndio mitanzania ilivyo. imepewa kazi haifanyi kazi. Mkurugenzi mzima anashindwa kutatua tatizo dogo tu mpaka mwakyembe aende.
 
Ndio faida za kumchagua gamba na kumuacha jembe LWAKATARE; huyo gamba mliempa siku hizi kazi yake kuruka na ndega za Tanapa tu amekwisha sahau alikotoka!!
 
Back
Top Bottom